Kard.Krajewski anapeleka gari ya pili ya wagonjwa Ukraine
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika safari ya kurudi kutoka Malta, Papa Francisko alikuwa amezungumza juu ya gari la pili ambalo mtoa msimamizi wa sadaka ya Papa angeipeleka nchini Ukraine. Dominika gari hilo limepangwa kuondoka, likiwa limebarikiwa pia na Papa mwenyewe, litakuwa likiendeshwa na Kardinali Krajewski na likiwa na vifaa vya kisasa vya matibabu hata kwa ajili ya watoto wadogo ambavyo vimetolewa na Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu. Gari hilo linapelekwa Kiev, mji unaoteswa na vita, lakini ambao haujaachwa na Kanisa na Papa ambaye kupitia kwa Balozi wa Vatican Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, anaendelea kusimama pamoja na wale wanaoteseka, wanaoomboleza wapendwa wao, wanaoishi katika hali ngumu ya maisha, kukaa au kuondoka milele. Kwa maana hiyo unaweza kurudishwa kwenye maneno ya Papa Fransisko, wakati wa kuwaosha miguu siku ya Alhamisi Kuu 2014, alipoinama juu ya watu kumi na wawili walemavu katika kituo cha Padre Gnocchi. Hii ni kutokana na kwamba unapofikia juu ya utume mpya wa Kardinali Konrad Krajewski, kuungwa mkono na kutamaniwa na Papa mwenyewe.
Gari la wagonjwa ni kwa ajili ya uponyaji, na hivyo siku ya Alhamisi Kuu itakuwa kama kubembeleza miguu, kuosha na kuifunga kwa kitambaa safi, ni ukaribu, huduma na kwa hiyo upendo juu ya yote kwa watu walioitwa katika mtihani huu mgumu. Wakati mtu aliyejeruhiwa, mgonjwa au mwenye matatizo anapopelekwa kwenye gari la wagonjwa, Kardinali Krajewski anasema, atahisi kukumbatiwa na kufarijiwa na Papa, ambaye anataka kuosha na kumbusu miguu ya ndugu hao wanaoteseka kwa ghasia zisizo za haki za vita. Msimamizi wa Sadaka ya kutme kwa Juma zima Kuu Takatifu katika taifa hilo, atakutana na watu na kuadhimisha siku sikuu kuu Tatu takatifu na jumuiya za Kikristo. Ishara ambayo ni mwaliko kwa Kanisa zima kuingia katika Juma Kuu Takatifu na mitazamo kwa Kristo wa unyenyekevu na mapendo, kufikia Pasaka ya Ufufuko wa iliyofanywa upya kikamilifu katika Roho hata ikiwa karibu na kelele za vita inayoendelea kusababisha hofu.
Tukiyasoma leo tunatambua jinsi maneno ya Papa yalivyo ya kinabii na ya kufariji aòiyosema wakati wa mkesha wa Pasaka 2021, wakati ulimwengu uligubikwa na janga hili: “Dada, kaka, ikiwa usiku huu umebeba saa ya giza moyoni mwako, siku ambayo bado haijapambazuka, nuru iliyozikwa, ndoto iliyovunjika, nenda, fungua moyo wako kwa mshangao wa tangazo la Pasaka: “Usiwe na huzuni, hofu, imefufuka! Anawangoja ninyi huko Galilaya”. Matarajio yako hayatabaki bila kukamilika, machozi yako yatakauka, hofu yako itashindwa na matumaini. Kwa sababu, unajua, Bwana daima utangulia mbele yako, daima hutembea mbele yako. Na, pamoja naye, maisha huanza tena".