Tafuta

Papa Francisko amekutana na Rais wa Macedodia ya Kaskazini Bwana Dimitar Kovachevski. Papa Francisko amekutana na Rais wa Macedodia ya Kaskazini Bwana Dimitar Kovachevski. 

Papa amekutana na Rais Dimitar Kovachevski wa Macedonia Kaskazini

Kati ya mikutano ya kwanza ya Papa Francisko ya Jumatatu 23 Mei 2022,alikutana na Rais wa Jamhuri ya Macedonia Kaskazini Bwana Dimitar Kovachevski.

Vatican News

Ni nusu saa ya mkutano siku ya Jumatatu 23 Mei 2022,  kati ya Papa Francisko na Bwana Dimitar Kovachevski, rais wa serikali ya Jamhuri ya Macedonia Kaskazini. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, imesema pamoja na mkutano wao wa faragha wamehitimisha kwa kubalishana zawadi ambapo Rais Kovachevski alimpatia Papa Francisko nakala ya sehemu ya Eulogia ya Clement wa Ohrid, rozari yenye  lulu ya Ohrid.

Papa amekutana na Rais wa Macedonia Kaskazini
Papa amekutana na Rais wa Macedonia Kaskazini

Pamoja na  zawadi nyingine Papa amempatia Rais wa Macedonia Ujumbe wa Amani wa mwaka huu na Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu.

Papa amekutana na Rais wa Macedonia Kaskazini
Papa amekutana na Rais wa Macedonia Kaskazini

 

23 May 2022, 16:54