Mkutano wa Familia:Bi Gambino kuna uhitaji wa kichungaji kwa miito tangu utoto!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna matarajio makubwa ya ufunguzi wa Mkutano wa X wa Familia, ambao unafanyika mjini Roma kuanziakuaniza Jumatano 22 hadi Dominika 26 Juni 2022 “Upendo wa familia: wito na njia ya utakatifu”, ndiyo Kauli mbiu inayoongoza toleo hili ambalo limeanza alasiri kwa Sikukuu ya Familia. Ni takriban wajumbe elfu mbili walioalikwa kutoka nchi 120, waliochaguliwa na Mabaraza ya Maaskofu, na Sinodi za Makanisa ya Mashariki na ukweli wa kimataifa wa kikanisa ambao wanawakilisha tukio hili kuu jijini Roma. Mkutano huu unafanyika katika wakati mgumu kwa ubinadamu, ulijaribiwa na janga na vita. Bi Gabriella Gambino, katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, muhamasishaji wa tukio hili amezungumza juu ya toleo hili na Vatican News kwamba baada ya mwaka mzima ambao wamejitolea kwa ajili ya uchungaji wa familia pamoja na kazi kubwa ambayo imefanywa, annaamini kwamba ni wakati wa kweli wa kuunda Kanisa pamoja na familia, wachungaji na familia pamoja. Hakika ni matumaini ya kukutana, matumaini ya kusikia maneno ya kutia moyo kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko ili, mwishoni mwa Mwaka huu wa familia, waweze kuendelea na safari pamoja. Anaaamini pia kwamba tumaini kubwa ni lile la kuanzisha michakato ya upyaishaji wa huduma ya kichungaji ya familia ili kuweza kusikiliza familia, na kuendelea kutembea nazo.
Katika toleo hili la Kongamano kwa maana sio kama makongamano yaliyotangulia kwa njia ya kitaaluma yenye maudhui ya mafundisho ya kitaalimungu zaidi lakini hasa itakuwa wakati wa kusikiliza na kukutana zaidi. Watoto wengi wa wanandoa waliopo pia kushiriki. Na hivyo ni muhimu sana kwa sababu kiukweli uchungaji wa familia ni utunzaji wa kichungaji wa familia. Familia nzima inaitwa kwa ajili ya tangazo la Kikristo na Bi Gambino anaamini kwamba leo hii moja ya changamoto kubwa kwa wao kama wazazi ni hasa ile ya kupeleka watoto wao katika ufahamu na pia ujasiri wa kumtangaza Kristo katika familia zao. Na pia kufundisha watoto kuiishi hata ikiwa wanaishi katika mazingira magumu wakati mwingine, ambayo hayafurahishi. Ni muhimu sana hata katika ngazi ya uchungaji, waanze kufanya kazi ya uchungaji unaovuka mipaka kati ya sekta mbalimbali, uchungaji wa watoto, uchungaji wa vijana, uchungaji wa wanandoa kwa namna ambayo mazungumzo thabiti na endelevu katika njia wito wa watu kutoka utoto hadi utu uzima yanatawala.
Malezi, usindikizaji, uhamishaji wa imani kwa vizazi vipya ni baadhi ya mada, lakini mada kuu ni tangazo la wito wa kila familia, wa kila mtu ndani ya familia. Familia ni njia ya utakatifu na utakaso ambayo kila mmoja wetu anayo mikononi mwake. Familia ni zawadi ambayo Bwana hutupatia. Bi Gambino anaamini neno msingi kuwa ni “uhalisia” yaani kuanzia kwenye uhalisia kwa sababu kila mmoja lazima aishi wito wake katika uhalisia wa kila siku anayoingia. Ni muhimu kuwafunza waundaji wanaojua jinsi ya kukabiliana na hali halisi ya familia za leo hii. Ni muhimu kwamba wasindikizane na familiahasa wanandoa vijana na wachumba katika hali halisi wanayoishi, kuanzia uhalisia wao, ili kutoka hapo waweze kugundua wito wao na kukutana na Kristo. Na ni muhimu tujifunze kueneza imani kwa vijana kuanzia uhalisia ambao wameingizwa ndani yake, kwa njia hiyo kuwa na ujasiri wa kushughulikia masuala ambayo yanawachosha sana leo hii, na ambayo wakati mwingine hawajajiandaa vyema. Bi Gambini amefikiria, kwa mfano, mazingira ya kidijitali ya vijana, mazingira ya mitandao ya kijamii, simu za kisasa, ambazo zinataka kuwa na ujuzi fulani wa uhusiano, kwa sababu kutoka hapo lazima waweze kufanya mazungumzo na vijana na kuwafanya wagundue imani, hata kutokana na mazingira hayo, amebainisha Bi Gambino.
