Kard.Grech:Binadamu atoe ahadi ya kulinda amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Mario Grech, katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, ameongoza Ibada ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Maria wa Rosario kwenye uwanja ulio mbele ya Madhabahu ya Pompeii, Dominika tarehe 8 Mei siku ambayo maelfu ya waamini husali sala kwa kujiweka wakfu kwa Bikira Maria wa Rosari. Kardinali katika mahubiri yakeamejikita katika njia ya sinodi iliyoanzishwa katika Kanisa. Mariam, ni mwanamke wa sinodi na uso wa Kanisa la Sinodi na uso pembejeo mbili muhmu ya sala na upendo. “Kanisa la sinodi ni Kanisa linalotoa ahadi juu ya mwanadamu na Huruma na upole. Kardinali amesema Mungu ameweka ahaadi kwa ubinadamu na anaendelea kufanya hivyo. Mbele ya Bikira Maria tunaleta watu wa Ukraine na wale wote wanaoteseka leo hii, katika ubinadamu. “Kupitia maombezi ya Maria, sisi pia tunaomba tuige Mungu, na wenye uwezo wa kutoa ahadi za binadamu wenye uwezo wa kujenga na kulinda amani. Hatuwezi kushindwa kuleta mbele ya moyo wa mama wa Bikira Maria huzuni na uchungu wa vita, vurugu na chuki ambazo leo zimemwaga damu Ulaya na sehemu nyingi za dunia.
Kondoo hufanya nini? Kondoo husikiliza sauti ya Mchungaji. Yesu anazungumza katika nafsi ya kwanza na kusema: “kondoo huisikia sauti yangu”. Jambo la kwanza ambalo kondoo hufanya ni kusikiliza sauti ya Mchungaji. Hii inazungumza juu ya uhusiano wa kibinafsi ambao ni tunda la maombi na kurudia Neno la Mungu mara kwa mara.Kwa hakika, tunasikiliza tu sauti tunayoijua, ile tunayoifahamu sisi, si ile ya mgeni (Yn 10, 5) ambayo hatujui. Mwanzoni kabisa Injili inasema kwamba mchungaji huwaita kondoo mmoja baada ya mwingine kwa jina na kwamba kondoo waijua sauti yake (rej. Yh 10:3-4). Ili kusikia sauti ya Mchungaji, ni muhimu kumfahamu na ujuzi huu, unaotuwezesha kutambua sauti yake kati ya sauti nyingi, ni maombi katika uzoefu wa kuamini. Pia katika hotuba ya ufunguzi wa safari ya sinodi, Baba Mtakatifu alithibitisha:“Sinodi inatupatia fursa ya kuwa Kanisa la kusikiliza: kupumzika kutoka kwa midundo yetu, kuacha mihangaiko yetu ya kichungaji ili kusimama na kusikiliza. Kumsikiliza Roho katika kuabudu na kuomba”.
Pili, kondoo hufuata mchungaji. Ni kitenzi cha pili ambacho kina kondoo kama mhusika wake. Haitoshi kusikiliza, ni muhimu kufuata. Hapa tunaweza kusema tunapata kipengele cha pili cha Kanisa chenye uso wa sinodi: upendo. Ni kusikiliza sauti ya Mchungaji ambayo inatafsiriwa katika maisha hai. Hakuna usikilizaji wa kweli ambao hautafsiri katika kumfuata Bwana, kufanya "sinodi" nyuma yake, kutembea pamoja. Ni muhimu kwamba tunazungumza juu ya kundi. Kwa kweli, katika kundi ni muhimu kutembea pamoja, kwenda pamoja nyuma ya mchungaji. Ni kwa njia hii tu kondoo wanaweza kupata uzima. Kondoo anapopotea na kutembea peke yake, huenda kwenye hatari. Lakini kundi hutembea pamoja si kwa sababu washiriki wake wamechaguana, bali kwa sababu ya uhusiano walio nao wote na mchungaji mmoja. Kama vile mchungaji ndiye afanyaye umoja wa kundi, ndivyo Yesu afanyaye umoja wa Kanisa, wa jumuiya ya wanafunzi wake. Kisha msingi wa kusikiliza na kufuata haupo kwa kondoo, bali kwa mchungaji. Ni lazima tumtazame ikiwa tunataka kupata msingi wa kuwa kwetu Kanisa.
