Tafuta

2022.05.20 Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na Nchi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje  Dmytro Kuleba, katika mkutano na waandishi huko Kyiv 2022.05.20 Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na Nchi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Dmytro Kuleba, katika mkutano na waandishi huko Kyiv 

Askofu Mkuu Gallagher:amani ni zawadi ya Mungu,watu lazima kuifanyia kazi daima

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano wa Nchi alizungumza na waadishi wa habari mara baada ya Mkutano na Waziri wa mambo ya Nchi za Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba:Vatican inasisitiza uwezekano wake wa kusaidia mchakato wa kweli wa mazungumzo.Tukio la kutisha la Bucha linaeleza wazi kuwa amani haiwezekani kufikiria ni jambo la kawaida lazima

Na Angella Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Ushirikiano na Nchi akizungumza na waandishi wa Habari huko Kiev  mara baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ukraine Bwana Dmytro Kuleba amesema kuwa ziara yake imemruhusu kugusa kwa mkono wake majeraha ya Nchi hiyo. Kauli hiyo ni mara baada ya kutembelea miji ya mashahidi wa vita huko Bucha, Vorzel e Irpin”.

Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ukraine
Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ukraine

Akizungumzia ziara kwa maana hiyo alisisitiza inataka kuonesha ukaribu wa Vatican na Papa Francisko kwa watu wa Ukraine kwa namna ya pekee katika mwanga wa uvamizi huo wa Urussi dhidi ya Ukraine.  Na pia ni mwendelezo wa umakini maalum wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya Ukraine kushuhudia kwa kumtuma Kardinali Konrad Krajewski,  Mwenyikiti wa Sadaka ya Kitume ya Papa na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ukraine
Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ukraine

Akifafanua, Askofu Mkuu alisema huko Bucha , iliyotekea mambo yasioelezeka barani Ulaya na kwa bahati mbaya, itaingia katika historia ya karne ya XXI. Ni mwamko wa kweli kwa sisi sote kusema: 'msichukulie amani kuwa kitu cha kawaida'. Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini pia ni jambo ambalo wanaume na wanawake wenye mapenzi mema, bila kujali dini au vyama vya siasa, wanapaswa kulifanyia kazi daima. Na ikiwa hatufanyi hivyo, tunafanya kuwa hatari yetu wenyewe, kama Bucha inavyoonesha kwa ufasaha ”.

Kufuatilia lengo la amani

Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza uchungu mkubwa wa Papa kwa vifo vingi, vurugu za kila aina, uharibifu wa miji, kutenganishwa kwa familia na kwa wakimbizi wengi. Akirejea majaribio ya kutafuta njia za haraka za kumaliza mzozo usio na maana Ukraine, Katibu wa Mahusiano na Mataifa amesisitiza kwamba “imani kwa Mungu na ubinadamu hutuongoza kudumu katika kufuata lengo la amani kupitia sala, maneno na vitendo bila kujiruhusu kushindwa na changamoto hii kubwa.”

Vatican kuingilia kati kupatanisha,  lazima kipokee mwaliko kutoka pande zote mbili

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Gallagher alisema kuwa Vativcan inasisitiza, kama ilivyofanya siku zote, nia yake ya kupendelea mchakato wa kweli wa mazungumzo, ikizingatia kuwa njia sahihi ya azimio la haki na la kudumu, lakini ili kupatanisha lazima ipokee mwaliko kutoka sehemu zote mbili. Kanisa, linajaribu kujibu mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya idadi ya watu, mara moja na kwa muda mrefu. Askofu Mkuu Gallagher hatimaye alitoa  shukrani zake kwa mamlaka ya Ukraine na kutoa shukrani za dhati kwa Kanisa Katoliki na Makanisa mengine na mashirika ya kidini kwa kujitolea kwao kwa amani na mshikamano, kwa matumaini kwamba watapata msaada wanaohitaji sana na kwamba juhudi za pamoja za ulimwengu wote hivi karibuni zitakomesha uharibifu na kifo .

21 Mei 2022, 17:10