Kard.Sandri:Mungu alinde vijana dhidi ya vurugu Ukraine,Siria na Ethiopia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mbele ya kukabiliana na kile kilichotokea na kinachotokea katika nchi ya Iraq, Siria, Ethiopia na Ukraine, na katiika mashirikika yote ya Roaco ni mojawapo ya majibu ambayo Mungu anakutana na watu wake yale ya upendo na Msamaria Mwema. Hivyo ndivyo Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, alisema katika mahubiri ya Ibada ya Misa Takatifu ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 95 wa Roaco (Mkutano wa Kazi za Misaada kwa Makanisa ya Mashariki), iliyoadhimishwa JUmanne tarehe 21 Juni katika Kikanisa Nyuma Mama ya Shirila la La Salle jijini Roma.
Kardinali wakati wa mahubiri hayo alikabidhi kazi ya mkutano huo kwa Mtakatifu Alois Gonzaga, mmoja wa walinzi wa vijana, ambaye kumbukumbu yake ya kiliturujia uahadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 Juni. Huyo siomtakatifu wa kuwaza katika vipicha kama inavyowakilishwa mara nyingi, lakini ni kijana, mtu mzima ambaye, wakati wa kukaa kwake Roma katika malezi kwenye Jumuiya ya Yesu, wakati wa mlipuko wa janga la wakati ule alifanya kila awezalo kusaidia maskini na wagonjwa, huku akibisha hodikwenye milango ya nyumba za wakuu aliokuwa akiwatembelea mara kwa mara kama mkuu wa baadaye. Kijana Gonzaga aliomba msaada ili kuleta faraja kwa waathirika wa tauni na, wakati wa kumbema mmojawake mabegani wameke naye aliambukizwa hadi akafa muda mfupi baadaye.
Alois Gonzaga alikufa kama shahidi na bingwa wa upendo alisema Kardinali Sandri. “Kwa maana hiyo alikabidhi kazi ya siku hizo za mkutano kwa maombezi yake hasa kuomba awalinde vijana wa Makanisa ya Mashariki ya Kikatoliki katika mazingira magumu ya ghasia na vita, hasa Ukraine, Siria na Ethiopia, na wale wote wanaoteseka na bado wanaendelea kuteseka na matokeo ya janga ambalo limeikumba dunia katika miaka ya hivi karibuni.
Kardinali akuchambu masomo ya siku yaliuoongoza Liturujia na hasa somo la kwanza likisimulia juu ya tishio la mfalme wa Ashuru ambaye alitaka kutiisha ufalme wa Yuda, Kardinali alisisitiza kwamba “Bwana Mungu pekee ndiye mfalme. Kila nguvu ya mwanadamu ambayo kupitia itikadi nyingi zilizofichika inajidai kuwa ya milele au iliyowekewa nguvu ya kimungu inakusudiwa kuanguka”. Mwenyikiti wa Baraza la Kipapa akigeuzia mtazamo kwenye kwenye changamoto za wakati huu alisema Michezo iliyoingiliana ya nguvu, udanganyifu wa uweza wote, ambao una alama moja ya kuzidisha hesabu na maumivu ya walio wadogo na maskini; wanafanya watoto kulia, wakiwaacha mayatima, wanatawanya familia kwa kuwalazimisha kuacha nyumba zao, kubaka wanawake kwa kuwaharibu sura, kujaribu kuingiza ndani yao utawala wa watu wengine kwa bahati mbaya zaidi . Mbele ya watu hawa wanaoteseka, Kanisa linaonesha na litaendelea daima kuonesha ukaribu wake: “Tunaishi katika upendo kwa sababu tulipendwa kwanza na tunapendwa kila siku, na hatuwezi na hatutaki kusahau hili”.