Tafuta

Kuna tishio kubwa la nyuklia, linaloikabili sayari.Kamwe usiwe wa kwanza kutumia silaha za nyuklia,na ufanye juhudi kwa upya za kufikia makubaliano yanayoweza kuthibitishwa ambayo yanazuia mbio za silaha. Kuna tishio kubwa la nyuklia, linaloikabili sayari.Kamwe usiwe wa kwanza kutumia silaha za nyuklia,na ufanye juhudi kwa upya za kufikia makubaliano yanayoweza kuthibitishwa ambayo yanazuia mbio za silaha. 

Vatican:Kujenga mfumo wa usalama wa pamoja bila silaha za nyuklia

Taasisi ya Kipapa ya Elimu Sayansi imechapisha hati ndefu kuhusu kuzuia vita vya kinyuklia,kwa kuorodhesha hatari ambazo zinaweza kuwapo kwa ubinadamu wote.Ni hatua tisa na miito minne ya kwa viongozi wa kitaifa na kikanda,kwa wanasayansi na wanaume na wanawake wa kila kona ya ulimwengu.Sayansi zisaidie kuishi amani,kusimamisha ununuzi wa vifaa hivyo vya kuhatarisha binadamu na sayari.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Chuo cha Kipapa cha Elimu ya Sayansi kimezungumza dhidi ya hali ya kutisha ambayo ulimwengu umeshuhudia kwa zaidi ya siku arobaini nchini Ukraine na kuchapisha tamko refu juu ya kuzuia vita vya nyuklia, lililopuuzwa kwa muda mrefu kwa maneno ya Papa Paulo VI na Yohane Paulo II na wito wa hivi karibuni wa Papa  Francisko. Kimsingi Wito ni kwa viongozi wa kitaifa, kuchukua hatua ya kumaliza vita vya Ukraine mara moja na kuanzisha azimio la amani, wakiangalia zaidi ya masuala finyu kwa faida ya taifa. Baadaye ni kwa wanasayansi, kujitahidi kutengeneza mbinu za kivitendo za udhibiti wa silaha, na vilevile kwa viongozi wa kidini, kuendelea kutangaza kwa nguvu na kwa kudumu masuala mazito ya kibinadamu yaliyo hatarini. Hatimaye, wito ni kwa wanaume na wanawake duniani kote kupambana vita moja tu ile dhidi ya kuamini kwamba vita ni lazima.

Ukosefu wa usawa kati ya mataifa na ndani ya mataifa

Ukosefu mkubwa wa usawa kati ya mataifa na ndani ya mataifa, matamanio ya kitaifa au ya kishirikina yenye maono mafupi, na uchu wa madaraka ni mbegu za mzozo unaoweza kusababisha vita vya jumla na vya nyuklia, linaonya Taasisi ya Vatican, na inaorodhesha hatari za “Tishio kubwa la nyuklia, kama ilivyoibuliwa na Urussi kwa wakati huu wa vita vinavyoendelea huko Ukraine. Kwanza kabisa, hatari inayoongezeka kwamba nchi nyingine nyingi na vikundi vya kigaidi vinaweza kupata silaha za nyuklia au kukuza uwezo wa kuzizalisha. Taasisi ya Kipapa aidha inaeleza juu ya uharibifu wa kukusudia au bila kukusudia wa vinu vya nguvu za nyuklia na matokeo mabaya kwa idadi kubwa ya watu, upotezaji usiodhibitiwa wa taka za nyuklia ambazo zinaweza kutumika kwa kinachojulikana kama mabomu machafu, matumizi ya uwezo kwa kile kinachojulikana kama silaha za nyuklia za busara katika uwanja wa vita. Tena, utunzaji wa silaha za nyuklia katika hali ya tahadhari ya hali ya juu, wa  kuongeza uwezekano wa kuzinduliwa kwa silaha za nyuklia kwa bahati mbaya au kama matokeo ya utumiaji wa kompyuta. Isitoshe, hatari ya utumiaji wa silaha zenye nguvu za nyuklia na zingine kimataifa zaidi ya Ukraine, wakati na ikiwa vita vitaongezeka zaidi.

