Tafuta

2022.05.19 Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Ukraine 2022.05.19 Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Ukraine 

Ziara ya Askofu Mkuu Gallagher katika utume nchini Ukraine

Katibu wa mahusiano na mataifa anaendelea kushuhudia ukaribu na mshikamano wa Papa Francisko na watu waliokumbwa na vita. Jumatano alikuwa katika mji wa Lviv, Alhamisi aliwasili katika mji wa Kiev.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa, aliendelea siku ya pili ya utume nchini Ukraine ambaye aliwasili nchini humo kushuhudia ukaribu na huruma ya Papa Francisko kwa watu ambao wamekuwa vitani kwa miezi hii, tangu tarehe 24 Februari iliyopita. Katika mji mkuu wa Kiev, alisimama na  mikutano mingi ya kitaasisi na kutembelea sehemu mbali mbali ambazo zimekuwa alama za ukatili wa vita ambavyo bado vinaendelea.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Katika mazingira ya ushiriki mkubwa na kutafakari, siku ya kwanza ya ziara ya Askofu Mkuu Gallagher, tarehe 18 Mei 2022 aliyopokelewa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki wa Lviv, Mieczysław Mokrzycki, iliisha. Askofu Mkuu huyo aliweza kutembelea vituo viwili vya watu waliokimbia makazi yao ambavyo, katika nyakati ngumu zaidi, vilihifadhi zaidi ya wakimbizi 500. Askofu Mkuu Gallagher alipeleka upendo, ukaribu na mshikamano wa Papa kwao kwa sababu ya mateso ya uchungu ambayo mzozo unaoendelea kusababisha, akitumai kuwa amani itarejea mapema karibuni kwa nchi yote ya Ukraine.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Miongoni mwa mikutano ya kwanza iliyofanywa na Askofu Mkuu Gallagher pia ule wa viongozi wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la mji huo ili kusisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kiekumene katika mchakato mgumu wa ujenzi mpya unaoingoja nchi hiyo katika siku za usoni. Kabla ya kuondoka, alitaka kubariki jiji lote la Lviv kutoka kwa mtaro wa jumba la askofu mkuu wa jiji hilo, ambalo licha ya utulivu wa dhahiri linaendelea kubaki lengo linalowezekana la milipuko ya mabomu, kama inavyokumbukwa na kengele za kuzuia ndege mara kwa mara mchana na usiku.

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

 "Mgogoro mkubwa wa kibinadamu,  ndivyo amesema Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa anavyosimulia hisia za kwanza za safari yake katika nchi ambayo imekuwa na vita kwa muda wa miezi mitatu iliyopita: kwa bahati mbaya, baada ya muda, uchovu unachukua nafasi katika kusaidia watu, katika shida, lakini Kanisa linasisitiza juu ya kusaidia watu na wito wa amani. Kusudi kuu ni kurudisha ziara iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine, Bwana Dmytro Kuleba, wakati fulani uliopita alifika Vatican. Akiendelea kufafanua kuhusu ziara hiyo amesema Askofu Mkuu Gallagher amesema kwa maana hiyo: “Nilimwambia nitakuja lakini haikuwezekana katika miezi ya hivi karibuni, ndipo vita vilipoanza na tukapanga tarehe mwanzoni mwa mwezi huu, lakini kwa bahati mbaya niliambukizwa Uviko hivyo tarehe hiyo ikahairishwa. Tumeweka mipango ya Ijumaa tarehe 20 Mei  huko Kiev na ndivyo tutakavyofanya, lakini kama kila mtu anajua ni vigumu sana kufikia Ukraine, Kiev na Lviv kwa wakati huu, inachukua muda lakini hii pia inaruhusu sisi kufanya fanya ziara na kuzungumza na watu kadhaa. 

Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine
Ziara ya Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Mataifa huko Ukraine

Mwakilishi wa Vatican akiendelea na kueleza amesema:"Tulikutana na Kanisa la Kilatini, Kanisa la Kigiriki-Katoliki, tulitembelea baadhi ya majengo ya kikanisa ambayo yanahifadhi wakimbizi kama vile nyumba ya watawa na parokia. Nilifurahishwa sana kuona jinsi Kanisa limeitikia mzozo huu mbaya wa kibinadamu. Ni Kanisa linalojilojishughuliza kabisa na watu wake na linalojaribu kujibu mahitaji, kusaidia kila mtu, si tu Wakatoliki bali pia wa dini nyingine. Naona kuna mvutano, ukosefu wa usalama miongoni mwa watu kwa sababu hatujui nini kitatokea huko mbeleni.”

20 May 2022, 10:37