Tafuta

2022.04.22 Kardinali Stanislaw Dziwisz, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Krakow. 2022.04.22 Kardinali Stanislaw Dziwisz, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Krakow. 

Vatican:Suluhishi la mashtaka dhidi ya Dziwisz kuhusu kesi za unyanyasaji

Kadinali wa Poland alikuwa ameshutumiwa kwa kuficha habari.Mnamo Julai 2021,Kardinali Bagnasco alitumwa Poland kuthibitisha shughuli zake wakati wa huduma yake kama Askofu mkuu wa Krakow.Kulingana na uchambuzi wa nyaraka zilizokusanywa,Vatican imeamua kutoendelea zaidi.Dziwisz:"Zilikuwa shutuma zenye uchungu dhidi yangu.Asante kwa uamuzi sahihi”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Zimehakikishwa shughuli za Kardinali Stanisław Dziwisz kuhusu kesi za unyanyasaji wakati wa huduma yake kama Askofu Mkuu wa Krakow (2005-2016) na kukuta hakuna makosa yoyote . Baraza la Kitaifa linathibitisha hili baada ya kuchunguza nyaraka zilizoundwa na Kardinali Angelo Bagnasco, mjumbe wa Vatican nchini Poland tarehe 17-26 Juni, 2021 kwa usahihi ili kuhakiki baadhi ya masuala yanayohusiana na shughuli za kardinali, kwa miaka arobaini akiwa katibu binafsi wa Mtakatifu Yohane Paulo II. Uchambuzi wa nyaraka zilizokusanywa ulifanya iwezekane kutathmini shughuli hizi za Kardinali Dziwisz kama sahihi na kwa hivyo Baraza la Kitaifa liliamua kutoendelea zaidi, kama, inavyosomeka maelezo mafupi kutoka katika Ofisi ya Kitume nchini Poland iliyotolewa alhamisi 22 Aprili 2022.

Miaka miwili iliyopita, wakati ambapo maandamano makali yalipozuka dhidi ya Kanisa la Poland kuhusu suala la nyanyaso za kijinsia kwa upande wa Makuhani, kufuatia kuchapishwa kwa baadhi ya filamu, Dziwisz alishutumiwa kwa kuficha malalamiko ya kuhani aliyedhulumiwa na kasisi rafiki wa familia hiyo. Katika utangazaji wa hali halisi katika mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya televisheni vya binafsi nchini Polandi, ilidaiwa pia kwamba kadinali huyo angeficha ukweli fulani wa unyanyasaji ili kubadilishana na matoleo kwa ajili ya Kanisa.

Kardinali daima alikataa mashtaka yoyote na kuyaita kashfa; yeye mwenyewe basi akaomba kuunda tume huru ambayo inaweza kufafanua ukweli uliobainishwa. “Nitakuwa tayari kushirikiana na tume kama hiyo. Ningependa kuwasilisha ukweli kwa uangalifu”, alikuwa emesema. Huku katikati kukiwa na mizozo mikali kutoka kwa waandishi wa habari na hata wanasiasa, rais wa Baraza la Maaskofu, Askofu Mkuu Stanisław Gądecki, pia aliingilia kati suala hilo, akiomba kwamba shutuma zozote zifafanuliwe na Tume yenye uwezo ya Makao ya Vatican. “Wakati huo huo ningependa kusisitiza kwamba Kanisa la Poland linamshukuru kardinali kwa miaka mingi ya huduma na Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa amesema mkuu huyo wa Kanisa.

Mnamo Julai 2021, Vatican iliamua kumtuma Kardinali Bagnasco kwenda Poland kuchunguza kesi ambazo, kama ilivyoripotiwa na Ubalozi, pia zilijitokeza hadharani. Katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican iliripoti kuwa Askofu mkuu mstaafu wa Genova wakati wa utume wake alichunguza nyaraka na kufanya mfululizo wa mikutano. Ripoti yake juu ya ziara hiyo itatumwa Vatican”. Miezi tisa baadaye, kwa msingi wa uchanganuzi wa kazi iliyofanywa na Kadinali Bagnasco, Vatican kwa hiyo inamwondolea Dziwisz mashitaka yote.

Askofu Mkuu Mstaafu wa Krakow alionesha kuridhika sana na zaidi ya yote shukrani kwa wale wote waliochangia kujibu kwa uwajibikaji kwa tuhuma zilizotolewa dhidi yake wakati wa utume wake wa kichungaji kama Askofu Mkuu wa Krakow. Shukrani pia kwa Bagnasco ambaye alifanya kazi kufafanua tuhuma zilizotajwa hapo juu, ambazo hazikustahili na zenye uchungu kwake, ameanddika Dziwisz katika barua. “Natumaini kwamba tangazo kutoka Vatican kwa ofisi ya Kitume nchini Poland iliyochapishwa tarege 22 Aprili sio tu itachangia ili kufafanua swali hilo, lakini pia kurejesha utulivu kwa wale wote waliohisi kukerwa na shutuma zilizotolewa dhidi yake.

22 April 2022, 19:00