Vatican katika Osce yahimiza kuhakikishia usalama wa wathirika wa biashara ya binadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican
Mara nyingiutamaduni wa kutokujali na ubaguzi unawazungukia waathirika wa biashara haramu ya watu kwa kuwafanya wasioonekana. Ili kuweza kupambana hali hizi, waathirika lazima wapokelewa, wasindikizwe na kulindwa kwa huruma na mshikamano. Na zaidi serikali lazima ziboreshe hupatikanaji wa huduma msingi kwa wahanga wa biashara mbaya ya binadamu na kuhakikisha kwamba wanapata ulinzi unaostahiki, usaidizi wa kisheria na njia zinazofaa za malipo au marejesho. Huu ni mwaliko wa Monsinyo Janusz Urbańczyk Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendelo Barani Ulaya (OSCE) katika hotuba yake kwenye meza ya duara ya kikao cha 22, kilichoandaliwa na Urais wa Poland cha OSCE, mnamo tarehe 4 Aprili 2022 huko mjini Vienna, Uswiss ili kujenga mifumo madhubuti ya ulinzi kwa waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu.
Lengo kuu la kuzuia biashara mbaya ya binadamu na ulinzi sitahiki
Mwakilishi wa Kudumuwa Vatican alisisitiza umuhimu wa mjadala huo kwa kuzingatia changamoto zilizoletwa na janga la UVIKO-19 na vita vinavyoendelea nchini Ukraine,na kutoa wito kuwa macho zaidi! mbele ya hatari hiyo iliyobainishwa wazi na mjumbe maalum wa Papa Francisko, Kardinali Michael Czerny, wakati wa ziara yake ya hivi majuzi nchini Hungaria na hasa katika mji wa Berehove, kwamba wakimbizi wa Ukraine, hasa wanawake na watoto, watatekwa nyara na kunyonywa na wasafirishaji haramu wa binadamu, wanaojaribu kuwatia utumwani walio hatarini kwa kuwapa msaada kwa uwongo na kisha kuwatega”. Monsinyo Urbańczyk pia alikumbusha juu ya dhamira na juhudi zinazofanywa na serikali za kitaifa katika kuzuia biashara mbaya sana na katika ulinzi wa waathirika wa kile alichokiita “uhalifu mbaya, juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia, pamoja na zile za Kanisa Katoliki na mamia ya Mashirika ya Kitwa ya kike na kume pamoja na mashirika ya walei ambayo hutoa makazi salama kwa watu hawa na kufanya kazi kwa ushirikiano wao wa kijamii.
Inahitajika kupunguza hatari ya kudhulumu na matumizi ya kuhamisha kiholela
Mwakilishi wa kudumu wa Vatican Monsinyo Janus alisisitiza haja ya taratibu za kisheria kuwalinda ndugu na marafiki wa waathirika, ambao mara nyingi hujikuta wakipata 'athari za pili za usafirishaji haramu wa binadamu', kama vile unyang'anyi na hali ya kuachwa na jamii, kwa maana hiyo kipaumbele cha kushughulikia na kupunguza hatari ya kudhulumiwa tena, kuonya dhidi ya matumizi ya uhamishaji holela 'uliodhibitiwa' wa waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Monsinyo Urbanńczyk alihitimisha kwa kuzitaka nchi kwa mara nyingine tena kushirikiana ili kuhakikisha matibabu ya kutosha kwa waathirika wa biashara haramu ya binadamu.