Papa akutana na Waziri Mkuu wa Bulgaria
Vatican News
Katika mkesha wa Siku ya Watakatifu Cyril na Methodius, watakatifu wanaoheshimika sana nchini Bulgaria kwa elimu na utamaduni wa Kibulgaria na fasihi ya Kislaviki iliyopangwa kufanyika 24 Mei 2022, Jumatatu asubuhi 23 Mei uwakilishi kutoka nchini humo ukiongozwa na Waziri Mkuu Kiril Petkov umepokelewa mjini Vatican na Papa Francisko.
Imekuwa ni zaidi ya robo saa ya mazungumzo ya faragha kati ya Papa Francisko na Waziri Mkuu, ambapo kumekuwapo na nafasi ya kubadilishana zawadi kwa kawaida. Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, kwa upande wa Kibulgaria,walileta sanamu za pango zilizotengenezwa kwa vitambaa vya sufu kutoka katika Kituo cha "Kzaliwa kwa Kristo", kinachohusiana na Kanisa la katoliki la Mitume la Kanisa la Byzantine-Slavic huko Sofia, na Kapeti la Kiutamaduni la Chiprovtsi.
Wakati Papa Francisko altoa zawadi ikiwa ni pamoja na nakala ya Ujumbe wa Amani kwa mwaka huu na Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu.