Maandalizi ya Jubilei 2025 Maandalizi ya Jubilei 2025 

Jubilei 2025:muhimu mkuu wa maandalizi jijini Vatican ya Jubilei

Tarehe 4 Aprili umefanyika mkutano wa Tume ya kichungaji kwa ajili ya maandalizi ya mwaka wa Jubilei 2025.Katika mkutano huo wamejikita kutazama juu ya umuhimu wa kiroho na matukio mengine kwa maelekezo ya Papa.Hivi karibuni lilizindulwa shindano la kimataifa kwa ajili ya kuandaa Nembo ya Jubilei 2025.Kwa sasa zimeanza kazi nyingi za wasanii kwa ajili ya Nembo hiyo,wa kwanza ni kutoka bara la Afrika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Safari yenye utajiri mkubwa ambao Makanisa yote yaliyoko ulimwengu mzima yanaweza kufanya pamoja. Ndiyo kipaumbele cha Jubilei ya 2025 kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Uinjilishaji Mpya,  Baraza la Vatican ambalo limepewa jukumu na Papa Francisko kuandaa tukio hilo. Katika mahojiano na Telepace, Askofu Mkuu Fischella amesema kuwa maelekezo ni yale ya kuepuka tukio lisiwe kama uzoefu wa kitu ambacho kinatokea kila baada ya miaka 25 tu bali kuwa hai kabisa.

Askofu Mkuu Fisichella akielezea kuhusu maandalizi ya Jubilei 2025

Katika mkutano ambao umefanyika tarehe 4 Aprili 2022,  wa Tume ya kichungaji kwa ushiriki wa wawakilishi kutoka Mabaraza ya Sekratarieti Kuu (Curia Romana’), Baraza la Maaskofu Italia na mashirika mengine ya kikanisa, Askofu Mkuu ameeleza kuwa wataanza kuona jinsi gani ya kuunda muhimili wa Jubilei hiyo kwa mtazamo, si tu wa kiroho, lakini pia hata kuwa na muhimili mkuu wa matukio kulingana na maelekezo yaliyomo kwenye barua ya Papa Francisko aliyomwelekeza yeye hivi karibuni.

Katika siku sijazo kuna ratiba ya mkutano wa Tume ya kiutamaduni ambayo lengo lake ni ulewa wa namna ya kuweka pamoja uzoefu wa kiroho na ule wa kiutamaduni. Upeo inatokana na uzoefui uliopita wa Jubilei mbali mbali ambazo zimewaweza kuonesha uhusiano wa nguvu kati ya ukuu wa hija na utalii. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Fisichella amesemakatika historia ya hija, ya watu daima wamejionesha kuwa na udadisi wa kutaka kujua na kuelewa utamaduni mahalia, kwa kurudi kwao wakiwa na utajiri usioelezeka. Maelekezo yenye thamani kutoka katika chombo kikuu cha maandalizi cha Vatican ambacho kiukweli kina muundo thabiti. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Fisichella amebainisha kuwa muundo huo unajikita kwa:  Kamati ya kiufundi, Tume ya kiekumene na Tume kwa ajili ya mawasiliano. Hizi tume zitakutana pamoja muda si mrefu. Hata mshikamano na vyombo vya habari ni msingi mkuu kwa mu jibu wa Askofu Mkuu. Katika meza kuna ulazima wa kuweka wazi, si jinsi gani ya kusambaza vipindi hivyo lakini hasa ni mitindo gani ya sasa kwa ajili ya kuwahusisha mahujaji wengi.

Nembo ya Jubilei

Hatimaye Askofu Mkuu Fisichella amethibitisha kuwa Nembo ya Jubilei itajulikana kwa namna moja au nyingine mwishoni mwa mwezi Mei.  Tarehe 20 Mei kiukweli ndiyosiku ya mwisho ya mashindano hayo ya kimataifa yaliyozinduliwa hivi karibuni mwezi Februari mwaka huu, ili kuweza kukusanya michoro mbali mbali kutoka kwa watu inayohusiana na tukio hilo kwa kuongozw na kauli mbiu ya ya Jubilei.  Kwa sasa tayari imeanza kufika michoro mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu. Na kazi za kwanza  kwa mujibu wa Askofu Mkuu Askofu Mkuu Fischella, zimefika kutoka bara la Afrika, na  hivyo amesisitiza kuwa hiyo ni ishara hai kabisa ya kuona kujihusiana kutoka katika bara hilo. 

Shindano la Kimataifa la kuchora Nembo ya Jubilei 2025
MAANDALIZI YA JUBILEI YA 2025 NA SHINDANO LA NEMBO KIMATAIFA
05 April 2022, 11:28