"Praedicate Evangelium" mahali pa kuwasili na kuondokea
Na Andrea Tornielli
Hatua ya kuwasili na kuondokea. Kiukweli ni kuanza tena. Kwa kuanza kutumika kwa Katiba mpya ya kitume "Praedicate Evangelium", kuanzia tarehe 5 Juni na sikukuu ya Pentekoste, inakalimisha njia ya mageuzi ambayo ilidumu karibu miaka kumi. Mchakato wa safari ambao umesindikizwa hadi sasa na upapa wa Papa Francisko ambao ulianza katika mijadala ya mikutano mikuu kabla ya uchaguzi mnamo 2013. Mageuzi hayo yanakuja baada ya yale yaliyofanywa na Yohane Paulo II (Pastor Bonus, 1988), ambayo nayo yalirekebisha yale yaliyotangazwa na Paulo VI (Universi regimini Ecclesiae, 1967). Kipaumbele cha Uinjilishaji na nafasi ya waamini ni mawazo makuu yanayounganisha Katiba mpya ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.
Kwanza kabisa, kuwa na mtazamo wa safari iliyofanywa tayari. Mageuzi zaidi ya lazima yanayohusishwa na habari za mahakama ambayo kwa chaguo la makusudi yalianza na taasisi za kiuchumi na kifedha ya Vatican. Mnamo mwaka wa 2014, Papa Fransisko alianzisha Baraza la Uchumi, ambalo lina kazi ya kusimamia usimamizi wa uchumi na kusimamia miundo na shughuli za utawala na kifedha za Mabaraza ya Curia Romana. Wakati huo huo, Papa Fransisko alianzisha Sekretarieti ya Uchumi, ambayo ni Baraza la Kanisa la Roma kwa ajili ya udhibiti na mwelekeo, inayosimamia kuratibu masuala ya uchumi na utawala wa Mamlaka ya Vatican na Serikali ya Mji wa Vatican.
Jukumu la wafanyakazi ambalo hadi sasa lilikuwa ni jukumu la Sekretarieti ya Nchi, sasa linahamishiwa kwenye Sekretarieti ya Uchumi. Pia kunako mwaka 2014, Papa alimkabidhi Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali jukumu la kufanya ukaguzi wa Baraza za Curia Romana. Taasisi zinazohusishwa au kutajwa na Makao Makuu na Tawala za Mji wa Vatican.
Hatua ya pili ilifanyika mnamo mwaka 2015, kwa kuundwa kwa Sekretarieti ya Mawasiliano, ambayo baadaye ilikuja kuwa Baraza la Mawasiliano, iliyokusanya vyombo 9 tofauti (kuanzia na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii hadi magazeti mbalimbali ya Makao Makuu Vatican, kuanzia Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii na uchapaji, Maktaba ya Uchapishaji wa vitabu na duka la Vitabu Vatican). Baraza jipya limekabidhiwa kwa uongozi wa Mwenyekitit Mlei tangu 2018. Kunako mwaka 2016 lilianzishwa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambalo liliunganisha uwezo na majukumu yaliyokuwa yanamilikiwa na Baraza la Kipapa la Walei na Baraza la Kipapa la Familia. Baraza huli lina uwezo mkubwa katika masuala yanayohusu kuhamaisha maisha na utume wa waamini walei, huduma ya kichungaji kwa vijana, familia na utume wake, ulinzi na tegemeo la maisha ya binadamu. Pia mnamo mwaka 2016, Papa alianzisha Baraza kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu. Ndani ya Baraza hilo liliunganishwa na: Mamlaka ya Baraza la Kipapa la Haki na Amani, Baraza la Kipapa Cor Unum, Baraza la Kipapa la Huduma ya Kichungaji kwa Wahamiaji na Wakimbizi na Baraza la Kipapa la Wafanyakazi wa Huduma za Afya (kwa ajili ya Huduma ya Kichungaji ya Afya). Kwa maanahiyo Baraza hili pia linawajibika kwa Caritas Internationalis.
Mnamo Novemba 2017, Papa pia alifanya mabadiliko kwenye Sekretarieti ya Vatican ambayo hadi wakati huo ilikuwa na sehemu mbili, ile ya Mambo ya Jumla (iliyoongozwa na Msaidizi) na ile ya Mahusiano na Mataifa (iliyoongozwa na Katibu wa Mahusiano na Mataifa). Kwa hakika Fransisko aliaanzisha sehemu ya tatu, inayoitwa Sehemu ya Watumishi wa Kidiplomasia wa Vatican, ili kuimarisha ofisi ya sasa ya Wajumbe wa Uwakilishi wa Kipapa. Sehemu hiyo, ambayo inategemea Sekretarieti ya Vatican yenye Katibu wake yenyewe, inataka kuonesha umakini na ukaribu wa Papa kwa wafanyakazi wa kidiplomasia. Inashughulikia masuala yanayohusiana na watu wanaofanya kazi au wanaojiandaa kwa ajili ya huduma ya kidiplomasia ya Vatican.
