Tafuta

Kardinali  Sean Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston, Marekani Kardinali Sean Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston, Marekani 

Kard.O'Malley kuhusu nyanyaso:kuna bahari ya mateso&tunaitwa kukabiliana!

Katika ujumbe kwa njia ya video kwa mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia,Kardinali O'Malley amesisitiza umuhimu wa kufanya kazi ili kutoa nafasi za kusikiliza na kuwalinda walionyanyaswa na wanaoishi katika mazingira magumu."Nina hakika kwamba una fursa ya ajabu ya kuendeleza mazungumzo ya haki na wote na watu wanaohusika!

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Mambo saba yanapaswa kubadilishwa kuwa vitendo ili kuanzisha mchakato mzuri wa marekebisho, mageuzi na upatanisho. Katika ujumbe wake kwa video kwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia  CEI  mjini Roma na ambao, umemchangua Kadinali  Matteo Zuppi kama rais, Kardinali Sean Patrick O'Malley Rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, ametumia historia yake binafsi kama askofu hadi uzoefu wake kama rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto ili kuonesha jinsi katika miaka ya hivi karibuni  angalau kwa miaka 20 nchini Marekani pekee kazi iliyofanywa duniani na Kanisa katika kuwakaribisha waathirika wa unyanyasaji na kuunda aina za ulinzi imetoa matokeo muhimu sana. “Hatuna chochote cha kuogopa katika kusema ukweli”, anamesema Kardinali, na hivyo “waamini wetu wanataka kujisikia salama katika Kanisa lao, na hii ina maana kwamba wanapaswa kuimarishwa katika imani kwa kujitolea kwa wachungaji wao.

Katika siku hizi kabla ya Pentekoste, kiukweli ni kama mitume waliokusanyika karibu na Mama  Yetu na Petro ambao wanaomba Roho Mtakatifu amimine juu ya Kanisa. Mtakatifu Fransisko wa Assisi alitaka Ndugu wadogo  kusherehekea sura zilizo karibu na Pentekoste ili Roho Mtakatifu ndiye baba mkuu wa utaratibu. Roho Mtakatifu amiminike kwa Kanisa lote  na hasa kwenye Baraza lao la Maaskofu kwani wameitwa kufanya maamuzi yenye changamoto nyingi. Mambo ya kuzingatia ni mengi na muhimu, lakini ni muhimu kukubaliana mambo yanayokwenda pamoja kwa hatua ili kushughulikia masuala  kwa njia muhimu. Kwa hivyo Kardinali aliwapongeza kwa juhudi zao na za wengine wengi. Katika Tume ya Ulinzi wa Watoto wako pamoja nao ili kutoa msaada wowote wawezao. Utata wa changamoto ni kwamba hata baada ya miaka thelathini na minane ya huduma, akiwa kasisi na askofu akishiriki katika utume wa kuwalinda watoto wadogo na katika mapambano dhidi ya unyanyasaji wa makasisi, bado anaendelea kujifunza mambo mapya.

Kardinali O Malley baada ya kueleza mengi, alipenda kuongeza tafakari ambazo zinaweza kuwa muhimu katika mjada wao. Ni ukweli kwamba watahukumiwa kwa msingi wa mwitikio wao kwa mgogoro wa unyanyasaji katika Kanisa. Kwa maana hiyo waunahitaji uongofu wa kichungaji unaojumuisha vipengele vifuatavyo:

1. Kutoa huduma bora ya kichungaji kwa waathirika;

2. Kutoa maelekezo wazi (na kusimamia) juu ya kozi za mafunzo kwa wafanyakazi katika jimbo;

3. Fanya uchunguzi wa kutosha na sahihi;

4. Ondoa wahalifu;

5. Kushirikiana na mamlaka za kiraia;

6. Tathmini kwa uangalifu hatari zilizopo kwa mapadre wanyanyasaji (kwa ajili yao wenyewe na kwa jumuiya) mara tu wanapokuwa wamerudihwa  kuwa walei;

7. Onesha matumizi ya itifaki zilizopo, ili watu wajue kuwa sera zinafanya kazi. Ukaguzi na ripoti ya utekelezaji wa sera ni muhimu sana.

