Tafuta

Padre Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp., ni Askofu moya  wa Jimbo la Dolisie, Congo Brazzaville Padre Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp., ni Askofu moya wa Jimbo la Dolisie, Congo Brazzaville 

Padre Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp.,ni Askofu mpya wa Dolisie

Papa amemteua Padre Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp., kuwa Askofu wa Jimbo la Dolisie nchini Congo Brazzaville na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu nchini Jamhuri ya Congo na Mratibu wa Umoja wa Mizunguko ya Kiroho nchini Congo na Afrika ya Kati (UCSAC).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu amemteua Padre  Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp., kuwa Askofu mpya wa  Jimbo la Dolisie huko Congo Brazaville  na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu nchini Jamhuri ya Congo na Mratibu wa Umoja wa Mizunguko ya Kiroho nchini Congo na Afrika ya Kati (UCSAC). Padre Toussaint Ngoma Foumanet, C.S.Sp, alizaliwa tarehe 1 Novemba 1975 huko Sibiti,  Jimbo la  Nkayi.

Mwaka 1988 alijiunga na  Shirika la Roho Mtakatifu (Spiritans). Kuanzia 1999 hadi 2002 alisoma falsafa huko Libreville, Gabon, tangu 2002 hadi 2003 alifanya unovisi huko Mbalmayo, Cameroon, na kutoka 2004 hadi 2008 alisoma taalimungu  katika Taasisi ya Mtakatifu  Cyprien huko Douala. Alifunga nadhiri za daima mnamo tarehe 14  Septemba 2007 huko Ngoya, Kameruni, na akapewa daraja la Upadre mnamo tarehe 26 Julai, 2008 huko Pointe-Noire, nchino Congo Brazzaville.

Maaskofu Katoliki wa Congo Brazzaville
Maaskofu Katoliki wa Congo Brazzaville

Baada ya kupewa daraja la upadre  alishika nyadhifa zifuatazo: Mshauri wa Mkuu wa kanda , Paroko wa Parokia (2008-2009) na Paroko wa Roho Mtakatifu (2009-2011) wa Roho Mtakatifu huko Pissa, Jimbo la Mbaïki, Jamhuri ya Afrika ya Kati; Mkuu wa Mbaïki na masomo ya sheria katika Chuo Kikuu cha Bangui (2009-2011); Paroko wa wa mama Yetu wa Afrika , katika Jimbo Kuu la Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati; Msaidizi wa Kwanza wa Kanda kusimami wanashirika (2011-2016); Mkuu wa Mama Yesu wa Afrika (2013-2016). Kuanzia 2016 hadi sasa amekuwa Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu (Spiritans) nchini Congo na Mratibu wa Muungano wa Mizunguko ya Kiroho ya Afrika ya Kati (UCSAC). Na zaidi aliwahi kuwa Rais wa Baraz ala Wakuu wa Shirika Roho Mtakatifu Afrika Madagascar (2017-2019); Paroko wa Mtakatifu Kisito Makélékélé (2018-2019), Parokia wa Parokia ya Mtakatifu Grégoire de Massengo (2019-2020) na Paroko wa Parokia ya Mama Yesu wa Ushindi huko Brazzaville (2020-2021).

11 May 2022, 17:57