Katika Kifungu cha Injili kinabainisha juu ya uhusiano kati ya Yesu-Mchungaji na kondoo-wanafunzi haujafungwa ndani yenyewe, lakini unaenea hadi kwa Utatu na Baba. Andiko hilo linaonekana kuthibitisha kwamba jambo la maana ni kwamba ni Baba aliyemkabidhi Yesu kondoo: kwa msingi huu wako salama mikononi mwake. Kama katika Injili yote ya Yohane, hapo pia inathibitishwa kwamba msingi wa uhusiano kati ya Yesu na wanafunzi wake ni uhusiano uliopo kati ya Yesu na Baba. Inatokea kama kitambulisho cha mkono wa Mwana na mkono wa Baba. Wanafunzi wako salama mkononi mwa Mwana, kwa sababu ndani yake mkono wa Baba unapatikana. Kardinali hakukua kuzungumzia mchakato wa Sinodi wa Kanisa unaeoendelea na kwamba pia katika sehemu hii ya kifungu cha Injili ya Dominika nikuelekeza katika kiini cha taalimungu ya sinodi. Kwa hakika ni katika ushirika wa Utatu ambapo jumuiya ya wanafunzi wa Bwana Yesu inagundua kielelezo chake yenyewe na chanzo cha kuwepo kwake. Hati ya Tume ya Kimataifa ya Kitheolojia inasema: "Kanisa linashiriki, katika Kristo Yesu na kwa njia ya Roho Mtakatifu, katika maisha ya ushirika wa Utatu Mtakatifu zaidi unaokusudiwa kukumbatia wanadamu wote (n. 43).
Na hapo Pompei zimehifadhiwa kweli ule ambazo zinapatikana katika kifungu cha Injili ya Dominika ya nne ya Pasaka hi ambazo ni viungo vya msingi vya njia ya sinodi inayoendela hasa sala na mapendo. Lakini kuna "mlinzi" mwingine wa zawadi hizi na ambaye ni sura ya Kanisa: Mariam, anayeheshimiwa hapo kama Bikira wa Rozari. Maria ni mwanamke wa sinodi kwa sababu yeye ni Bikira wa kusikiliza na huruma. Ndani yake linalitafakariwa Kanisa la Mama na Bibi-arusi lililoitwa kutoa wingi wa watoto kwa Mwanae, ambaye alikufa na kufufuka kutoka kwa wafu. “Kusasisha ombi kwa Mama Yetu wa Pompeii mwaka huu hakuwezi ila kutufanya tufikirie hali halisi nyingi. Ombi hilo lilizaliwa kwa kurejelea maisha ya Kanisa na ya dunia: ni kuleta mbele za Mungu, kwa njia ya Maria, “furaha na matumaini, huzuni na mahangaiko ya watu wa leo, hasa maskini na wote wanaoteseka”. GS 1). Kwa maana hiyo leo, katika sala kwa Bikira Maria, Bikira wa Rozari, amesema hawawezi kushindwa kupeleka “furaha na matumaini” ya njia ya sinodi inayoendelea na ambayo Baba Mtakatifu anatoa mwaliko mara kwa mara kutembea kwa ari na uaminifu,kwa kujiachia wenyewe kwake ili kuongozwa na Bikira Maria wa Sinodi.
Kuanzia Mei Mosi ilianza kile kiitwacho ‘Habari za asubuhi kwa Maria ambapo ni mpango wa sala za asubuhi saa 12.30 kwa kukabidhi siku mpya kwa Bikira Maria. Jumamosi 7 Mei kulikuwa na Mkesha wa Maria na kilele chake ni sherehe ya usiku wa manane iliyoongozwa na Askofu Mkuu Tommaso Caputo wa Pompeii. Askofu mkuu wa Pompei, Monsinyo Tommaso Caputo, katika mahojiano miaka miwili iliyopita, katikati ya janga hili, akielezea maana ya ombi na kutoa maoni juu ya maneno ya Bartolo Longo katika sala, ambayo yanakumbuka wasiwasi na shida, hatari kwa nafsi na mwili na kwa misiba na mateso, alisema kwamba hakuna, katika historia ya ubinadamu au hata katika mambo ya kibinafsi ya watu binafsi, wakati ambapo mtu anakuwa huru kutokana na wasiwasi wote.
Na alikuwa amesema kwamba kuamini, kusali kwa Bikira wa Rozari wa Pompei, kuwa na imani, ni kuamini Mungu anayesimamia maisha yetu. “Na kujikabidhi ni sala yenye kuzama imani, ya kina. Hatutaepuka uchungu na matatizo lakini hatutaogopa wakati, katika mioyo yetu, tutakuwa na uhakika kwamba Mungu Baba yuko pamoja nasi, akitembea pamoja nasi. Na Maria yuko pamoja naye”. Kwa maana hiyo inahitaji kuwa na upendo ambao unatafsiriwa kwa jirani na ndiyo hutafsiri imani unakuwa kitulizo, msaada, kazi ya huruma na akaongeza kwamba ikiwa katika magumu hakika nyingi huporomoka, hatupaswi kusahau faraja ya Mungu, lazima tukuze imani. Kuishi kwa imani haimaanishi kuwa na kichocheo cha matatizo yote -lakini kutafuta, kila wakati, jibu la kibinafsi, kuzingatia mitindo ya Mungu na kushika maswali ya historia. Kama alivyofanya Bartolo Longo, mwanzilishi wa Patakatifu pa Pompeii, ambapo kardinali alikuwa amefanya muhtasari wa njia ya maisha ambayo ilikuwa imempeleka kuanza kazi nyingi za hisani.