Umoja wa wanawake katoliki ulimwenguni:kusikiza sauti za wote duniani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwakilishi wa Uchunguzi wa Wanawake Duniani na ripoti yenye kichwa: “Athari za UVIKO-19 kwa wanawake katika Bara la Amerika Kusini na Carribien”. Haya ni matukio makuu yatakayosikika siku ya Jumanne tarehe 14 Juni 2022, katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani (WUCWO/UMOFC). Ni mkutano wa kimataifa utakaokaribisha hotuba ya Kardinali Marc Ouellet, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu, Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte, rais wa Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini, Sr. Alessandra Smerilli, katibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu na wa Profesa Emilce Cuda, katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini.
Tukio hili limeandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Maaskofu la Amerika ya Kusini na kwa udhamini wa Mabalozi wanaowakilisha nchi za Argentina, Australia, Austria, Colombia, Haiti, Uholanzi na Uingereza katika jiji la Vatican. Madhumuni ya Taasisi ya Uchunguzi ya Wanawake Duniani yanahusishwa na changamoto muhimu: kutoa uonekanaji wa wanawake, hasa walio hatarini zaidi, ambao wanaonekana kwamba “hawaonekani”; kuuunda mikakati ya kichungaji, ushirikiano kati ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs); upyaishaji wa sera za umma na kuchangia ajenda ya kimataifa. Juhudi ya kufuatwa ili kukuza maendeleo shirikishi ya binadamu ya wanawake na yale ya familia zao, jumuiya na watu.
Athari za Uviko- 19 kwa wanawake wa Amerika Kusini na Visiwa vyake
Ripoti hiyo yenye kichwa “Athari za Uviko-19 kwa wanawake wa Amerika ya Kusini na Carribien" ilikuwa fursa ya kusikia sauti za thamani lakini mara nyingi zilizosahaulika kutoka bara hilo. Na ilikuwa uzoefu wa kusonga mbele. Haya ndiyo alisisitiza Maria Lia Zervino, rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani, akiongeza kuwa lengo sasa ni kuwasikiliza wanawake kutoka pande zote za dunia. Na kwamba sasa wanapoanza kufanya kazi barani Afrika, uwezekano unafungua wa kukusanya mateso na ustahimilivu wa wanawake wengi ambao wanaonekana kutoonekana katika ulimwengu wote. Monica Santamarina Noriega, mweka hazina mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Ulimwenguni, ameelezea Vatican News kwamba hali inayoashiria kukosekana kwa usawa kwa kiasi kikubwa inatoka kwenye ripoti, kuhusu janga hilo la uviko ambalo kiukweli limeonesha ukosefu wa usawa wa kijamii, kimuundo na kiuchumi, na kuzidisha ukosefu wa usawa kati ya wanaume na wanaume. Pia kumekuwa na ongezeko la ukatili dhidi ya wanawake. Katika kipindi hiki, huduma za afya kwa wanawake pia zimepungua na pengo la upatikanaji wa elimu limeongezeka.