Tafuta

2021.03.08 Mons. Gallagher 2021.03.08 Mons. Gallagher 

Gallagher:mazungumzo na udugu ni mambo mawili muhimu ili kushinda migogoro ya sasa!

Hotuba yake Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Nchi katika Mkutano kuhusu “Utamaduni wa kukutana:Chachu katika ulimwengu uliogawanyika”, uliohamasishwa na Chuo Kikuu cha Georggetown na Civiltà Cattolica,amesema mazungumzo na udugu ni taa mbili muhimu kwa ajili ya kushinda migogoro ya sasa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuelimisha utamadununi wa kukutana maana yake ni kuelimisha sanaa ya harakati kuelekea amani, kwa kumtoa mtu nje yake, mataifa, na watu wanaokumbwa na vita ili kuwapelekea katika njia ya mazungumzo na kutafuta wema wa pamoja. Huu  Ujumbe wa Askofu Mkuu Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusinao na Ushirikiano na Mataifa katika Mkutano kuhusu: “Utamaduni wa kukutana:chachu kwa ajili ya ulimwengu uliogawanyika”, uliondaliwa huko Villa Malta, Roma na Civiltà Cattolica kwa ushirikiano na  Chuo Kikuu Georgetown. "Ni lazima kukubali leo hii kwamba tunaishi katika ulimwengu ambao daima unaongozwa kidogo na utamaduni wa kukutana na kwa kuendelea namna hivyo, kuna hatari kwamba ulimwengu wetu unakufa kwa sababu ya ubinafsi", alisema Askofu Mkuu Gallagher.

Utambuzi wa hadhi ya binadamu

Katibu wa Vatican wa mahusiano, amenukuu kwa maana hiyo maneno ya Papa Francisko ambaye anawaalika ulimwengu kushinda utamaduni wa kutupa na kubagua ili kuendeleza utamaduni wa kukutana, kwa kukataaa utandawazi wa sintofahamu, na utandawazi wa kidugu. Askofu Mkuu Gallagher alikumbushaa kuwa leo hii Vatican, kwa njia ya diplomasia yake iliyo hai ni mwanachama wa Mashirika ya Kimataifa, ambapo hushiriki mikutano ya kimataifa inahitijika kufuatilia mbinu za Kimataifa na kuendelea kuhamasisha utambuzi wa hadhi ya mtu, amani na maelewano kati ya Mataifa.  Vile vile alibainisha kuwa Vatican kwa haraka imejikita kutendeleza kile ambacho ni diplomasia ya mataifa mengi, karibu kwa mantiki za kiutamaduni zaidi kwa nchi zote.

Ulimwengu unakatishwa na ukosefu wa msimamo

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Vatican, amesema kuwa katika Jumuiya ya Mataifa inapokosekana utamaduni wa kukutana, watu peke yake, tabaka, utambulisho wa nguvu unachukua nafasi katika ulimwengu kwa kuwabagua wadhaifu zaidi na kulundikana kwa mivutano inayozaliwa kutokana na kujisikia na vita. Kwa maana hiyo jamii haina amani kwa sababu ya kukosa upendo; na ni ubinafsi, hakuna kujifungulia shida za wengine. Askofu Mkuu Gallagher, aliwaalika  kwa maana hiyo kusimika katika mtazamo endelevu wa ulimwengu na kujiuliza juu wakati ujao wa ubinadamu. Ulimwengu unakatishwa na ukosefu wa msimamo na hofu ya kile ambacho kinaweza kusababisha vita vya ulimwengu, hasa kwa kuchukua maneno ya Papa Francisko ili kueleza kwamba mazungumzo na udugu ni taa mbili msingi kwa ajili ya kushinda mizizo ya wakati uliopo. Ni lazima kufikiria pia namna ya kutazama, ya mawazo ya maendeleo, ya ukuaji, ya utandawazi na jitihada ya kupima ukuaji katika maana tofauti  ya ile ya uhusiano wa idadi, ili kufikia kuelekeo unaojifafanua.

Kupyaisha uwajibikaji wa kimataifa

Askofu mkuu amebainisha ni kwa jinsi gani ambavyo sasa kuna ugomvi ambao hakuna anayejua unaweza kuzaa kitu gani ambapo kamwe haikuwahi kutokea kama leo hii katika siasa ambapo utafikiri ni kuchagua tabaka la uongozi wenye maono kidogo. Katika maoni yake  amesisitiza kuwa lazima hasa kukabiliana na janga la mgogoro wa utamaduni ili kuweza kupata demokrasia na kutoa uaminifu wa kisiasa. Kwa kuhitimisha, Askofu Mkuu Ghallagher alitumia tena  maneno ya Papa Francisko katika fursa ya miaka 75 tangu kuzaliwa kwa  Umoja wa Mataifa, alipobainisha kuwa: "Kuondoka katika  mgogoro hauwezi kutoka unafanana, kwa sababu kuna uwezekano wa aina mbili; mmoja unaopelekea kuongeza juhudi za kimataifa kama vile kupyaisha uwajibikaji ulimwenguni, na pili kuondoa utaifa na kujibagua kwa kuwabagua maskini zadi na walio katika mazingira magumu, ya wakazi wa pembezoni mwa maisha. 

Waathirika wa vita ni wengi 

Akijibu hata hivyo swali mojo mara baada ya hotuba yake, Askofu Mkuu, Gallagher alithibitisha kuwa migogoro ya sasa barani Ulaya, kwanza waathirika wa vita ni wa ukweli na alimalizia akisisitiza kuwa vita hivyo vimeweka bayana uwepo wa silaha za kinyukilia akiwa na matumain kwamba wanaweza kubadilisha kuwa fursa ya kuruhusu mwisho wa mantiki inayojikita utengezaji wa nyuklia.

 

29 May 2022, 17:31