Habari njema ni kwamba pale ambapo sera madhubuti zimewekwa na kutekelezwa ipasavyo, idadi ya kesi hupunguzwa sana. Kikwazo kikubwa kwa uongofu wa kichungaji kinawakilishwa na uchaguzi wa kuchukua mara moja mtazamo wa ulinzi wa Kanisa. Ni wazi kwamba kulilinda Kanisa kunaweza kuonekana kuwa jambo la kawaida kwa Maaskofu ambao wamepewa jukumu la kulinda kundi na Kanisa ambalo wao ni sehemu yake. Lakini Papa Francisko aliwasihi wasikubali jaribu hilo na akasisitiza haja ya kuwakaribisha watu bila kujilinda sana. Haishangazi, Baba Mtakatifu amelitaja Kanisa kuwa ni hospitali kambini, tayari kuwaponya wale ambao wamevunjika na kujeruhiwa na dunia. Kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya Kanisa ni kama ugonjwa ambao watu hupata wakiwa ndani ya hospitali. Hakuna mtu hospitalini na hasa wale wanaoiendesha na anataka kukubali kwamba mtu aliugua mahali ambapo alipaswa kupona. Kwa kufanya ulinganisho huo Kardinali O’Malley alisema unaweza kueleza kwa nini ni vigumu kwao kama  Maaskofu kukubali na kujibu pamoja na ukweli wa dhuluma katika Kanisa. Mada nyingine aliyotaka kushiriki nao ni jinsi uaminifu wa Kanisa unavyoweza kulindwa na kuimarishwa.

Hivi karibuni, Baba Mtakatifu Francisko aliomba Tume yao kuandaa Ripoti ya Mwaka juu ya juhudi zote zinazofanywa katika Kanisa zima kuwaweka watoto na watu wanaoishi katika mazingira magumu na salama. Hapana shaka kwamba, Kanisa ni miongoni mwa watendaji wakuu duniani kote katika kutengeneza nyenzo bora za ulinzi wa watoto wadogo. Unapofuatilia njia iliyo mbele  historia ya unyanyasaji katika Kanisa itadhihirika zaidi na zaidi. Haya ndiyo yametokea katika kila nchi ambako mchakato huo umeanza. Wakati huo huo, Papa Francisko alionesha hitaji la umakini ufaao. Unyanyasaji wa kijinsia umekuwa sio sawa kila wakati, hiyo ni hakika. Lakini majibu ya viongozi wa kikanisa na kiraia pia hayakuwa sahihi. Kwa maana hiyo jKama Kanisa wamejifunza mengi katika miaka arobaini iliyopita. Ni baadaya wakati tu ambapo wamekuja kuona na kuelewa maisha yaliyoharibiwa, kwa mfano na dawa za kulevya na hata hali ya kutisha ya watu wanaojulikana na kujiua kwa siri.

Kuna bahari ya mateso ambayo kama wachungaji wanaitwa kukabiliana nayo amesisitiza Kardinali O’Malley Akisisitiza zaidi aliwambia kwamba hawapaswi kuogopa kukiri uovu ambao umefanywa kwa ndugu na dada zao wengi. “Mtazamo wa nyuma” unaweza kuwa hakimu mwenye nguvu sana, lakini tu kwa kujibu kwa haki kwa waathirika itawezekana kufikia tiba. Pale ambapo watu binafsi wameshindwa kutimiza wajibu wao, lazima wao wachukue hatua madhubuti za kuwawajibisha kwa makosa yao. Bila haki hakuna uponyaji. Ikiwa waathika watanyimwa haki, itakuwa ngumu kupata suluhisho la shida.

26 Mei 2022, 16:36