Tafuta

2022.05.11  Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin nchini Kroatia. 2022.05.11 Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin nchini Kroatia. 

Kard.Parolin:kuongezeka kwa vita Ukraine ni tishio la ubinadamu wote

Katibu wa Vatican ameanza ziara yake huko Kroatia katika fursa ya miaka 30 utambuzi wa uhuru wa Jamhuri ya Nchi hiyo kwa upande wa Vatican,amepo akizungumza na waandishi wa habari amekumbusha uwezekano wa Papa kufanya kila liwezekanlao ili kuwepo mwisho wa mgogoro wa ukraine.Kardinali amesema kuongeza kwa mgogoro una matokeo mabaya katika ulimwengu wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wasi wasi wa Vatican kwa uwezekano wa kuongezeka kwa vita nchini Ukraine, umeelezwa na Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican wakati wa kukutana na waandishi wa habari huko Zagreb katika fursa ya ziara yake nchini Kroatia kwa ajili ya kuadhimisha miaka 30 tangu kutambuliwa uhuru wa Jamhuri ya Croatia na uhusiano na  Vatican  na kumbukumbu ya miaka 25 ya kupitishwa kwa Mikataba Mitatu kati ya Vatican nan chi hiyo ya kibalkani.

Vita vinavyoendelea ni tishio la ulimwengu

Kardinali Parolin aliyewasili katika mji mkuu wa Croatia alisema kuwa kwa kuzingatia uharibifu wa silaha ambazo zinamilikiwa leohii kupanuka kwa mzozo kutakuwa tishio kwa uharibifu wa ubinadamu wote. Katibu wa Vatican aidha akakumbuka maneno mazito  ya Baba Mtakatifu Francisko dhidi ya wazimu wa vita na nia yake ya kufanya kila kitu ili kuchangia amani, akitoa upatanishio kutoka Vatican na kusema yuko tayari kwenda Moscow, lakini wazo ambalo halijakubaliwa hadi sasa. Kardinali  Parolin alisema “Inaonekana kwamba kwa sasa hakuna matumaini makubwa kwamba hitimisho la makubaliano la vita linaweza kufikiwa, lakini Vatican bado iko wazi kusaidia kukomesha vita hivi haraka iwezekanavyo”.

Giza la vita hufunika akili

Katika janga linaloendelea Ulaya, Kardinali Parolin amezungumzia hata wakati wa Misa aliyoadhimisha huko Zagreb. Katika mahubiri yake amebainisha kwamba “giza la vita pia hufunika nuru ya akili ya kibinadamu na hata kuonekana kushindwa akili. Katika miaka miwili iliyopita tumeishi katika giza la janga ambalo tumejikuta gizani, bila kujua jinsi ya kuchukua hatua, bila kujua la kufanya. Jaribio lolote la suluhisho lilionekana kutotosha”. Baada ya janga hili kumekujaa mzozo huko Ukraine: Katika hali kama hizi za 'giza' tunajikuta tumechanganyikiwa lakini nuru ya Kristo mfufuka ina nguvu na inatoa tumaini na faraja, hata kupitia mashahidi wake”. Miongoni mwa hawa alimnukuu Mwenyeheri Alojzije Stepinac kwamba: “Katika nyakati hizi za vita huko Ulaya inafaa kukimbilia maombezi yake. Sisi leo kama yeye basi tunakabiliwa na maovu ambayo yanazaliwa ndani ya mioyo ya watu na huelekea kuchukua akili na nafsi.”

Uhusiano mzuri kati ya Kroatia na Vatican

Ziara ya Zagreb imeanza kwa kukutana na maaskofu wa Kroatia ambapo amewapa salam una ukaribu wa Papa. Katika mchakato wa karne kwa watu wa Kroatia walionesha daima uaminifu kwa Vatican. Kwa upende mwingine, Mapapa waliihusika kwa moyo kuongeza uhusiano wa dhati na watu wa Kroatia na walionesha ishara nyingi za wema kuelekeza katika Kanisa na ardhi hiyo. Katibu wa Jimbo aliongeza kusema kwamba: “Katika miaka hii 30 nchi na Kanisa mahalia limechukua hatua muhimu sana, ambazo Makao ya Vatican imefuata kwa ukaribu. Miaka michache baada ya uhuru, Serikali ilitambua jukumu maalum la kihistoria na kiutamaduni la Kanisa mahalia, pamoja na nafasi yake ya kijamii, na kutia saini na kuridhia mikataba minne ya nchi mbili na Vatican, kati ya 1996 na 1998. Ofisi ya Kijeshi na Majimbo mengine 5. Mafundisho ya dini yamerejea mashuleni na yale ya kitaalimungu katika vyuo vikuu vya serikali. Chuo Kikuu cha katoliki cha Kroatia huko Zagreb kilifunguliwa, pamoja na shule kadhaa za Kikatoliki na makanisa mengi yalijengwa au kukarabatiwa na kwa hiyo kutokana na ahadi ya pamoja, uhusiano mzuri umeanzishwa kati ya Kanisa na Serikali”.

12 May 2022, 15:48