Tafuta

Walinzi wa Kipapa Walinzi wa Kipapa  

Kikosi kipya cha Walinzi kitaapishwa Mei 4&saini katika Protokali za ukarabati wa jengo

Kitendo hicho cha kutia saini kitafanyika katika Jumba la Kitume Vatican,katika muktadha wa sherehe za kuapishwa kwa watumishi wapya wa kikosi cha ulinzi wa Kipapa wa Uswiss.Ni katika fursa ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa 147 walinzi wa kipapa waliokufa katika vita jijini Roma wakiwa wanamlinda Papa Clemente VII.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Muktadha wa sheherehe za kiapo cha wanafunzi wapya 36 wa kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka  Uswiss ambapo Jumatano tarehe 4 Mei  2022, kwenye mida ya  saa 4 asubuhi katika Jengo la Kitume, jijini Vatican,  kwanza kutakuwa na tendo la kutia saini Protokali ya makubaliano kwa ajili ya kukarabati jengo la Kikosi cha Ulinzi cha Kiswiss. Makubaliano hayo yatakuwa  chini ya Sekretarieti ya Vatican na Mfuko kwa ajili ya kukarabati Jengo hilo la Walinzi wa Kipapa wa Kiswiss jijini Vatican.

Ikukumbwe Kikosi cha Walinzi wa Papa kutoka Uswiss, kimekuwa na dhamana na utume wake katika mji wa Vatican kwa shughuli mbali mbali kwanza kulinda na kupokea wageni wa kila siku. Kwa njia hiyo Wanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi wa Kipapa kutoka Uswiss, katika siku hiyo pia wanafanya kumbu kumbu ya askari 147 kutoka Uswiss waliotoa maisha yao mjini Roma wakiwa wanamlinda Papa Clement VII  mnamo  mwaka 1527 jijini Roma.

02 May 2022, 12:45