Kusikiliza ubinadamu zaidi ya kishindo cha vita
Na Alessandro Gisotti.
Papa Francisko ni mtu ambaye sio kusikia tu, lakini anasikiliza’. Ina maana kubwa kwa katibu mkuu wa Caritas-Spes Ukraine, Padre Vyacheslav Grynevych, aliyetoa ufafanuzi huu kuhusu Papa, mara baada ya mkutano wa hivi karibuni na Papa katika Nyumba ya Mtakatifu Marta. Kuhani wa Shirika la Wapallotini alithibitisha hili kwamba kusikiliza kiukweli ni kazi muhimu zaidi ambayo yeye, kama waendeshaji wengine na watu wa kujitolea wa Caritas Ukraine, amekuwa akifanya, pamoja na shughuli za kibinadamu, tangu mwezi Februari 24 iliyopita, siku ya mwanzo wa uvamizi wa Urussi nchini humo. Kusikiliza mateso ya akina mama waliofiwa na watoto wao, yale ya akina baba wanaopigania utetezi wa nchi yao na hawajui kama wataiona familia yao tena. Kusikiliza kilio kisichoweza kufarijika cha watoto ambao, kwa karibu siku mia moja, wamekuwa wakiishi hofu kubwa ya vita vya kikatili ambavyo vimekatiza maisha yao ya asili yanayojumuisha michezo, mapendo ya shule na familia, kama maisha ya kila mtoto yanavyopaswa kuwa. Kwa hiyo kusikiliza. Si kusikia. Kwa sababu katika kusikia hata sikio linatosha, lakini kusikiliza kunahitaji moyo. Hapo ndiyo makao ya kusikiliza.
Papa Francisko alipochagua kusikiliza kama mada kuu ya Siku ya Upashanaji habari duniani mwaka huu, tafakari yake ilihamia zaidi ya yote kwenye uzoefu wa kutisha wa janga la Uviko-19. Alikuwa akimaanisha upweke uliokuwepo ambao sehemu ya ubinadamu ililazimishwa na vizuizi vya kuzuia maambukizi ambayo yamelemaza kile kinachomtofautisha zaidi mwanadamu, mtu, yaani uhusiano na wanadamu wenzake. Haishangazi, tunasoma katika Ujumbe kwa Siku itakayo adhimishwa Dominika 29 Mei ijayo, kwamba “uwezo wa kusikiliza jamii ni wa thamani sana katika wakati huu uliojeruhiwa na janga la muda mrefu”. Kwa uapande wa Papa Francisko, “unahitaji kutega sikio na kusikiliza kwa kina, hasa wasiwasi wa kijamii unaoongezeka kwa kudorora au kukoma kwa shughuli nyingi za kiuchumi”. Kwa hiyo, kuweza kufahamu shauku ya kusikilizwa, ambayo imekua kutoka katika uwiano wote katika mikunjo ya ukimya huo usio wa asili ambao umeangukia jamii zetu kwa miezi mingi, na kutufanya kugundua tena hitaji la kuwa karibu (mada ya mwisho inaendana na Ujumbe wa Papa Francisko wa Upashanaji wa habari Kijamii wa 2014) Ikiwa unamkaribia mwingine na kuwa karibu ya kusikia mapigo ya moyo, Papa anaonekana kupendekeza kwamba inaweza kumsikiliza kweli.
Kwa hivyo, ikiwa mada ya kusikiliza iliibuka, awali ya yote, kutokana na uzoefu wa janga, hii haina thamani ya chini katika muktadha wa kutisha wa vita vya Ukraine, na vile vile mzozo wowote. Kwa hakika, ikiwa katika janga hili, uwezo wa kusikiliza ulipaswa kupata masafa sahihi katika ukimya, sasa ni katika sauti ya silaha, katika kelele za vita kwamba mtazamo huu wa moyo lazima uweze kuizuia sauti ya wale wanaoteseka. Kwa mtazamo wa kiutendaji wa mawasiliano, hii “hutokea” ikiwa kuna mtumaji, mpokeaji na gombo inayoshirikishwa. Kwa maana hivyo mawasiliano yanalenga “kusema kitu” badala ya “kumsikiliza mtu”. Vita, kama janga la uviko, badala yake vimeonesha kile ambacho mwanafalsafa Abraham Kaplan (aliyezaliwa Odessa) tayari alionesha, akinukuliwa na Papa katika Ujumbe, ambachao ni kwamba mawasiliano ya kweli hayajapunguzwi kwa umoja wa sauti mbili (duologue), lakini yanahitaji kwamba mimi na nyinyi nyote ni “tunaotoka nje”, tufikiane. “Kusikiliz, anaandika Papa Francisko kwa hivyo ni kiungo cha kwanza cha lazima cha mazungumzo na mawasiliano mazuri. Mtu hawasiliani ikiwa hajisikiliza kwanza na hafanyi uandishi mzuri wa habari bila uwezo wa kusikiliza”.
Hapa, katika uthibitisho wa mwisho tunapata ushauri na uwasilishaji kwa wahudumu wa taarifa hasa katika wakati wa kihistoria ambao ni tete na usiotabirika kama ule tunaoupitia. Kufanya mawasiliano mazuri, uandishi wa habari mzuri, unapaswa kusikiliza. Awali ya yote, sikiliza wale ambao wana sauti dhaifu. Kazi ambayo waandishi wengi wa habari nchini Ukraine wanafanya, hata kuhatarisha maisha yao, pamoja na wale walio kazini mahali pengine popote pale ambapo vita zaidi au kidogo vimesahuliwa. Kusikiliza kunahitaji uvumilivu, unyenyekevu. Fadhila ambayo, kama ilivyosemwa na Papa alipokutana na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kigeni nchini Italia mnamo tarehe 18 Mei 2019, kwamba hufanya kuwa huru na sio kuwa ya wastani. “Mwandishi wa habari mnyenyekevu ni mwandishi wa habari huru. Huru dhdi ya ubaguzi, na kwa hivyo jasiri”, alisema katika fursa hiyo Papa. Uhuru ambao leo hi ina zaidi ya wakati mwingine wowote lazima uhifadhiwe, katika ufahamu kwamba ule wa wafanyakazi wa habari si taaluma tu, bali ni utume katika huduma kwa ajili ya manufaa ya wote.