Tafuta

2022.05.12  Askofu Edgar Peña Parra alizindua makao makuu ya shughuli za WYD 2023 huko Lisbon 2022.05.12 Askofu Edgar Peña Parra alizindua makao makuu ya shughuli za WYD 2023 huko Lisbon 

Wasimamizi 13 wa Siku ya Vijana duniani(WYD)huko Lisbon

Maisha ya Kristo yanajaza na kuwaokoa vijana wa kila zama.Haya yanashuhudiwa na watakatifu wasimamizi 13 wa Siku ya Vijana Duniani(WYD)ijayo ambayo itaadhimishwa mjini Lisbon 2023.Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican imetoa uwasilishaji wa sura hizi zilizoandikwa na Patriaki wa Lisbon,Kardinali Manuel Clemente na kuingizwa kama utangulizi wa kitabu kilicho chapishwa na Toleo la Mtakatifu Paulo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani itakayofanyika huko Lisbon nchini Ureno kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023 yanaendelea, ambapo kila mji wa Ureno umechagua watakatifu wasimamizi ambao ni kumbu kumbu katika kila Jimbo. Huu ni ukweli ili kuwasaidia washiriki wa siku ya Vijana ijayo kwa maana hiyo watapewa mfano wa wenzao, wenyeheri kama vile Joan wa Ureno, binti wa Mfalme Alfonso wa V, ambaye alipendelea maisha ya utawa wa ndani; kijana Mjesuit Giovanni Fernandes aliyeuawa shahidi mwaka 1570 nje ya Visiwa vya Canary alipokuwa akielekea Brazili kama mmisionari; Maria Clara wa Mtoto Yesu, kijana wa familia ya kitajiri ambaye, baada ya kubaki yatima, aliamua kuwa mama wa waliosahaulika kwa kuanzisha Hospitali ya Kifransiskani ya Mama Bikira Mkingiwa.

Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati  pia anaungana na Walisbone ambao mchakato wa kutangazwa kuwa mtakatifu unaendelea. Yeye kwa kupanda Milima mirefu ya Italia na kuwahudumia maskini, aliishi Injili kwa furaha, nguvu na mapendo hadi kifo chake huko Torino akiwa na umri wa miaka 24 tu. Mwenyeheri Marcello Callo, skauti, aliyefariki mnamo mwaka 1945 katika kambi ya mateso ya Mauthausen ambako alitekeleza utume licha ya hali ngumu ya kambi ya mateso na Mwenyeheri Chiara Luce Badano na Carlo Acutis wote wawili  waliishi kwa na ugonjwa na kufa wakiwa ni vijana tu na waliweza kuishi mateso pamoja na Kristo Msulubiwa, wakitoa ushuhuda wa imani katika siku zetu.

Msimamizu Mkuu hata hivyo ni Bikira Maria, kijana mwanamke ambaye alikubali kuwa Mama wa Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu. Maria ni  yeye ambaye anapeleka Yesu kwa wengine na ni kielelezo hata leo hii katika ulimwengu unaongoja tangazo la Wokovu wa Kristo. Miongoni mwa mashujaa wa imani wamo hata Mtakatifu Yohane Paulo II, Mwanzilishi wa Siku ya Vijana duniani ( WYD), Mtakatifu Yohane Bosco,  mwalimu na mlezi wa vijana, Mtakatifu Vincent, shemasi na mfiadini wa karne ya sita na baadaye kwa watakatifuwalioondoka huko Lisbon kupelekea Injili duniani, kama vile Mtakatifu Anthoni, Mtakatifu Bartolomeo shahidi na Mtakatifu Yohane wa Brito.

19 May 2022, 10:21