Mwezi wa Maria katika Kanisa Kuu la Kipapa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika fursa ya Mwezi Mei, ambapo Watu wa Mungu hujikita kwa namna ya pekee kwa ibada ya Bikira Maria, Vikarieti ya Vatican na Parokia ya Mtakatifu Petro inaanzaa mfululizo wa matukio ya kuadhimisha ibada ya Bikira Maria ambaye anaheshimiwa katika Kanisa Kuu kwa jina la: “Mater Ecclesiae”, yaani mama wa Kanisa. Kwa njia hiyo kila Jumatano za Mwezi Mei saa 10: 00 jioni kuanzia mwanzoni mwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutakuwa na sala ya mzunguko ambayo itagusa uwakilishi mkuu wa wakfu kwa Bikira Maria. Sala hiyo itamalizika saa 11.00 jioni kwa adhimisho la Misa Takatifu
Na kila Jumamosi jioni, kwa mwezi wote wa Mei, kuanzia saa 3.00 usiku hadi saa 4.00 kutafanyika maandamano na mishumaa mikubwa katika uwanja wa Mtakatifu Pietro wakiwa na picha ya “Mater Ecclesiae”, yaani Mama wa Kanisa akisindikiza sala ya Rosari Takatifu itakayoongozwa na Kardinali Angelo Comastri. Picha ya “Mater Ecclesiae” imechotwa juu ya nguzo ya kizamani ya Kanisa Kuu la Kostantini na ilikuwa ndiyo hiyo kabla ya Mtakatifu Paolo VI kutoa jina jipya kwa ajili ya Mtakatifu Petro na kwa ajili ya Kanisa la ulimwengu.
Liturujia inawaita mitume wa Kristo nguzo na msingi wa Kanisa, ikirejea maono ya Yerusalemu ya mbinguni iliyoelezwa katika kitabu cha Ufunuo. Na Mtakatifu Yohane Paulo II, mnamo 1981, miezi michache baada ya kushambuliwa, alibariki picha hiyo (mosaic) yenye jina la “Mater Ecclesiae” akionesha shauku kwamba kwa wale watakaokuja kwenye Uwanja huo wa Mtakatifu Petro waweze kuinua mtazamo wao kuelekeza Yeye kwa kumpati hisia za uaminifu wa kitoto, salamu binafsi na sala zao binafsi.