Tafuta

Ukraine  Siku 100 za vita nchini Ukraine Ukraine Siku 100 za vita nchini Ukraine  

Siku mia moja za vita ni kusema "hapana" kwa kila vita vyovyote"

Uvamizi wa Urussi nchini Ukraine umekamilisha siku 100 na hauachi:siku za kifo na uharibifu,wakati hofu ya kuongezeka kwa migogoro inakua.Sasa ni rahisi sana kuzungumza juu ya uwezekano wa vita vya nyuklia.Lakini watu wanahitaji ishara za ujasiri wa amani.

Na Sergio Centofanti

Siku 100 tayari zimepita tangu mwanzo wa vita hivi vya wazimu: na hakuonekani  mwisho wake mbele. Hakika, badala yake wasiwasi pia inazidi kuongezeka wa mzozo na hata vita vya ulimwengu vya kinyuklia ambavyo haviwezi kutengwa. Inazungumzwa zaidi na zaidi. Kwenye Televisheni inaelezwa kuwa inatosha sekunde chache kuharibu miji mikubwa. Na sisi tunaizoea lugha hii. Itakuwa ni kuua ubinadamu.

Historia inatufundisha kwamba unapoanzisha vita vidogo haufikirii jinsi vita hiyo inaweza kuwa kubwa. Utaiona baadaye. Kiongozi anapoamua kuanzisha vita anatafakari ushindi wake anaoweza kuwa nao: lakini historia inatuonesha mwisho mbaya wa viongozi wengi hawa. Historia inatufundisha kwamba si mara nyingi hujifunza kutokana na historia. Na makosa hurudiwa, makosa ambayo ni hatari kwa wale wanaoyafanya na kwa bahati mbaya ni makubwa kwa mamilioni ya watu wanaoteseka.

Vita ni dhidi ya watoto

Wakati huo huo, uvamizi wa Urussi  uliopendwa na Putin unasababisha vifo na uharibifu nchini Ukraine: Magharibi ina wajibu wake katika kuzidisha hali ya wasiwasi katika eneo hilo, lakini shambulio la Kirussi halina uhalali. Watoto wanakufa, raia wanakufa, majengo ya makazi, hospitali, nyumba, shule, makanisa yanaharibiwa. Familia zimegawanyika, wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao wanafikia mamilioni. Hivyo maisha mengi yaliyo na urka na kuharibiwa nchini Ukraine. Nchi iliyoharibiwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Hata huko Urussi kuna watoto wengi wanaopelekwa kufa hatujui kwanini. Na ulimwengu umeathiriwa na uchumi ambao ulikuwa unaanza kupona kutokana na mapigo ya janga la uviko. Sasa pia kuna vita vya gesi, vita vya mafuta, vita vya nafaka: na kwa maskini kuna umaskini zaidi na njaa zaidi. Bila kusahau chuki inayokua, hisia za hasira, vurugu na kisasi ambazo huongezeka na kujiandaa kwa vurugu zaidi, malalamiko mengine, na huzuni nyingine.

Tunataka amani!

Vita ni wazimu, Papa Francisko  amesema mara kadhaa. Ni tukio lisilo na kurudi,  Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa amesema. Tunahitaji neno la amani, unabii ambao unaweza kusema kwa nguvu "basi inatosha" vita hivi na vita vyote vilivyosahaulika duniani: Siria, Yemen, Ethiopia, Somalia, Myanmar ... Tunahitaji ujasiri wa kutafuta njia ya kufanya hivyo katika uharibifu mwingi. Tunahitaji kupata ujasiri wa kuasi vita vinavyoamriwa na mtu fulani mwenye nguvu ambaye huwatuma wengine kufa. Je, itachukua vifo vingapi ili kuweza kusema "inatosha"? Ni lini watu watadamka na kusema wanataka kuishi kwa amani?

03 June 2022, 15:56