Kard.Parolin:Itikadi na chochezi hazitatusaidia kukabiliana na matatizo ya maisha yetu
Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, alizungumza katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana katika Kongamano lililojikita katika 'majadiliano na manufaa ya wote', uliohamasishwa na ubalozi wa Morocco jijini Vatican na Shirika la Kijeshi la Malta. Katika hotuba yake amesema "Katika kipindi hiki chenye machafuko yasiyo na maana, Vatican inajitahdi kuchangia juhudi za amani, ambazo, pamoja na haki na udugu, pia ni zawadi kutoka kwa Mungu ambaye tunamsihi kwa bidii. Kwa maana hiyo janga la uviko na mzozo wa Ukraine ndio masuala makuu ya kujibiwa na sanaa ya amani ambayo taasisi za kijamii zinachangia kuunda. Japokuwa kuna hata uhuunzi wa amani ambao inawahusu watu wote amesema Kardinali Parolin.
“Ulimwengu wetu una kiu ya amani, kwa wema huu usioonekana ambao unahitaji juhudi na mchango wa kila wakati” amesema na hata kuhusu janga, Kadinali anaongeza, ni muhimu kuendeleza michakato madhubuti katika huduma ya amani, kuweka hadhi takatifu ya ubinadamu na heshima kwa manufaa ya wote katikati ya kila hatua. Sote tumeitwa kuchangia usanifu wa kimataifa na wa kudumu wa amani”. Katibu wa Vatican amekumbuka maneno ya Papa kwa Wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao Vatican na hasa amesisitiza maneno mawili muhimu, "mazungumzo" na "udugu", vyanzo muhimu vya kushinda machafuko ya wakati huu, yenye sifa za kelele za kufanya viziwi za vita na migogoro. Mara kadhaa katika siku za hivi karibuni Papa Francisko amewataka watendaji wote wa jumuiya ya kimataifa kujitolea kwa kukomesha vita hivi vya kutisha kwa dhati",amebainisha Kardinali Paolin.
Kardinali Parolin akiendelea na hotuba yake pia amekumbuka kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Morocco ulioanzishwa mnamo mwaka 1976, ziara ya Papa Yohane Paulo II mnamo mwaka 1985 na ile ya Papa Francisko mnamo mwaka 2019 ambaye aliifafanua nchi hiyo kuwa ni daraja la asili kati ya Afrika na Ulaya na alikuwa ameshauri kujenga dunia iliyounganishwa zaidi na kujitolea zaidi kwa ajili ya mazungumzo ambayo yanaheshimu kwa namna ya pekee kila watu na kila raia. Amani lakini pia maendeleo, na dhana iliyothibitishwa tena na Papa katika ujumbe kwa ajili ya Mkutano wa tisa wa Maji Duniani huko Dakar, kipengele cha mwisho ambacho ni ishara ya kweli ya kugawana, ya mazungumzo ya kujenga, amesisitiza tena Kardinali Prolin.
Mwaliko huo kwa maana hiyo ni wa kufanyia kazi pamoja zaidi ya yote kupambana na tatizo la ukame ambalo, katika siku za hivi karibuni, limeathiri maeneo ya vijiji vya Morocco. Vile vile katika hotuba yake Kardinali Parolin, pia wazo kwa mtakatifu mpya Charles de Foucauld ambaye alikuwa amekwenda Morocco na ambaye kuwepo kwake kulikuwa na muktadha mkubwa kwa Kanisa Katoliki la Morocco na kuzaa mipango mingi ya kutoa maelezo madhubuti kwa wito wa Mtaguso wa II wa Vatican kwa kufanya mazungumzo na dini nyingine, hasa na Waislamu. Morocco ni nchi tajiri kwa uzuri, ambayo imekuwa mahali pa kukutana kwa ustaarabu, inayojulikana na utamaduni wa uvumilivu. Kama waamini, Kardinali Parolin amebainisha kuwa ana uhakika kwamba ni lazima watambue kwa furaha maadili ya kidini ambayo tunafanana. “Itikadi na chochezi hazitatusaidia kukabiliana na matatizo ya maisha yetu ya kila siku na ya jamii zetu. Ni maadili tu ya kiroho na maadili yanaweza kufanya hivi, shukrani kwa Mungu na rehema zake”.