Tafuta

Biashara mbaya ya binadamu. Biashara mbaya ya binadamu. 

Vatican:kuunganisha jitihada dhidi ya matukio ya biashara haramu

Monsinyo Janusz Urbańczyk Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendelo Barani Ulaya (OSCE) katika hotuba yake kwenye meza ya duara ya kikao cha 22,kilichoandaliwa na Urais wa Poland cha OSCE,huko mjini Vienna,Uswiss amesisitiza kwamba lazima kuongeza miundo mipya ya ulinzi na usaidizi kwa waathirika wa biashara haramu ya binadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutokana na kuongezeka kwa wimbi kubwa kwa uhamiaji wa watu katika kutafuta amani na wakati ujao wenye usalama, wakiwemo wengi kwa sababu ya vita nchini Ukraine, inaonesha dharura ya ulazima wa msimamo wa suluhisho la kudumu na mifumo ya usalama, kwa namna ya pekee kwa kusaidia waathirika na ulinizi wa wahamiaji wadhaifu. Amesisitiza hayo Monsinyo Janusz Urbańczyk Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendelo Barani Ulaya (OSCE) katika hotuba yake kwenye meza ya duara ya kikao cha 22, kilichoandaliwa na Urais wa Poland cha OSCE, huko mjini Vienna, Uswiss mkutano kuhusu kuthibiti biadhara mbaya ya wanadamu kwa kuongoza na mada “Ulinzi: kusaidia haki kwa waathirika na kuongeza nguvu ya usaidizi.

Lazima kusonga mbele kupambana na biashara mbaya ya binadamu

Kwa mujibu wa Vatican, Mataifa lazima yaongeze nguvu mara mbili ili kuweza kuelewa na kuongeza mitindo mipya ya ulinzi na msaada. Lazima kuongeza nguvu ili kukabiliana na janga baya sana la biashara mbaya ya binadamu. Katika hotuba yake nyingine ambayo imejikita kwenye mada hiyo hiyo, Monsinyo Urbanczyk, baadaye amesisitiza kuwa nyakati za matatizo ya kiuchumi na kifedha, baadhi ya serikali zinaweza kutoweka fedha za kuweza kubamba dhidi ya biashara mbaya ya binadau na kulindwa waathirika. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba fedha hizo zinahitajika ili kusaidia mipango ya umma na ya kibinafsi ambayo inalinda, kusaidia na kuunganisha waathirika na kuhakikisha usalama wa kitaifa na kikanda. Na alikumbuka, hasa, maneno ya Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video wa mwaka huu kwa Siku ya Dunia ya Sala na Tafakari Dhidi ya Usafirishaji haramu wa binadamu: “Tusonge mbele katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu na aina zote za utumwa na unyonyaji. Ninawaalika nyote kuweka hasira hai, wekeni hasira hai! na kila siku kutaguta nguvu ya kujitolea kwa uamuzi stahiki juu ya suala hili. Msiogope mbele ya kiburi cha jeuri”.

Katika Nchi zenye kipato cha chini watoto ni nusu ya waathirika

Kwa mujibu wa Monsinyo Urbanczyk, Mikataba ya kimataifa, maelekezo kikanda, kanuni na sheria mbalimbali za kitaifa inatambua hitaji la kuwalinda watoto na kulinda maslahi bora ya mtoto”. Kwa bahati mbaya, haya yote bado hayatoshi kuwalinda watoto dhidi ya kusafirishwa. Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2018 katika maadhimisho ya Kongamano la Kitaifa huko  Mexico kuhusu uhamiaji wa kimataifa, alionesha uangalifu wa pekee unaopaswa kulipwa kwa watoto wahamiaji, familia zao, waathirika wa mitandao ya biashara ya binadamu na wale ambao wamekimbia makazi yao kutokana na migogoro na majanga ya asili na mateso. “Wote wanatumaini kuwa tuna ujasiri wa kubomoa ukuta wa ule ushirika wa starehe na wa kimya ambao unazidisha hali yao ya kuachwa na kwamba tunapaswa kuweka umakini wetu, huruma yetu na kujitolea kwetu kwa ajili yao”. Biashara mbaya ya watoto, kwa mujibu wa Monsinyo JanuszUrbanczyk umezidi kuongezeka. Kwa ngazi ya Ulimwengu, mwathirika mmoja kati ya watatu ni mtoto. Katika nchi zenye kipato cha chini, watoto ni nusu ya waathirika. Kwa hivyo, alihitimisha akisema kwamba ni muhimu kusasisha mara kwa mara kanuni za kimataifa na kitaifa ili juhudi za pamoja za kulinda watoto sio tu kuzingatia data muhimu zaidi na za kisasa, lakini zaidi ya yote, ziwe na ufanisi.

UTHIBITI WA BIASHARA MBAYA YA BINADAMU
07 Aprili 2022, 16:30