Tafuta

Uwezekano wa Papa kwenda nchini Lebanon unafanyiwa utafiti. Uwezekano wa Papa kwenda nchini Lebanon unafanyiwa utafiti. 

Uwezekano wa ziara ya Papa kwenda Lebanon unafanyiwa utafiti

Kwa mujibu wa Msemaji wa vyombo vya habari Vatican,mara baada ya tweet ya Rais wa Lebanon Bwana Aoun kuhusu uwezekano wa ziara ya Papa Francisko katika Nchi ta Mierezi,amebainisha kwamba uwezekano huo unafanyiwa utafiti.

VATICAN NEWS

Akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari juu ya uwezekano wa safari ya Papa kwenda nchini Lebanon Msemaji wa Vyombo vya Habari vya Vatican Dk. Matteo Bruni, amesema hiyo ni dhana inayochunguzwa. Alikuwa Rais wa Lebanon Michel Aoun ambaye alitoa habari, katika tweet, kuhusu ziara ijayo ya Papa Francisko katika Ardhi ya Mierezi. “Walebanon wamekuwa wakingojea ziara hii kwa muda ili kutoa shukurani zao kwa umakini wa Mwenyezi Mungu kwa Lebanon na kumshukuru kwa mipango aliyoifanya kwa ajili ya nchi na kwa maombi ambayo ameiomba kwa ajili ya amani na utulivu wake”, Alisema Rais Aoun katika ujumbe huo.

Hivi karibuni ulifanyika mkutano wa Papa Francisko na Rais Aoun

Hivi karibuni msemaji wa vyombo vya habari Vatican, alikuwa amethibitisha juu ya Papa Francisko kukutana na rais wa Lebanon Vatican mnamo tarehe 22 Machi iliyopita. Na mara baada ya mkutano huo Rais Aoun alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na na ushirikiano na Mataifa. Wakati wa mazungumzo ya kirafiki walielezea umuhimu wa uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Vatican na Lebanon, maadhimisho ya miaka 75 ambayo mwaka huu ni alama kubwa tangu kuanza kwake.

Papa Francisko alikutana hivi karibuni na Rais wa Lebanon.
Papa Francisko alikutana hivi karibuni na Rais wa Lebanon.

Katika mkutano huo pia walitazama  matatizo makubwa ya kijamii na kiuchumi ambayo Taifa linakabiliana nayo na hali ya wakimbizi, wakitumaini kwamba msaada wa jumuiya ya kimataifa, uchaguzi ujao wa sheria na mageuzi muhimu yanaweza kuchangia katika kuimarisha kuishi pamoja kwa amani kati ya maungamo mbalimbali ya kidini,  wanaoishi katika Nchi hiyo ya  mierezi. Hatimaye, kulikuwa na mazungumzo juu ya matokeo mabaya ya mlipuko katika bandari ya Beirut ya mnamo tarehe 4 Agosti 2020 na juu ya ombi la haki na ukweli lililotolewa na familia za waathirika.

Nia ya Francisko kwenda Lebanon

Papa Francisko amerudia mara kwa mara kuhusu nia yake ya kwenda Lebanon. Mwaka mmoja baada ya mlipuko katika bandari ya Beirut, mnamo tarehe 4 Agosti iliyopita, wakati wa Katekesi yake, Papa alikuwa ameelekeza mawazo yake kwa nchi nzima hasa kwa waathirika, familia zao na wale waliopoteza makazi na kazi zao. Na kuongeza: “Shauku yangu ya kuja kuwatembelea ni kubwa na sichoki kuwaombea ili Lebanon iweze tena kuwa ujumbe wa udugu, ujumbe wa amani kwa nchi za Mashariki ya Kati yote.” Pia mwaka jana, tarehe 1 Julai, Baba Mtakatifu aliomba siku ya sala na tafakari kwa ajili ya Lebanon kwa kuwakaribisha wazee na wakuu wa Makanisa ya Mashariki ya Lebanon jijini Vatican, pia mwaka jana, tarehe 8 Machi, Papa Francisko alifichua kwamba aliahidi, katika barua kwa Kadinali Bechara Raï, juu ya safari ya Lebanon.

Mapapa huko Lebanon

Papa Yohane Paulo II alitembelea Nchi ya Mierezi mwaka 1997 na Papa Mstaafu Benedikto XVI mwaka 2012; kwa Papa Ratzinger ilikuwa safari ya mwisho ya kitume ya upapa wake. Lakini lazima tukumbuke kusimama kwa sababu ya kiufundi kwa Papa Paulo VI mnamo 1964, ambaye alikuwa ni Papa wa kwanza kukanyaga ardhi ya Lebanon. Papa Paulo VI alisimama kwa saa moja huko Beirut, akielekea kwenye Kongamano la Ekaristi huko Bombay, nchini India. Akikaribishwa na Rais wa Jamhuri, Charles Hélou, na mamlaka kuu ya kisiasa na kidini ya nchi hiyo, Paul VI alitoa hotuba fupi kwa lugha ya Kifaransa. “Lebanon, tunafurahi kusema mahali hapa, inashikilia nafasi yake kwa heshima kati ya mataifa. Historia yake, utamaduni wake na tabia ya amani ya wakazi wake imepata, inaweza kusemwa, heshima ya jumla na urafiki. Historia zake za kidini za kale na zinazoheshimika, zaidi ya yote, zinaonekana kustahiki sifa zetu. Na hatuwezi kusahau, hasa yote ambayo imani ya Wakristo wa Lebanon inawakilisha kwa Kanisa, iliyooneshwa kwa wingi wa ibada, wingi wa jumuiya za kidini na za watawa, katika shughuli nyingi za kanisa, tabia ya kitume, kielimu, au kitamaduni” alisema Papa Paulo VI.

06 April 2022, 16:51