Tafuta

2022.04.22 Monsinyo Mirosław Wachowski,Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Nchi (wa nne kutoka kushoto). 2022.04.22 Monsinyo Mirosław Wachowski,Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Nchi (wa nne kutoka kushoto).  

Vatican an Vietnam wakutana na Kikundi cha pamoja:upo uhusiano chanya

Katika siku ya tarehe 21 na 22 Aprili 2022 huko Ha Noi, Vietnam,kumefanyika mkutano wa mazungumzo na wawakilishi walioongozwa wote pamoja na Ha Kim Ngoc,Makamu waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Monsinyo Mirosław Wachowski,Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na Nchi.Katika mkutano huo wamebainisha hatua za kutimiza hasa ofisi ya Mwakilishi wa Kipapa Mkazi huko Hanoi.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni kuhusu mkutano wa Kikundi cha pamoja kati ya Vietnam na Vatican, uliofanyika huko Ha Noi kwa tarehe 21 na 22 aprile 2022, amethibitisha kuwa  uliongozwa pamoja na Bwana Ha Kim Ngoc, Makamu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje,  Mkuu wa Uwakilishi wa Vietnam na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Uhusiano na Ushirikiano na Nchi, ambaye alikuwa ni Mkuu wa Uwakilishi wa Vatican. Kwa sehemu zote mbili wamekuwa na mazungumzo mapana na kushirikishana kwa karibu kuhusiana na uhusiano kati ya Vietnam na Vatican kwa kuhitimisha na masuala yanayotazama Kanisa Katoliki nchini Vietnam. Pande zote mbili zilitambua kuwa uhusiano wa Vietnam na Vatican una maendelea mazuri licha ya matatizo yaliyotokana na vizingiti vya bara kwa sababu ya janga la Uviko-19, lakini kulikuwa daima na mawasiliano na maono endelevu.

Matarajio ya ufunguzi wa ofisi ya Kipapa huko Hanoi

Kwa pande zote mbili aidha wamekubaliana kuwa mahusiano kati yao yanapaswa kuendelea kubaki katika misingi ya kisasa ya ushirikishi na juu ya mazungumzo yenye kuzaa matunda kwa lengo la kuimarisha imani ya pamoja iliyojionesha na kuongeza nguvu za uhusiano kwa sehemu zote katika jumuiya Katoliki nchini Vietnamu. Vile vile kwa pande zote mbili ziliafikiana makubaliano juu ya masuala muhimu ya kuinua, kwa siku za usoni, kiwango cha mahusiano kati ya Vietnam na Vatican hasa kweza kuwa na Mwakilishi wa Kipapa asiye mkazi hadi kufikia Mwakilishi Mkazi wa Kipapa na kukubaliana juu ya hatua za baadaye zitakazo chukuliwa kuanzisha ofisi ya Mwakilishi wa Kipapa Mkazi huko Hanoi.

 Vatican iko makini kwa Jumuiya Katoliki Vietnam

Hata hivyo Vatican linafuatilia kwa umakini juu ya maisha ya kina na changamfu ya Jumuiya katoliki nchini humo na kuhimiza Kanisa Katoliki nchini Vietnam kuchangia katika manufaa ya ustawi wa wote wa Vietnam, kama ambavyo Jumuiya katoliki imeweza kushuhudia kwa dhati katika kipindi kigumu zaidi cha janga la uviko, kujitolea katika hospitali na kusaidia mahitaji ya wale wanaohitaji. Mkutano huo ulifanyika katika hali ya utulivu na heshima na wakaweza kukubaliana hata kuhitisha mkutano wa X wa Kikundi cha Kanisa cha pamoja kati ya Vietnam na Vatican. Tarehe ya mkutano hata hivyo itatangazwa baadaye kupitia nafasi ya kidiplomasia. Katika fursa hiyo uwakilishi wa Vatican pia umefanya ziara ya faragha kwa baadhi ya Mamlaka ya Nchi na ambapo pia atakutana kwa siku zijazo na wajumbe wa Baraza la maaskofu wa Vietnam ambao wako wanafanya mkutano wao wa mwaka huko Thai Binh.

22 April 2022, 16:02