Ratiba ya maadhimisho ya Papa kwa mwezi Julai,Agosti na Septemba
Kuanzia tarehe 3 Julai, katika Dominika ya XIV ya mwaka C, wa kipindi cha kawaida cha mwaka, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican, saa 3.30 asubuhi, Baba Mtakatifu anatarajia kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya Jumuiya ya Wakongo Roma.
Tarehe 27 Agosti 2022 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa 10.00 jioni katika Kikanisa cha Kipapa, kutakuwa na Mkutano wa umma wa uundaji wa Makardinali wapya na kura juu ya baadhi ya mchakato wa kutangaza watakatifu.
Tarehe 28 Agosti 2022, katika Dominika ya XXII mwaka C, kipindi cha kawaida cha Mwaka, Baba Mtakatifu anatarajia kufanya ziara ya kichungaji huko Aquila Italia.
Tarehe 30 Agosti 2022 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican saa 10.30 jioni katika Kikanisa cha Kipapa, kutakuwa na Misa Takatifu kwa ajili ya kuwasimika Makardinali na Baraza la Makardinali.
Tarehe 4 Septemba 2022, katika Dominika ya XXIII ya mwaka C, kipindi cha Kawaida cha Mwaka, majira ya saa 4.30 asubuhi Baba Mtakatifu anatarajia kumtangaza Mtumish wa Mungu Papa Yoane Paulo I kuwa Mwenyeheri.