Tafuta

Upinzani wa mama wa Urusi na uvumilivu wa watu wa Ukraine. Upinzani wa mama wa Urusi na uvumilivu wa watu wa Ukraine. 

Upinzani wa mama wa Urusi na uvumilivu wa watu wa Ukraine

Nchini Ukraine vijana sana wa Urusi wametumwa kujifunza kupambamba bila kujua kuwa hiyo ni operesheni ya kivita.Mama zao wanapinga kwa sauti kubwa kwa sababu hawana habari za watoto wao.Wakati huo huo,watu wa Kiukreni wanajaribu kumpinga mvamizi:mapambano yasiyo sawa ya kutetea uhuru.

Sergio Centofanti

Huko Urusi kuna akina mama wajasiri ambao hawaogopi kuandamana kwa sababu watoto wao wametumwa kuivamia Ukraine bila hata kujua. Wengine ni askari wasio na ujuzi na umri mdogo, askari watoto ambao hawataki kupigana vita vya wengine. Wapo akina mama wanaoweza kukubaliana na sababu za vita hivyo, kwa sababu kuna propaganda na taarifa za upotoshaji, lakini ukiwa na mtoto aliyedanganywa, akatumiwa na kupelekwa mbele kuua na kufa badala ya kuishi na kuacha kuishi, basi uasi unakuwa na nguvu zaidi kuliko hofu yoyote. Haijalishi ikiwa sasa kuna sheria inayohukumu hadi miaka 15 jela ikiwa mtu anazungumza juu ya uvamizi. Ikiwa mama wanaasi, serikali lazima iwe na wasiwasi.

Kuna mama wa Urusi ambao wametelemka kwenye viwanja kuandamana, wamepigwa na kukamatwa. Mtoto kwa upande wa mama ni kila kitu. Wanataka kujua mahali walipo vijana wao waliotumwa kwenda kukabiliana na mauaji na ambao hawana tena habari yoyote kwa sababu mamlaka hawajali lolote kuwapa taarifa. Wapo akina mama wa kirusi walioingia barabarani kuandamana, wakapigwa na kukamatwa. 

Kuna mama wanaotarajia, kwa sababu mtoto aliyetekwa wa Waukraine aliweza kupiga simu, akilia. Bado yuko hai. Kuna watoto wengine askari ambao wanatoroka na kukimbia. Hawaelewi kwanini wafe kwa ajili ya vita hivyo. Kinyume na haya kuna upinzani wa ujasiri wa watu huru, Waukreni, ambao hawataki kuwa watumwa na utawala wa kigeni. Kwa wale wanaoamini au wanaotaka kuamini uwongo kwamba jeshi la Urusi lilikwenda kuwakomboa watu mikononi mwa Wanazi, inatosha kuona ni Waukraine wangapi kutoka ulimwenguni kote wanaacha upendo, mali, utajiri na faraja na kurudi kwao, nchi yao ili kuilinda dhidi ya mvamizi.

Inatosha kutazama ni wazee wangapi, wanawake na raia wa Kiukreni wasio na silaha wanaomiminika kwenye mitaa inayokaliwa na mizinga iliyotumwa kutoka Moscow wakipiga kelele ili warudi nyuma. Zimetolewa shuhuda za wazi kutokwa ambazo kabla yake histroai zinazotoa masimulizi kinyume na ambayo huonekana kuwa uwongo wao wote. Hapa kuna watu, wa Ukraine, ambao wanataka kuwa huru kuamua maisha yao ya baadaye na watapinga hadi mwisho. Ndio maana jeshi la Urusi linawachoma moto raia kwa silaha na kuwaua kwa njaa, na kuharibu kila kitu, kupiga nyumba, hospitali, shule, makanisa: kwa sababu Moscow inajua inaweza kushinda vita lakini sio vita dhidi ya watu wanaotaka uhuru.

14 March 2022, 14:28