Miaka 100 ya Shirika la watawa wa Mtakatifu Basili na Mabinti wa Mtakatifu Macrina
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, akitoa mahubiri kwa Watawa wa mabinti wa Mtakatifu Macrina wanaoadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa shirika lao mwaka huu mnamo tarehe 30 Aprili, alisema kwamba mwanzoni mwa taasisi yao kuna vipindi vyoto vya maisha ya kitawa na njia pekee ya karama yao hasa ya kuwa na uhusiano wa kina na Bwana, wawe wa kike na kiume na Mwalimu wao, utii na hali ya kuwa ndani ya Kanisa, kutoa huduma kwa watoto na maskini, uwazi wa kimisionari, ustahimilivu katika shida, hata kifungo nchini Albania, shauku ya umoja wa watoto wa Mungu iliyogawanyika kati yao.
Kardinali aliongoza Ibada ya utamaduni wa Kibizantini, ambayo ilifungua maadhimisho ya jubilei, kwenye Abasia ya Upatriki wa Grottaferrata nchini Italia. Katika mahubiri yake, Kardinali Sandrialikumbuka pia miaka hamsini tangu Shirika la Masista wa Mtakatifu Basili na ambalo tayari kisheria ni la kipapa ambalo limetanda huko Sicicilia, Albania, Kosovo na India. Na alisisitiza kwamba kupandikizwa kwa kufuata mapokeo makuu ya Kibizantini kumeweka hazina za kiroho zenye thamani, ambazo zinaweza kupatikana katika adhimisho la Liturujia. Hililinawafanya wao kuwa warithi na mashuhuda wa njia ya umoja ambayo Mtakatifu Basili na dada yake Mtakatifu Macrina walijikita nayo katika maisha ya utawa wa Mashariki.
Kardinali Sandri alisema wao wamepewa kuhisi mateso ya Baba kwa ajili ya mafarakano na migawanyiko kati ya Watoto wake na yale ya kale na yale yaliyotangazwa, yale ya hila zaidi ya leo katika uso wa mlipuko ndani ya ulimwengu huo huo wa Kiorthodox na Kibizantini. Aidha alikumbuka, hasa, historia ya Albania ya taasisi ya kitawa inayotafutwa na watawa wa Kiitaliano, na Kialbania kwa ajili ya utume katika jumuiya hizo za Mashariki. Ibada hiyo ina lengo la kuchangia mazungumzo ya kiekumene. Kardinali amehimiza juuu ya kujikita katika sala ya kina na mapendo yao hasa kwenye majeraha ya moyo wa mtu wa leo hii, wa ulimwengu na wa Makanisa, huku akiwaalika kumwaga mafuta ya faraja na divai ya furaha ya Kiinjili. Na kuomba pamoja na Yesu akimwomba baba ili wote wawe kitu kimoja.
Kadinali Sandri alitazama kwa kina juu ya hatau za kukua kwa shirika hili ambalo amesema, lililozaliwa kwa mpango wa Padre Nilo Borgia wa Piana ya Albania na ambaye huko Grottaferrata alikuwa kiongozi wa Elena na Agnese Raparelli, wanawake wawili wa kwanza watawa wa Shirika hilo. Watawa hao wawili walianza maisha ya utawa katika nyumba ya kitawa ya kale ya Mtakatifu Basili huko Mezzojuso, katika jimbo la Palermo Italia, wakichukua majina ya Macrina na Eumelia. Macrina, ambaye alikuwa mama Mkuu wa familia mpya ya watawa, alitangazwa Mtumishi wa Mungu na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 23 Machi 2017. Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki alimfafanua kama mwenye roho safi, ambayo katika sala ilielimishwa kuingia ndani kwa kina katika uhusiano na Mungu ambaye hatua zake daima zilikuwa na alama ya utiifu wa Kikristo, unaotokana na kumsikiliza kwa makini Baba wa Mbinguni.