Tafuta

Juma la Laudato si 22-29 Mei 2022 Juma la Laudato si 22-29 Mei 2022 

Juma la Laudato si’,22-29 Mei:mitindo mipya ya kujibu kilio cha dunia

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo ya Binadamu inapyaisha tena Juma la Laudato Sì kuanzia tarehe 22 hadi 29 Mei katika kumbu kumbu ya miaka saba ya Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko. Ni kwa kazi ya uhamasishaji,mipango na matendo mema ili kujikita katika uharaka wa kulinda nyumba yetu ya wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Juma la Laudato si linarudi tena kuwa hai ambalo litaona matukio yenye mguso wa kimataifa, kikanda na mahalia, kila moja yakihusishwa na lengo maalum la Waraka wa Laudato si' na sekta saba za Jukwaa la  Laudato sì. Yote yatahusu dhana ya ikolojia shirikishi. Ushiriki wa mamia kwa maelfu ya Wakatoliki watakaounganika ili kuimarisha juhudi za Jukwaa la Mipango unatarajiwa. Hiki ni chombo kipya kinachoruhusu taasisi, jumuiya na familia kutekeleza kikamilifu Hati ya Papa. Kwa maana hiyo JUma hili linaanza tarehe 22 hadi 29 Mei 2022.

Bioanuwai, migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa, kukaribisha maskini

Miongoni mwa masuala muhimu yatakayochunguzwa ni  jinsi Wakatoliki wanavyoweza kukabiliana na anguko la bayoanuwai; jukumu la nishati ya mafuta katika migogoro na na kipeo cha mabadiliko ya tabianchi; jinsi gani wananchi wote wanavyoweza kuwakaribisha maskini katika maisha yao ya kila siku. Miongoni mwa mazungumzo yaliyopangwa kufanywa, pia kuna moja inayolenga uwezekano wa kutoa nguvu kwa sauti watu wa Asilia  ambayo itashuhudiwa ushiriki wa Sr. Alessandra Smerilli, Katibu  Mkuu wa Baraza la  Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Mpango unalenga kuongeza sauti za kiasili

Jibu la kilio cha Dunia ni mada itakayoguswa siku ya Jumatatu tarehe  23 Mei na mipango ambayo itaonyshwa moja kwa moja kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Australia kilichopo Roma. Kitazungumzia jinsi ya kusawazisha mifumo ya kijamii na asili na itaona ushiriki wa Padre Joshtrom Kureethadam akitoa mchango wake ambao utazingatia ongezeko la sauti za kiasilia kwa kuzingatia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bayoanuwai utakaofanyika mwaka huu.  “Kusaidia ECO-Jumuiya: Kukaribisha maskini” hii itakuwa mada ya siku inayofuata. Jumatano, Mei 25 itajikita na suala la uchumi wa ikolojia, uliopungua chini ya kipengele cha nishati ya mafuta, vurugu na shida za tabianchi. Alhamisi tarehe 26 Mei,  itaendelea na kupitishwa kwa mitindo ya maisha endelevu: uwekezaji unaoendana na imani. Onesho la filamu ya hali halisi kuhusu Laudato si' itaoneshwa Ijumaa alasiri,  tarehe 27 Mei. Jumamosi jioni, Mei 28 eneo la kiroho la ikolojia litachunguzwa. Dominika tarehe 29 Mei itahitimishwa kwa mada ya uthabiti na uwezeshaji wa jamii kama sehemu ya safari ya sinodi. Mkutano wa sala umepangwa kufanyika saa 3 usiku katika siku hiyo ya mwisho.

Wazungumzaji wa kimataifa

Kati ya Wazungumzaji wengine ni pamoja na: Theresa Ardler, Afisa Uhusiano wa Utafiti wa Watu wa Assili katika Chuo Kikuu cha katoliki cha Australia, mkurugenzi na mmiliki wa Gweagal Cultural Connections; Vandana Shiva, mwanzilishi wa Taasisi ya Utafiti ya Navdanya ya Sayansi, Teknolojia na Ikolojia nchini India na Rais wa Kimataifa wa Navdanya ; Angela Manno, msanii aliyeshinda tuzo; Greg Asner, mkurugenzi wa Kituo cha ASU cha Ugunduzi na Sayansi ya Uhifadhi Ulimwenguni. Mpango kamili wa  Juma la Laudato Si unaopatikana kwenye kiungo cha LaudatoSiWeek.org, unajumuisha matukio mengine nchini Uganda, Italia, Ireland, Brazil na Ufilipino, isipokuwa filamu ya hali halisi itatangazwa kwenye Facebook na vituo vya YouTube vya Harakati ya Laudato Si' .

20 May 2022, 15:20