Tamko la kuzuia vita vya nyuklia 1982

Chuo cha Kipapa cha kisayanisi kilikuwa tayari kimeshughulikia suala hilo katika “Tamko la kuzuia vita vya nyuklia, lililoandaliwa mnamo 1982 na marais wa Vyuo na wanasayansi kutoka ulimwenguni kote. Kauli nyingi zinabaki kuwa za mada, lakini hali ya ulimwengu imebadilika na hata kuwa mbaya zaidi, kuanzia na ukweli kwamba kutokuaminiana na tuhuma kumeongezeka kati ya Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini, na kati ya wakubwa na wenye nguvu wa Marekani, China, Umoja wa Ulaya (EU) na Urussi.  Baadaye zinarekodiwa kashfa ya umaskini, njaa na uharibifu ambao wenyewe unazidi kuwa tishio linaloongezeka kwa amani. Na inashuhudiwa kuzuiwa kwa uzalishaji wa kilimo nchini Ukraine na biashara ya chakula kutoka Ukraine na Urussi ambayo inazidisha mgogoro wa chakula duniani.

Sayansi itumike kumsaidia mwanadamu na sayari nzima

Kwa kutambua haki asilia ya mwanadamu ya kuishi, na kuishi kwa hadhi na utu na kutamani furaha, sayansi lazima itumike kumsaidia mwanadamu kuelekea maisha ya ustawi, utimilifu na amani, kinabainisha Taasisi ya Kipapa cha Sayansi. Badala yake, kinachoonekana ni kukuza uwezo wa silaha za nyuklia, lakini pia wa makombora ya kemikali, ya kibaolojia au ya hali ya juu ambayo yameundwa kukwepa mifumo ya ulinzi iliyopo. Hali mpya ambayo inahusisha hasara kubwa ya ubinadamu na uhuru, pamoja na mazingira magumu zaidi, sio tu ya watu binafsi, hasa wasiokuwa wapiganaji, kama vile watoto, wanawake, wazee na wagonjwa bila ubaguzi au kulazimishwa, kuhama, lakini ya sayari nzima, wanasisitiza.

Tatizo la Sayansi na dhamiri

Katika waraka huo unaonesha kuwa ni tatizo la sayansi na dhamiri. Kwa hakika dhamiri, haiwezi kuhalalisha matumizi ya nguvu haribifu zinazosababisha kifo kila mahali ili 'kustaarabu' na 'kufanya maadili' au kuchukua tu. Kwa upande wake, sayansi ina wajibu wa kusaidia kuzuia upotoshaji wa mafanikio yake. Utafiti na sayansi juu ya kushinda na kuzuia vita, na sayansi ya kukuza amani, lazima itafute kutokuwepo kwa vita na ndiyo lazima liwe lengo la wote, na taaluma za kisayansi. Kwa upande mwingine, viongozi na serikali wana wajibu wa kuepuka kwa kila njia janga la vita kinasisitiza Chuo cha Vatican. Jambo ambalo linatia shaka ubinadamu wenyewe"kuchukua hatua kwa ajili ya kuendelea kuishi, kuendeleza mazungumzo, sheria za kimataifa, mazungumzo, na njia nyingine zozote za amani.

Hatua 9 ambazo zinaweza kuchukuliwa kimataifa

Kwa upande wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi kimeorodhesha mambo tisa ya  kupiga hatua za kimataifa: “Heshimu kanuni kwamba nguvu au tishio la nguvu halitatumika dhidi ya uadilifu wa eneo au uhuru wa kisiasa wa nchi nyingine”; “Kuzuia matumizi ya nguvu kama njia ya kusuluhisha la migogoro ya kimataifa, kwani ina hatari ya kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi, pamoja na matumizi ya vita vya nyuklia, kemikali na kibaolojia”; “Kutoa makazi na ulinzi kwa mamilioni ya wakimbizi kutoka duniani kote”; Kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia katika nchi zingine, ambayo inaweza kusababisha, pamoja na mambo mengine, ugaidi wa nyuklia. Aidha, kamwe usiwe wa kwanza kutumia silaha za nyuklia, na ufanye juhudi kwa upya za kufikia makubaliano yanayoweza kuthibitishwa ambayo yanazuia mbio za silaha; Kutafuta njia bora zaidi na njia za kuzuia kuenea zaidi kwa silaha za nyuklia”; “Kuzuia matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia dhidi ya kuelekezwa kwenye kuenea kwa silaha za nyuklia”; “Kuchukua hatua zote za kivitendo zinazopunguza uwezekano wa vita vya nyuklia ambavyo kwa bahati mbaya, makosa au hatua zisizo za busara zinajionesha. Hatimaye, mwaliko wa mwisho ni “Kuendelea kuzingatia mikataba iliyopo ya kukomesha kwa silaha, kwa lengo la kujenga mfumo wa usalama wa pamoja ambao silaha za nyuklia hazina nafasi.

WITO WA TAASISI YA KIPAPA YA SAYANSI KUHUSU TISHIO LA KINYUKLIA
09 April 2022, 16:50