Kwa maoni yake kuhusiana na shauku kuu walio yao familia ambayo Papa Francisko leo hii anakuwa na umakini sana ambao umekusanywa kupitia Wosia wake wa Amoris laetitia, uingiliaji mwingi juu ya mada ya familia, na Video nyingi zilizotengenzwa na Baraza lao la Kipapa, Bi Gambino amebainisha kuwa yeye binafsi anaamini kuwa unapendwa zaidi na Baba Mtakatifu ni ule wa kutangaza leo hii uzuri wa ndoa na familia. Hii ni kutokana na kwamba “Tunaishi katika mazingira ya kijamii ambapo vizazi vipya vinapata ugumu wa kuamini ndoa, wana changamoto nyingi zinazowazunguka zinazowapeleka kwenye njia nyingine na wanahitaji ushuhuda kutoka kwa familia zinazoaminika ambazo zinawaambia kuwa maisha ya familia yanajibu mahitaji ya utimilifu wa familia, mtu na maisha ya familia ambayo yamejengwa juu ya ndoa ya Kikristo na kwa hiyo familia imara, ni ile iliyojengwa karibu na imani katika Bwana ambaye kiukweli anapaswa na anakaa nyumba zeti na maisha yetu, na ni vizuri na inawezekana na si kitu kisichoweza kufikiwa”. Hii sio dhana potofu na ni kwa sababu hiyo kwamba moja ya mada ambazo zimechaguliwa katika Mkutano wa X wa Familia Ulimwengu za siku hizi ni mada ya utakatifu ili kuwa kielelezo cha baadhi ya familia takatifu ambazo tayari zimefunga mchakato huo wa safari hii mbele yao na inaweza kuwaoneesha kwamba inawezekana kushika ishara za uwepo wa Mungu katika maisha yao, katika uhalisia wanaoishi kila siku.
Hivi karibuni walichapisha hati kuhusu Taratibu za Katekesi kwa ajili ya maisha ya ndoa kama sehemu ya miongozo ya kichungaji kwa Makanisa mahalia iliyotayarishwa na Baraza la Walei, Familia na Maisha na kuwepo utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko. Kiini ni suala la kutekeleza katekesi halisi kwa familia: kabla, wakati na baada ya ndoa. Swali msingi katika ulimwengu wa leo hii ni hatari ya wanandoa kuachana daima inakuwa kubwa zaidi, ambapo Bi Gambino amebainisha kwamba ni kweli na anaamini kwamba hili ni jambo muhimu sana. Hati hiyo ilitamaniwa waziwazi na Baba Mtakatifu kwa sababu tunaishi katika enzi ambayo ndoa inahitaji kutangazwa kwa nguvu kubwa zaidi, kwa uwazi zaidi, lakini zaidi ya yote ni lazima ma ambayo itatangazwa kwa wakati. Kwa sababu hiyo anaamini kwamba moja ya vipengele vya kuvutia zaidi vya hati hiyo ni ukweli kwamba inapendekeza maandalizi ya muda mrefu kwa maisha ya ndoa. Hii ina maana hata kuzungumza na watoto kuhusu sakramenti ya ndoa katika mapito ya kufundwa kwa Kikristo, yaani, kuhakikisha kwamba wanasikia kuhusu ndoa, kwamba wanaona ushuhuda wa wanandoa ambao labda ni makatekista wao, wanaoshuhudia uzuri wa wito na kwamba labda Bwana pia aliwaandalia, lakini ambao ni wito na kuitwa.
Ni muhimu kwamba kuona katika Kanisa miito ya ndoa, kwa sababu haichukuliwi tena kuwa vijana wanaoaoana leo hii. Kipengele kingine muhimu sana ni kusindikiza hata baada ya ibada na sherehe ya ndoa na kwa hiyo kutekeleza huduma ya kichungaji ya kifungo chenye nguvu, kwa sababu wanandoa, hasa katika miaka ya kwanza ya ndoa, wanahitaji kusindikizwa. Hii ni miaka yenye ugumu zaidi wakati mwingine, na ni miaka ambayo wanandoa huanza kujuana, kukutana na shauku za kwanza, jitihada za kwanza, hata furaha za kwanza, lakini sio hizo tu. Kwa hiyo, panahitajika usindikizaji ambao hauwaachi peke yao, unaowafanya wajisikie kuwa sehemu ya jumuiya ya kikanisa na unaowasaidia kuondokana na awamu ya mgogoro kwa sababu awamu ya mgogoro ni awamu ya kawaida katika maisha ya ndoa ya watu wawili wanaoishi pamoja kwa muda mrefu, katika maisha yote, lakini wanandoa lazima wasindikizwe ili wajue jinsi ya kuishi majanga haya kama fursa za ukuaji na sio kama nyakati zinazoashiria majeraha yasiyowezekana kuyashinda.