Mons.Urbańczyk:kubadili mifumo ya nishati ni uwekezaji wa muda mrefu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kupata faida ya teknolojia zinazoibuka ili kuondokana na nishati ya mafuta na kubadili nishati mbadala na endelevu, huku wakihakikisha uendelevu wa binadamu, ndiyo maneno yaliyosemwa na Monsinyo Janus Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo Barani Ulaya (OSCE), kuanzia tarehe 23-24 Mei 2022 wakati wa mkutano wa pili wa matayarisho ya Jukwaa la XXX la Uchumi na Mazingira la OSCE huko Łódź nchini Poland kuhusu mada ya: “Kuhamasisha usalama na utulivu katika eneo la Osce kupitia ufufuo endelevu wa uchumi kutokana na janga la UVIKO-19. Ni Mkutano ulioandaliwa na Urais wa Poland na Ofisi ya Mratibu wa Shughuli za Kiuchumi na Mazingira wa Shirika OSCE.
Changamoto za eneo la OSCE
Mwakilishi wa Kuvumu wa Vatican katika hotuba yake alibainisha jinsi kwa bahati mbaya mazingira ya usalama barani Ulaya yamebadilika tangu mkutano wa kwanza wa maandalizi ya Jukwaa la 30, uliofanyika mwezi Februari iliyopita. Kuzuka kwa vita nchini Ukraine kumechochea mgogoro mpya wa usalama ndani ya eneo la Osce, ambao unashinda masuala mengine yote na kuleta changamoto zaidi kwa mifano yao ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Imezidisha hali ambayo ilikuwa tayari imefanywa kuwa tete na usumbufu uliosababishwa na kuenea kwa janga la UVIKO-19. Vita kwa mujibu wa Mwakilishi wa Vatican, daima vina madhara ya kutisha ya kimazingira na kiuchumi, ambayo yana athari juu ya afya na maisha ya watu binafsi na familia nchini Ukraine. Bila kusahau kuzorota kwa usalama wa chakula katika nchi nyingi ambazo zinategemea uagizaji wa ngano, shayiri, mbolea na mafuta ya mboga kutoka nje ya nchi, kutokana na kuvuruga kwa masoko ya bidhaa duniani na mtiririko wa biashara.
Kubadilisha mifumo ya nishati ni uwekezaji wa muda mrefu
Katika muktadha huo, hata hivyo, Monsinyo Urbańczyk, akimnukuu Papa Francisko, alibainisha juu ya dharura ya uingizwaji wa haraka wa mafuta na vyanzo vya nishati safi kwa faida ya sayari. “Kubadilisha mifumo yetu ya nishati ni uwekezaji wa kimkakati wa muda mrefu ambao utaleta sio tu faida za kiuchumi kwa muda mrefu, tu lakini pia faida za mazingira”. Akiendelea alisema “Kipindi cha shida tunachopitia, kiafya, mazingira na usalama, lazima tukukumbushe kwamba kila shida inahitaji maono, uwezo wa kuunda mipango na kuitekeleza haraka, ili kufikiria tena mustakabali wa ulimwengu, nyumba yetu ya pamoja, na kutathmini upya lengo letu la pamoja”. Mikutano hii, alihitimisha mwakilishi wa Vatican, kwa hiyo inatoa fursa kufanya kazi pamoja kufikiria upya mustakabali ulio salama, wa haki na endelevu zaidi.