Tafuta

2022.06.23 Kardinali  CZERNY aliongoza mkesha wa sala. 2022.06.23 Kardinali CZERNY aliongoza mkesha wa sala. 

Kard.Czerny:utawala wa mabavu wa mwanadamu juu ya mwanadamu hutengeneza kuzimu

Katika mkesha wa sala ulioongozwa na mada:“Kufa kwa matumaini" katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria huko Trastevere,katika Siku ya Wakimbizi Duniani,,kwa kumbukumbu wale ambao mwaka huu walikufa katika Bahari ya Mediterania,Kardinali Czerny alisema wlikuwa wakikimbia migogoro,kutofautiana na kutojali.Wito wake ni kujiweka huru dhidi ya upotovu wa uweza,kwa kutazama nguvu'ya Mungu tu kwani msingi ni kushiriki enzi kuu yake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu Kardinali Michael Czerny aliongoza mkesha wa sala uliokuwa unaongozwa na mada “Kufa kwa matumaini, uliofanyika Alhamissi jioni  tarehe 23 Juni 2022 na Jumuiya Mtakatifu Egidio na Mashirika mengine katika Kanisa kuu la Mtakatifu Maria huko Trastevere Roma katika fursa ya Siku ya Wakimbizi Duniani. Katika mahubiri yake alisema inawezekana kufa na matumaini, au kwa matumaini. Kihusishi kimoja hubadilisha kabisa mtazamo. Tukikumbuka majina ya wale ambao, kwa mara nyingine tena mwaka huu, katika bahari ya Mediterania wamepoteza maisha na ndoto zao za uhuru kutokana na kukosekana kwa usawa, migogoro na kutojali. Kardinali amesema kwa upande mmoja, uwezo wa Bwana na kwa upande mwingine, unaotumiwa na mwanadamu ambaye, ikiwa anapoteza ufahamu wa uhusiano na Baba, ikiwa ametengwa na Muumba wake, hatambui zaidi kuwa ameitwa kulinda udugu na viumbe.

Hatari ya kutumia nguvu huchosha

Kardinali Czerny amebainisha hata hatari ya kutumia nguvu kama ilivyobainishwa ambayo huchosha na kuwachosha na  hupelekea juu na kutofautisha, hutenganisha, hukandamiza, na baadaye  huangusha. Akienda mbali zaidi  alisema kwamba inafikia hata utawala wa mabavu kuwadumbukiza kuzimu kwa wale wanaoteseka, lakini pia kuwatenga, kuwaondoa, kuwafunga wale wanaoishikilia. Tabia za kibinadamu hupotea, na kila mmoja wetu ni mtoto na ndipo wakati mwingine anakuwa mnyama na shetani. Yesu hakuwa kwa kila kitu na ni kinyume cha kila kitu, yeye haoni kila kitu na kila neno kuwa zuri, badala yake ana utambulisho, anafungua njia mpya, anaweka nafasi kwa mambo ya wakati wote, lakini anayafanya kama  vile hatujawahi kuona.

Yesu alikataa cheo

Katika kifungu kingine muhimu cha mahubiri ya Kardinali Czerny, ambacho kinakumbuka jinsi  ambavyo Yesu alikataa cheo cha kuwa mfalme, kuwazuia pepo wasimwasilishe kama Mwana wa Mungu. Hivyo alisema mwaliko kwa Wakristo kumfuata Kristo kwa kuchukua msalaba wao bila kuacha wengine,  na majukumu yao. Hata tukitupwa na wale wanaoitawala dunia, au ndoto zetu zikivunjwa, hakuna kitakacho kamilika ni mwito wake Kardinali kwa sababu pembezoni kuna tofauti kubwa. Vile vile alisema lakini si kwa bahati kwamba ‘ulimwengu mpya’ ulianza pale pale Nazareti, nje kidogo, na pale Kalvari, nje ya malango ya jiji.

Kukiri imani kwa mdomo tu haitoshi

Kardinali Czerny akiendelea alisisitiza kuwa Bwana ndiye hutoa nafasi, hufurahi kushiriki ukuu wake. Mbingu yake ina watu wengi na  sio kwa njia ya mahakama, lakini kama udugu uliokamilika. Huu ndio mfano wa kujumuisha. Kukiri imani kwa midomo tu haitoshi kwa sababu ni matendo ya upendo ambayo yanafanya kazi. Udugu unaotufanya kutawala, kifungo ambacho Bwana atatusukuma ili kukaa karibu naye, ni kukua pamoja na matendo ya huruma. Ni kazi ambayo kila mmoja ana uwezo wake, anatia alama tena huku akiangalia hilo, kwa matumaini. Mkesha wa sala ni tukio lingine la kuwakumbuka waathirika wote wa hali duni ya nguvu. Kila mmoja ana jina lake, kuwakumbuka watu hawa kwa majina ni ishara inayotaka kuwapa hadhi. Yeyote anayelikana jina hilo, anafanya uovu ambao unajitokeza katika miundo ya dhambi, alisisitiza Kardinali.

Ibilisi anapendekeza kuchukua njia ya mkato

Kardinali hatimaye alisema kwamba ibilisi anapendekeza kwa hila kuchukua njia za mkato; anaahidi utawala mkubwa na wa haraka, akitaka kutuepusha na dhana ya safari na makabiliano na ndugu. Kuepuka kwenda sambamba na jaribu hilo kinyume chake  kunamaanisha kutazama tena safari ya Kristo ambayo ina thamani ya juu ya kibinafsi, lakini inazalisha uzuri, furaha, umoja. Kardinali Czerny alisema: “Kutuweka huru kutokana na udanganyifu wa uweza hutufunga kwa kina sana, hutuweka huru kichwa na moyo, ili tuweze kupigwa na kile kilicho mbele yetu kama wito, kama fumbo la kubisha hodi”.

24 June 2022, 16:25