Tafuta

Kipindi cha Sala kwa Wamonaki. Kipindi cha Sala kwa Wamonaki. 

Kwa kuanzisha Mashirika mapya ya Kitawa na Kazi za kitume ruhusu inaombwa kutoka Vatican

Kuanzia sasa na kuendelea,Askofu wa jimbo atatakiwa kuwa na kibali maalum kutoka Baraza la Mashirika ya Kitawa na vyama vya Kitume kabla ya kuanzisha vyama vya waamini ambavyo vina lengo la kuwa Shirika ya Kitawa au Jumuiya za Kazi za Kitume

Vatican News.

Kabla ya kuanzisha shirika la umma la waamini kwa nia ya kuwa Taasisi ya Maisha ya Kitawa  au Jumuiya ya Maisha ya Kitume chini ya sheria na  haki za Jimbo, Askofu wa Jimbo lazima apate kibali cha maandishi kutoka kwa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume.

Hivi ndivyo Papa Francisko aliamuru katika maandishi kuhusu vyama vya umma vya waamini katika mchakato wa safari, kufuatia na mkutano uliofanyika mnamo tarehe 7  Februari iliyopiti na  Kardinali João Braz de Aviz Mwenyekiti wa na Askofu Mkuu José Rodríguez Carballo,Katibu  ambao wote wawili wa Baraza la Kipapa la Mashirikia ya Kitawa na Kazi za Kitume.

Maandiko na utekekezaji huo umeanza kutimika tarehe 15 Juni 2022 na kuchapishwa katika Gazeti la Osservatore Romano ambapo ni mtazamo wa  sehemu ya sinodi iliyohamasishwa na Papa Francisko, inayokusudia kukuza ushirikiano wa karibu kati ya ofisi za Vatican  na maaskofu wa Majimbo katika kusikilizana, kama Baba Mtakatifu alivyosisitiza katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi zaKitume uliofanyika mnamo tarehe 11 Desemba 2021.

Usikilizaji na ushirikiano ambao unaoneshwa katika mchakato wa kufanya mang’amuzi na kusnidkiza kwa umakini maalum katika misingi ya hivi karibuni na aina mpya za maisha ya watawa, kama ilivyoelezwa katika Kanuni ya Sheria ya Kanoni kifungu cha (can. 605).

16 June 2022, 17:39