Papa awathibitisha Czerny na Smerilli kuwa wakuu wa Baraza la Maendeleo Fungamani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 23 Aprili amemteua Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Kardinali Michael Czerny, S.I., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa tayari ni mwenyekiti wa muda wa Baraza hilo. Na akamteua Katibu wake Sr. Alessandra Smerilli, F.M.A. ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni katibu wa muda wa Baraza hilo. Baba Mtakatifu Francisko pia amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza hilo hilo kwa ajili ya Uwajibikaji wa Kitengo cha Wakimbizi na Wahamiaji na Mipango Maalumu, Padre Fabio Baggio, C.S., na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa katibu katika kitengo hicho hicho cha Baraza la kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu.
Shukrani kwa Papa kwa utume aliowapatia
Katika kumshukuru Papa kwa imani aliyowapatia, viongozi hao wapya wamethibitisha katika tamko la pamoja juu ya upeo ambao hatua yao itaendelezwa hasa katika maendeleo fungamani ya kila mtu na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. Pia wameahidi kujitoa kutekeleza pamoja na mambo mengine , yale mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Tathmini iliyoundwa na Baba Mtakatifu katikati ya 2021 inayoongozwa na Kadinali Blase Cupich. Kwamaneno yao wamehitimishwa kwa kumpongeza mtangulizi mkuu wa Baraza hilo, Kardinali Peter K.A. Turkson, aliyeitwa sasa na Baba Mtakatifu kulitumikia Kanisa katika nafasi yake mpya kama Kansela wa Vyuo vya Kipapa vya Sayansi na Sayansi ya Jamii.
Uharaka wa kukuza hisia za kichungaji sambamba na Baraza hilo
Papa ni mfano wa Msamaria Mwema ambaye ni dhahiri kama dira ya uinjilishaji, unaofanya kwa wengine kama Yesu alivyofanya kwamba kuthibitishwa ni ishara ya upya kama ambavyo Kardinali Michael Czerny amesisitiza na kuahidi kutimiza katika Baraza zima. Kwa mujibu wake amesema uharaka uliopo ni ule wa kukuza hisia za kichungaji sambamba na jina lenyewe la Baraza la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu na lazima yachunguzwe kwa kina katika nyanja zake zote.
Kusikiliza na kutumia Makanisa mahalia
Na kwa mujibu wa Sr. Alessandra Smerilli, amesema "Anachotupatia Papa ni fursa ya kutumikia na kusikiliza Makanisa mahalia na kuwahudumia wale wanaouguza majeraha yao kila siku, kuwasiliana na wale wanaohitaji zaidi ambapo maendeleo fungamani ya binadamu hayaonekani sana, na wapo badala wanatupwa". Kuwa Roma, amesisitiza mtawa wa Kisalesiani, ambaye kwa namna fulani yuko katika kituo chake anatoa uwezekano wa kuweka pamoja, wa kuunganisha na kuweza kuleta sauti ya wasio na sauti, ambapo labda hawangesikika bila upatanishi wao.