Kard.Mardiaga:Praedicate Evangelium.Curia mpya kwa wakati mpya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Marekebisho ya Kanisa la Roma ni safari, mchakato, roho, tafakari ya kina, na Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi iliyopita na ambayo itaanza kutumika tangu tarehe 5 Juni 2022 katika siku ya Pentekoste, ni sehemu tu ya mageuzi mapana ambayo yalianza na Upapa wa Francisko. Katika uwasilishaji wa kitabu chake kwa lugha ya Kihispania, kiitwacho 'Praedicate Evangelium'. Curia mpya kwa wakati mpya kwa Mchapisho wa nyumba ya Claretian, Kardinali Óscar Andrés Rodríguez Maradiaga alifafanua kwa maneno haya kile kilichoandaliwa na Baraza la Makardinali kujibu mapendekezo ya Mkutano Mkuu, kabla ya Mkutano wa uchaguzi wa 2013, ambapo lilisisitiza kama uharaka na muhimu wa mageuzi mapya ya Curia Romana. Kitabu hicho chenye utangulizi wa Papa Francisko, ni mazungumzo marefu ambayo yaliendelea kwa muda na Padre Fernando Prado Ayuso, mkurugenzi wa shirika la Claretian ambalo limechapisha kitabu hicho na kufafanua kwamba ni miaka tisa ya kujitolea inayohitajika na Katiba mpya ya Kitume.
Mazungumzo ambayo hata janga hili halijakatiza kwa lengo la kujulisha mageuzi ya Curia na Praedicate Evangelium ili iweze kutekelezwa. Sisi sote tumeitwa kukunja mikono yetu, aliandika Papa Francisko katika mahojiano ya kitabu, akionya kwamba sheria na hati sikuzote zina mipaka na karibu kila wakati ni za kawaida na kusisitiza kwamba nyakati zingine zitakuja na kwamba hali zingine zitatoa katika dunia rangi mpya. Kwa sababu hiyo, "Kanisa, katika mazungumzo yake ya kudumu na walimwengu, likiwa na msingi thabiti katika chimbuko lake na uaminifu kwa Mapokeo, kwa mara nyingine tena litarekebisha maisha yake na miundo yake ya kibinadamu kwa mabadiliko ya hali ya nyakati. Kwa hivyo Kanisa litaendelea kutoa Injili kwa ulimwengu katika muundo mpya, aliandika Papa.
Katika kurasa 264 kitabu hicho, Kardinali Maradiaga anarejea hatua za Baraza la Makardinali, washauri wa Papa na anaweka bayana, anaboresha simulizi kwa ucheshi wake mkubwa na anaelezea mambo muhimu ya mageuzi, matokeo ya rasimu kadhaa ambazo Papa amesoma na ya mwisho ambayo iliidhinishwa mnamo tarehe 8 Juni 2020, na kazi ambayo sio huru kutoka kwa upinzani na vizuizi. Lakini uzoefu wa thamani wa sinodi, ambao ulianza tarehe 16 Machi 2013, siku tatu baada ya kuchaguliwa katika kiti cha upapa cha Jorge Mario Bergoglio, wakati Kardinali wa Honduras alipokea simu ambayo inamshangaza. Ni Papa mpya, ambaye anamwalika kwa chakula cha mchana katika nyumba ya Mtakatifu Marta. Papa Francikos alimwomba kuratibu kundi la Makardinali ili kumsaidia katika kuliongoza Kanisa. “Kusema kweli, sijui kwa nini Papa alinifikiria,” anakiri Kardinali Maradiaga katika kitabu hicho. Alikuwa amefanya kazi na Bergoglio katika Kongamano la Aparecida na alikuwa na mawasiliano kupitia Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini, (Celam). Lakini Papa wa Argentina pengine alisukumwa na kitu kingine alipomfikiria askofu mkuu wa Tegucigalpa. Papa Francesco anajua kuwa mimi ni muimbaji na nimekuwa nikiongoza kwaya, kwa kutania Kardinali na labda alifikiria ili aweze kuunganisha sauti tofauti”.
Akikutana na wanahabari, hata hivyo Kardinali Maradiaga alisema kwamba jina lenyewe Katiba mpya linaangazwa kwa usahihi roho mpya ambayo mageuzi lazima yaletwe, kwa sababu inasisitiza sababu ya Kanisa kuwepo na kuinjilisha. Ni tangazo hilo ambalo linahitaji roho ya kimisionari na ambayo kwa sababu hiyo inalisukuma Kanisa kwenda nje. Kisha Kardinali akiorodhesha uvumbuzi mkubwa unaoletwa na waraka huo, ambao ndani yake unajitokeza umuhimu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji, utakaoongozwa na Papa mwenyewe, aliye Mwinjili wa kwanza; kigezo ambacho lazima kuhuisha kazi katika Curia Romana ya huduma; haja ya muundo wenye sifa ya sinodi na ili wazi kwa ajili ya kusikiliza Mabaraza ya Maaskofu. Marekebisho hayo pia yanaangaza hata uwezo wa kikanisa wa ofisi na madaraka hivyo kwamba kardinali ni mhudumu tu wa Papa na mteule wa Papa. Katika Curia nyadhifa hizo zitadumu kwa miaka mitano ili kutokuza vituo vya madaraka katika nyadhifa za serikali. Na tena askofu mkuu wa Tegucigalpa alizungumza juu ya upinzani ambao mageuzi yamekutana nayo, upinzani, maoni yanayopingana. Lakini hii ndiyo njia ya sinodi, alisema, ‘kusikiliza kila mtu, kutafuta suluhisho, kujadiliana, kukabiliana”.