Rozari ya Amani,Papa atafunga mwezi wa Maria katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuomba kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria dhidi ya vita vya wazimu, kwa sababu "hakuna lisilowezekana kwa Mungu". Kwa mara nyingine tena Papa Francisko atafanya hivyo, kwa njia ya sala ya Rozari takatifu pamoja na waamini wa ulimwengu kwa kushirikiana na madhabahu mengi ya ulimwengu kuomba neema ya kisitisha vita na matukio yanayohusiana na vurugu duniani. Itakuwa ni hitimisho la mwezi Mei uliowekwa kwa ajili ya Maria na ambapo Papa Francisko alikuwa ameufungua kwa kuwaomba waamini wote kusali Rozari kila siku kwa kumwomba Malkia wa Mbingu na wa amani. Baraza la Kipapa la kuhamasisha Uinjilishaji Mpya limetoa taarifa kuwa tarehe 31 Mei, saa 12:00 jioni masaa ya Italia, mbele ya Picha ya Bikira Maria Malkia wa Amani kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Maria Mkuu, Papa Fransisko atasali sala ya Rozari pamoja na shauku ya"kutoa ishara ya matumaini kwa dunia nzima hasa kwa wanaosumbuliwa na migogoro nchini Ukraine, na waliojeruhiwa na vurugu ya zilizogawanyika vipande vipande duniani kote.
Kwa hiyo kutakuwa na aina mbalimbali za watu wanaowakilisha Watu wa Mungu: wavulana na wasichana ambao wamepokea Komunyo ya kwanza na Kipaimara, Skauti, familia za Jumuiya ya Kiukreinezilizopo Roma, wawakilishi wa Vijana wa Ardente Mariana (GAM), kikosi cha ulinzi cha Vatican na Walinzi wa Kipapa wa Uswisi na parokia tatu za Roma zilizowekwa wakfu kwa Bikira Maria Malkia wa Amani, pamoja na washiriki wa Curia Romana. " Kama ishara ya ukaribu na wale walioathiriwa zaidi na athari za mzozo katika moyo wa Ulaya, kwa mujibu wa taarifa imesema "walialikwa kusali makumi ya Rozari: familia za Kiukreine, watu wanaohusishwa na waathirika wa vita na Kundi la mapadri. Aidha Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya limesema ishara nyingine muhimu ya ushiriki wa kimataifa ni wa ana kwa hana lakini pia kupitia njia ya mtandaoni kwa kuunganishwa na madhabahu ya Mama Maria ulimwenguni yaliyo katika nchi ambazo wameathirika na vita au na ukosefu mkubwa wa utulivu wa kisiasa.
Madhahau hayo yatakuwa ya Iraq, Siria, Ukraine, Bahrain na tena na madhabahu ya kimataifa ya Mama Yetu wa Amani na Yesu Mwokozi; Madhabahu ya Jasna Góra, Poland; Madhabahu ya Kimataifa ya Mashahidi, Korea; Nyumba Takatifu ya Loreto, Italia; Bikira Mwenyeheri wa Rozari Takatifu, Pompei; Madhabahu ya Kimataifa ya Mama yetu wa Knock Ireland; Mama yetu wa Guadalupe; Mama yetu wa Lourdes. Na Waamini wanaalikwa kusali na kuunga mkono Baba Mtakatifu Francisko katika siku hiyo.