Kard.Czerny:ukatoliki umo ndani ya moyo wa mwanadamu na ukamilifu wake wa nguvu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika kukuzungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Shule yaKimataifa ya biashara ya Norman Paterson, Chuo Kikuu cha Carleton, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Mikaeli na Chuo Kikuu cha Toronto, Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu amehutubia juu ya Mchango wa Ukatoliki kwa ajili ya maendeleo endelevu ya ulimwengu wote. Katika hotuba hiyo amesisitizia kuhusu Waraka wa Papa Francisko wa Laudato si unaohusu utunzaji bora wa mazingra na nyumba yetu ya pamoja na Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii. Kwa kutazama hasa matukio ya sasa, ya uvamiwa Ukraine kwa upande wa Urussi na katika vita vingine vya umwagaji damu katika sayari vinavyoendelea, awali ya yote amebainisha jinsi gani ilivyo ngumu leo hii, kuwa ndugu katika nyumba yetu ya pamoja.
Kardinali Czerny alikumbuka kwa upande huo hata unyeti wa mchakato wa safari ya Kanisa ambavyo inaendelea kuwa karibu na watu wa Asilia wa Canada mara baada ya ugunduzi wa janga baya na jinsi gani Papa Francisko alikutana nao na kuleza juu ya kuondolewa mizizi ya watu wengi na familia nyingi katika ardhi za ona tamadunu za ona na nyanyasi ambazo zimeweka madoa kwa wakatoliki mbali mbali kwa namna yua pekee wahusika wa kielimu. Kwa mujibu wa Kardinali Czerny amefafanua kwamba ukatoliki upo ndani ya moyo wa mwanadamu na ukamilifu wake wenye nguvu, na kwa maana hiyo yeye anatafua kuchambua hata vizingiti ambavyo vinazuia maendeleo fungamani ya binadamu. Kwa njia hiyo Kardinali amebainisha kuwa Tamko la Haki za mwanadamu zilizotangazwa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa mnamo 1948 ni moja ya kilelelezo cha juu zaidi cha utambuzi wa hadhi ya binadamu. Na hiyo ni dira ajibishi kwa ajili ya demokrasi.
Pamoja na hayo lakini ameelezea kuwa mauaji yaliyofanyika dhini ya hadi ya binadamu na ambayo leo hii bado yao kama vile mauaji, mateso ya kimwili, adhabu ya kifo, ugaidi, ubaguzi wa rangi, ubaguzi mdhidi ya wanawake, hairuhusu kuzungumza usawa wa haki watu wote. Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendelo fungamani ya Binadamu, ameweka usahii kwamba kutoka katika Waraka wa Fratelli Tutti inaeleweka kwamba kuwa Ndugu kunatokana na mshikamana uliokita mzizi kutokana na utambuzi wa usawa msingi wa wanaume, wanawake, vijana na wazee bila upendeleo, Na hiyo inahitaji kuelimishwa,na kuta na utambuzi wa mwingine kama jirani mwenye mahitji sana na mwingine.Akirejelea tena Juu ya Waraka wa Fratelli tutti yaani Wote ni Ndugu Kardinali Czerny alisisitiza kwamba ubinafsi haufanyi mtu kuwa huru zaidi, sawa zaidi, kuwa na udugu zaidi na kwamba ikiwa haitatambulika kwamba kila mwanadamu ana haki msingi na isiyoweza kuondolewa kwa maendeleo yake binafsi, hakuna hata wakati ujao si kwa udugu wala kwa ajili ya kuendelea kwa ubinadamu utakuwapo. Kardinali pia ameongeza kusema ni muhimu kuzingatia mada mbili muhimu za mafundisho jamii ya Kanisa ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameendeleza katika waraka wa Fratelli tutti katika kanuni ya mshikamano na nafasi ya mali katika jamii. Kardinali alisisitiza kwamba familia, shule, parokia, vituo vya kitamaduni na burudani lazima vikuze udugu na kusambaza tunu za uhuru, kuheshimiana, kushirikiana na kujumuika, pamoja kwamba vizazi vipya lazima vielimishwe na kuunda kujua mshikamano wa ulimwengu wote na kwamba ubaguzi na tabia za utamaduni wa kutupa ni kinyume.
Ikiwa kigezo cha upendo kinachovuka mipaka ya ubinafsi kinatumika kwa haki ya mali ya kibinafsi na haki nyingine zinazohusiana, hii itakuwa na athari kwa utendaji wa kila kanda na kwa uhusiano wa kimataifa kati yao. Baadaye Kardinali Czerny akasisitiza kwamba, kila taifa linawajibika kwa ajili ya maendeleo ya nchi nyingine na kuhamasisha maendeleo shirikishi ya watu, hata nje ya mipaka yake. Na pia alirudia kutoa mwaliko wa Papa Francisko kwa nchi zilizo na uchumi wa juu kusaidia, badala ya kutawala, nchi zilizoendelea kidogo, kwa wito wa dhati wa mshikamano ili kila mtu apate kile kinachohitajika kuishi kwa heshima. Hatimaye, kadinali alihitimisha hotuba yake kwa kusema kwamba kutambua matatizo ya ulimwenguni ya leo hii kulingana na kigezo cha upendo kunamaanisha mchakato wa kuchochea na kusindikiza si kulazimisha mbinu fulani. Kwa hivyo kutia moyo kubadili mtazamo na kujitazama kama ndugu, kwa kuushinda ubinafsi.