Hatua zaidi zimefanyika mnamo Februari 2022. Papa Francisko alirekebisha muundo wa ndani wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Motu Proprio akitenganisha waziwazi, na kuanzishwa kwa sehemu mbili tofauti, kwa ajili ya uwezo wa mafundisho na nidhamu, ya Sakramenti na kuwagawia kila mmoja katibu wake. Kwa hivyo Kardinali Mwenyekiti wa Baraza hilo atakuwa na manaibu wawili. Madhumuni ya mageuzi hayo ni kutoa umuhimu unaostahili pia kwa sehemu ya mafundisho na jukumu lake msingi katika kukuza imani, bila kuacha shughuli za kinidhamu, kuchukua nafasi ya nyuma, baada ya miongo kadhaa ambayo juhudi nyingi na rasilimali watu zimetumika kuchunguza kesi za unyanyasaji. Hakuna hata mmoja wa makatibu wawili wapya aliyeteuliwa kuwa askofu.
Kwa hivyo ilifikia mnamo 19 Machi 2022, kwa kuchapishwa kwa Katiba mpya, ambayo inajumuisha mchakato wa safari nzima iliyoelezwa hadi sasa na kuanzisha ubunifu mwingine unaokamilisha mageuzi. Muhimu zaidi: Baraza la Kwanza la Curia ni la Uinjilishaji ambalo linaunganisha Baraza la Unjilishaji wa Watu, na Baraza la Kipapa kwa ajili ya uinjilishaji Mpya. Uchaguzi huo unamaanisha umakini wa Papa unaotolewa kwa ajili tangazo la Injili. Upekee ni kwamba Mwenyekiti wa Baraza hilo anakuwa Papa mwenyewe, ambaye anazingatia mada ya uinjilishaji kuwa muhimu. Kwa njia hiyo atasaidiwa na wasimamizi wakuu wawili (mmoja kwa ajili ya sehemu ya masuala msingi ya uinjilishaji ulimwenguni; na mwingine kwa ajili ya sehemu ya uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya mahalia).
Mabadiliko ya pili yanahusu kuunganishwa kwa Baraza la Utamaduni na Elimu Katoliki ambalo litakuwa na Mwenyekiti mmoja. Jambo jipya la tatu la Katiba ni mabadiliko ya Sadaka ya Kitume, hadi leo hii ilikuwa Ofisi rahisi tu, na ambapo sasa inakuwa sehemu ya Baraza la Curia Romana linaloitwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma ya Upendo”. Jambo jipya la nne ni ufafanuzi ambao umetajwa kuwa sehemu ya Curia Romana na ambao hadi sasa uliitwa "Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu" sasa inakuwa "Sekretarieti Kuu ya Sinodi".
Jambo lingine jipya la Katiba linawakilishwa na ukweli kwamba wakuu wa Mabaraza ya Kipapa hata wale wa Mabaraza ya Kizamani hawatalazimika tena kuwa makadinali. Zaidi ya Kardinali Camerlengo, Makadinali wawili pekee waliotajwa katika "Praedicate Evangelium" ni Mwenyekiti wa Mahakama ya Saini ya Kitume, na mratibu wa Baraza la Uchumi. Papa pia alithibitisha kwamba nafasi za mapadre na watawa katika Curia zinaweza kurejeshwa kwa miaka mitano kwa kipindi cha pili cha miaka mitano, na uhamaji mkubwa na mwingiliano kati ya Roma na Makanisa mahalia.
Hatimaye, kuna kipengele muhimu cha Katiba mpya kinachokusudiwa kuwekea masharti, katika maendeleo yake ya baadaye, pia uthabiti wa maisha ya Makanisa mahalia na miundo yao. Baba Mtakatifu Francisko anakumbuka katika Dibaji ya Katiba kwamba “Kila Mkristo, kwa njia ya Ubatizo, ni mfuasi mmisionari kiasi kwamba amekutana na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu”. Hivyo ni ushiriki wa walei katika majukumu ya serikali na uwajibikaji. Ikiwa "mwamini yeyote" anaweza kusimamia Baraza au muhimili wa Curia Romana "kutokana na umahiri wake mahususi, mamlaka ya utawala na kazi maalum", ni kwa sababu kila taasisi ya Curia hufanya kazi kwa uwezo anaokabidhiwa kutoka kwa Papa.