Kard. Gambetti:Hata sisi tunaalikwa kugeuka kuwa Ekaristi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Alhamisi tarehe 16 Juni 2022 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa kuu la Vatican, ameongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Maadhimisho ya Corpus Domini yaani Mwili na Damu ya Yesu Kristo iliyofuatiwa na maandamano ya Ekaristi ndani ya Kanisa kuu lenyewe. Katika mahubiri yake Kardinali Gambeti amesema “Yesu anatushika mkono ili kutusindikiza kugundua njia ya Uzima na kushiriki nasi. Habari njema ya upendo kamili na wa kibinafsi ililetwa na Yesu hasa aliposema kuwa “huu ni Mwili wangu ambao ni kwa ajili yenu na habari hii si kuitazama kama wapokeaji wa upendo huu tu, lakini pia kama wahusika wakuu kama asemavyo Mtume Paulo, kwamba tumeitwa kuwa Ekaristi kama Yesu anayerudia kusema kwamba; ‘Tufanye hivi kwa ukumbusho wangu’.
Kadinali Gambetti ameonesha kwamba sisi pia hupinga kuhusika wakati linapotugusa jambo fulani katika mwili, katika mifuko yetu, katika mapendeleo tunayofurahia. Tatizo ni imani ndogo. Ni kana kwamba wanafunzi walikuwa wamemwambia Yesu hivi: ‘Tazama, haiwezekani kutambua ulichotuomba, umetufanya kupita kiasi. Au kwa maneno mengine: 'Ulikosea, hujui unachosema'. Hii pia hutokea kwetu, kwa mfano, wakati kwa makisio yetu au hukumu zetu tunapowanyima wengine sifa, hasa wale waliowekwa kwenye mamlaka, tangu utoto, wazazi, maprofesa, mameneja, watawala, maaskofu, Papa, Mungu. Badala ya kutafuta uhalali wa kutohusika, tunahitaji kujiuliza ni nini Mungu anatutaka tufanye, na baadaye ni kutii tu. Hivi ndivyo wanafunzi walivyofanya, wakijishinda wao wenyewe na kutegemea kile ambacho Yesu aliamuru. Na kwa maana hiyo hutokea vya kushangaza.
Kardinali Gambeti aidha amesema : "Tunapoadhimisha Ekaristi hatuna nia ya kukumbuka tukio tu, bali tuko tayari kuwa sisi wenyewe kumbukumbu hai ya Yesu na kamwe tusiharibu ukuu wa upendo huo, ili kamwe kusijitenge na njia ya Uzima wa Milele. ‘Corpus Domini’, yaani Ekaristi au Mwili na Damu ya Yesu Kristo ni shule ya Yesu kwa sababu Yesu anatushika mkono kama alivyofanya na wanafunzi na kutuongoza kwenye maisha haya kamili na ya upendo ambayo hupitia mabadiliko halisi kutoka katika mkao wa kujifikiria wenyewe tu ili kuweza kwenda kwa ndugu" alisema Kardinali huku, akikumbusha jinsi ambavyo Mtakatifu Paulo alisema kuwa: “Nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapelekeeni”, kwa maana hiyo na sisi pia tunaitwa kuwa Ekaristi kama Yesu, kuwa kumbukumbu hai ya Yesu kwa mwito wa kushuka katika ubinadamu, tukiacha nyuma kila aina ya utukufu wa kidunia, kijamii, kibinafsi, ili kamwe kutokuathiri ukuu wa upendo na tusishindwe katika upendo , yaani,kuishi maisha ambayo Yesu alishiriki nasi.