Umuhimu wa kuanzia moja, ujasiri na nguvu za Mattia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Historia iliyopendekezwa na Rai Tre kuanzia tarehe 7 Aprili jioni ni historia ya ujasiri na matumaini, historia ya Davide, mwalimu na mwanafunzi wa udaktari katika Takwimu za (Methodological) yaani mbinu za kidaktari katika Chuo Kikuu cha La Sapienza, Roma na mtoto wake Mattia, mwenye umri wa miaka mitano, mwenye ugonjwa wa moyo tangu kuzaliwa. Na matumaini hayo kwa Mattia yanawakilisha matumaini kwa watoto wengi waliolazwa katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù jijini Roma. Historia hii ya uchungu na ya ujasiri ilisimuliwa kwa usikivu na ukakamavy na mkurugenzi Alice Tomassini katika Dokumentari ambayo inafungua picha ya mikono ya baba anayekata nywele za mtoto wake, picha inayoonesha ukaribu na uaminifu, na ambayo hufunga kwa tabasamu ya Mattia ambaye anasema “Jibini!” huku Davide akimpiga picha.
Hisia na unyeti
Filamu inayojumuisha matukio ya karibu sana, ambayo hisia daima huwa kati ya muafaka, hasa katika tofauti kati ya ufahamu wa uchungu na wasiwasi wa ushuhuda wa wazazi, Davide na Stefania, na kutokuwa na hatia kwa Mattia kwa furaha na kutojua. Kwa mujibu wa maelezo ya mtayarishaji akisimulia histroia hiyo kwa utamu na heshima amethibitisha kuwa ilihitaji kutoroka mitego. Jambo kuu, anasema, lilikuwa ni kuchukua hatua kwa kupunguza, kuonesha maumivu lakini bila ya kuongeza.
Msaada wa akili ya bandia
Hatari kwa Mattia, na kwa watoto wengine wengi, inaitwa AKI, ambayo ni maambukizi makali ya figo ambayo kwa hila na ghafla huwapata watoto wengi wenye ugonjwa wa moyo kila mwaka. Inapotokea kujionesha mara nyingi inakuwa imeesha chelewa sana kuingilia kati. Davide Passaro, shukrani kwa mafunzo yake, alihisi kwamba, kwa kutumia Akili Bandia kwa data inayofuatiliwa kila siku juu ya wagonjwa wadogo katika uangalizi mkubwa (shinikizo la damu, joto, uchambuzi wa damu), inawezekana, kupitia utaratimu wa muda kutabiri mwanzo wa AKI na kwa njia hiyo kuokoa maisha ya watu wengi. Ni mfano wa furaha wa mazungumzo na mwingiliano mzuri kati ya taaluma tofauti, amesisitiza Davide Passaro, ambaye anakiri ugumu wa kuishi ubaba kwa kukabiliana na maumivu kama hayo.
Kamati ya maadili ya Hospitali ya watoto ya Bambino Gesù iliidhinisha mpango wa majaribio katika uhamasishaji, uliothibitishwa tena katika mkutano wa waandishi wa habari na Rais Mariella Enoc, wa kuwa na haja ya teknolojia na utafiti wa matibabu kuendelea pamoja, ili kuimarisha muungano huo muhimu kati ya familia na wafanyakazi wa matibabu ambao ndiyo wako kwenye msingi wa tiba. Kwa maama hiyo ni historia halisi ya ujasiri na matumaini, lakini kabla ya hayo ni historia ya upendo.
Siku ya Afya Duniani ni siku ya uhamasishaji ya afya duniani inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 7 Aprili yak ila mwaka, chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kuangazia maendeleo ya afya kwa watu wote. inasemakana kamba angalau robo tatu ya vifo vya ulimwengu kutokana na ugonjwa wa moyo na mishipa (CVD), au ugonjwa wa moyo, kutokea kwa chini- na kipato cha kati. Ugonjwa wa moyo unaweza kutibika na kuepukwa ikiwa utakamatwa mapema. Sababu moja inayoathiri watu masikini zaidi katika maeneo haya ni ukosefu wa kugunduliwa. Hata hivyo tathmini ya ugonjwa wa moyo katika nchi zinazoendelea ingekuwa ya msingi kabisa, bora. Utaweza kupata elektroni katika kliniki nyingi lakini kumbuka, katika mataifa masikini na yanayoendelea, kiwango cha utoaji wa huduma ya afya mara nyingi ni ada ya huduma. Ikiwa mtu ana shida kali ya kiafya, watajitokeza kwa idara ya dharura, mara nyingi hufuatana na familia zao, watazungumza na daktari na mgonjwa. Kwa kuzingatia hilo, uchaguzi wa tathmini ya utambuzi unaweza kuwa mdogo katika maeneo mengine.