Kutoka kwa Papa,waendesha baiskeli wa “Mzunguko wa Italia kwa matibabu ya watoto"
Vatican News.
Waendesha baiskeli 5 vipofu ambao waliondoka siku ya Jumatano kutoka Dosson(Treviso) sanjari na waongozaji wao waliwasili katika uwanja wa Mtakatifu Petro saa 6 mchana baada ya kuendesha baiskeli kwa kilomita 700 kupitia Njia ya Francigena (hii ni njia ya kiutamaduni na ya zamani sana wanayopitia kila wakati wanahija mbali mbali kuja Roma). Waliosindikizana nao katika hatua ya mwisho kwa mfano njia ya Castel Gandolfo-Vatican, walikuwa waendesha baiskeli watatu 3: Emiliano Morbidelli, Simone Ciocchetti na Rino Alberto Bellapadrona kutoka Riadha ya Vatican/na waendesha Basikeli wa Vatican.
Aliyewakaribisha, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ni Michele Salata, mkuu wa kituo cha huduma ya watoto kilichofunguliwa mwezi Machi na Hospitali ya Bambino Gesù huko Passoscuro. Kwa hakika, waendesha baiskeli kutoka Veneto na Riadha ya Vatican wanaunga mkono kampeni ya “Mzunguko wa Italia” kuhusu matunzo ya tiba shufaa kwa watoto.
Jumatano tarehe 15 Juni 2022 katika katekesi ya Papa, waendesha baiskeli vipofu walikutana na Papa Francisko kwa kumwambia kuhusu uzoefu wao na mipango yao, pamoja na kampuni ya baiskeli ya Treviso ya DOPLA, ambayo imejitolea kukuza elimu ya baiskeli kwa watu wenye ulemavu na kuwashirikisha katika Mapngo wa “ We Bike” ambao ni uzoefu wa michezo unaojumuisha sana, katika kusaidia huduma shufaa kwa watoto wagonjwa.