Tafuta

Askofu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi za UN huko Geneva Uswiss Askofu Fortunatus Nwachukwu, Mwakilishi wa Kudumu katika ofisi za UN huko Geneva Uswiss  

Mons.Nwachukwu,Mazungumzo ya kidini yasaidie kuishi kama kaka na

Katika mkutano huko Malaga tarehe 9 Mei 2022, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Taasisi Maalumu huko Geneva,Monsinyo Nwachukwu,alisisitiza na kualika mazungumzo ya kidini ili kuishi kama kaka na ndugu wakati wa mkutano kuhusu elimu ya tamaduni na dini mbalimbali kama chombo cha kuzuia migogoro na kuhamaisha Amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Taasisi Maalum huko Geneva, Monsinyo Fortunatus Nwachukwu, wakati wa mkutano kuhusu Elimu ya tamaduni na dini mbalimbali kama chombo cha kuzuia migogoro na kama chombo cha kuhamaisha Amani, ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Amani na UNITAR, alisisitiza na kutoa mwaliko wa mazungumzo ya kidini ili kuishi kama kaka na ndugu. Mkutano huo ulifanyika huko Malaga tarehe 9 Mei 2022 ambapo mwakilishi huyo alisema kuwa: “Wakati ambapo hisia ya kuwa wa familia moja ya kibinadamu inafifia na ulimwengu unaonekana kugawanyika na kutawanyika, mkutano huu unatoa fursa ya kutafakari jinsi mazungumzo ya kitamaduni na ya kidini unavyoweza kusaidia kushinda changamoto za kawaida ambazo ubinadamu unakabiliwa.

Mpango wa utekelezaji wa ahadi ya kiutamaduni na dini

Askofu Nwachukwu, katika hotuba yake mjini Malaga kwenye mkutano wa wataalamu waliojitolea kwa ajili ya Mpango wa Utekelezaji wa Ahadi ya Kiutamaduni na Dini kama Kichocheo cha Kuzuia Migogoro na kuhamasisha  Amani, ambapo pia  Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni na Baraza la Kiyahudi  Ulimwenguniwalishiriki alisisitiza kwa hakika kwamba “ni kupitia mazungumzo ya dhati ya kidini inawezekana kugundua tena hali ya kidugu ya kuishi pamoja, kuelewa utofauti ziliopo kati yetu, kutuliza hali za vurugu. Ili kusisitiza jinsi juhudi za kila mtu zilivyo za msingi na za lazima katika elimu ya watoto, Askofu Nwachukwu alikumbuka methali kutoka nchi yake, Nigeria, isemayo: Inahitaji kijiji kulea mtoto. Na hivyo aliongeza kusema kwamba “Tunaweza kusema kwamba kijiji hapa ni dini zetu, na mtoto wetu ni ubinadamu.

Dini zina wajibu wa kuonesha njia ya kwenda mbele kuepuka migogoro

Kwa hiyo, dini zina wajibu wa kuonesha njia ya kusonga mbele zaidi katika ulimwengu ambao migogoro na utawala,  hutawala juu ya masuala ya manufaa ya wote. Katika suala hilo, alikumbuka wakati, wakati wa safari yake nchini Iraq mwaka jana, Papa alipendekeza kurejea kwenye mizizi yetu ya pamoja, kwenye vyanzo vya kazi ya Mungu, kwenye asili ya dini zetu, akibainisha kwamba  uadui, itikadi kali na vurugu vinafanya. hayatokani na moyo wa kidini: ni usaliti wa dini na kwamba sisi waamini hatuwezi kunyamaza wakati ugaidi unaponyanyasa dini. Aliongeza   kusema kwamba Papa Francisko  kupitia safari zake za kitume na matendo yake zaidi ya ishara alisisitiza jukumu lisiloweza kutenganishwa kati ya dini tofauti,, mazungumzo na kukuza amani . Mazungumzo ambayo, ili kuzaa matunda, yanahusisha kwanza hisia thabiti ya utambulisho wa mtu, lakini pia ujasiri wa kufungua wengine kwa hamu ya kusikiliza, kuthamini na kutetea ubinadamu  haki za kimsingi na uhuru wa mwingine, pamoja na uhuru wa kidini .

10 May 2022, 17:07