Sauti za vilio kufika kwa Papa ili kuokoa watu huko Mariupol
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mtego ni mauti na kwa sababu hiyo kilio cha kuomba msaada kinajaribu kupaa zaidi juu iwezekanavyo ya makombora. Sauti hiyo ambayo imefikia hata Papa ni kama ngome ya mwisho ya matumaini. Utafikiri ni kama kusikia kishindo cha silaha zikipiga bila kuzuilika nyuma ya maneno ya wito huo mrefu wa heshima lakini pia wa kukata tamaa ulioelekezwa kwa Papa Francisko kutoka kwa wamama, wake, watoto mbapo ni kama watetezi wa Mariupol, ambayo ndiyo walio tia saini na imefika Vatican katika mikono ya Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Hayo yamewezekana katika mahojiano na Vatican News. Kwa wa Kardinali Czerny amesisitiza jinsi ambavyo barua iliyoandikwa imeelekezwa kwa Baba Mtakatifu inavyotoa ushahidi wa kile alichosema tangu mwanzo, hasa wakati wa ujumbe wa Pasaka wa Urbi et Orbi, alipozungumzia waziwazi kutokuwa na mantiki vita kamili.
Aliyewasilisha barua kwa Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu alikuwa mwandishi wa habari Saken Aymurzaev, wa televisheni ya serikali ya Ukraine (UATV-channel). Kurasa mbili ambazo ni sehemu ya kile ambacho habari zimekuwa zikieleza kwa wiki nyingi sana kuhusu uchungu wa mauaji ya kinyama katika jiji la vita nchini Ukraine. Mji ambao sasa umegeuzwa kuwa majivu, unaoshambuliwa kwa masaa 24 kwa siku na ambao ni kitovu cha janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea katika karne ya 21 barani Ulaya na ambapo kwa hakika litatokea kwa mara nyingine tena suala la kutokubalika hasa kuzingirwa kwa miji hiyo pamoja na seti yake ya mashambulizi ya kiholela kwa raia, uharibifu usio na msingi,na mateso yasiyoelezeka kwa wale ambao badala yake wanalinda sheria za kimataifa za kibinadamu.
Kwa mujibu wa msemaji wa Papa, bado inawezekana kusaidia mateso, licha ya idadi ya wale ambao hawataki kisikia kila siku na ndiyo wito wa Papa. Kwa wanawake na watoto wa wale ambao bado wanalinda Mariupol, ikiwa ni pamoja na wanawake mia moja waliovaa mavazi ya kijeshi, wengi wao wakiwa madaktari na wapishi, wanafanya ijulikane juu ya uwepo wa mamia ya raia na askari waliojeruhiwa, bila tiba yoyote ya dawa na hivyo lazima waondolewe kwenye uwanja wa vita. Kurasa za barua hiyo zinaelezea hali ya Azovstal, kiwanda cha chuma ambacho kimekuwa mbele ya vita vya maamuzi, ambayo, pamoja na jeshi la Kiukreine, bado kuna raia elfu. Mwanzoni mwa mapigano watu hawa walidhani kwamba kuishi na jeshi kungewapa sio usalama tu, bali pia fursa ya kupata chakula, maji na huduma za matibabu. Badala yake, kwa wanawake wengi na watoto kile kilichoonekana kama ngome sasa kimekuwa mtego, usioweza kufikiwa hata kwa kupeleka chakula na maji ya kunywa.
Ombi hili linaloonesha hata kukata tamaa kwa mujibu wa Kardinali Czerny pia linaelekezwa kwa wale wote ambao wana fursa ya kusaidia katika mikondo ya kibinadamu na usitishaji wa mapigano, ambayo ndiyo hasa hali inahitaji kwa wakati huu. "Wakati ambao, ni pamoja na imani na furaha ya Ufufuko lazima tuweze kufariji mateso na uchungu wa kaka na dada zetu wa Ukraine na pia wa maeneo mengine mengi duniani ambako kuna hali kama hiyo ya kutokuwa na mantiki mbaya ya vita". Wanawake, watoto na waliojeruhiwa hawastahili kifo kama hicho machoni pa ulimwengu ni wapiganaji wa siku hizi, inahitimisha barua ya kilio kwa Papa Francisko. “Msaada wake katika uokoaji wao kutoka Mariupol utakuwa tendo la kweli la baba, msaada wa mchungaji mzuri na tendo la kweli la huruma”.