Tusiwaache waukraine!
Sergio Centofanti
Watu wengi wa Ukraine wamejisikia kutelekezwa katika siku hizi za janga. Hawataki kusikia masuala kuhusu “bei ya gesi” kwa sababu wanahisi kuuzwa. Wanajua kwamba uingiliaji kati kutoka nje unaweza kuzua mzozo mkubwa zaidi, unaoweza kuharibu ulimwengu. Rais wa Belarus Lukashenko alisema hata vikwazo vinaweza kumsukuma Putin katika vita vya nyuklia. Tukio ambalo hatutaki hata kulifikiria.
Lakini mbele ya mashambulizi ya Urusi na vitisho vya kijinamizi, mshikamano unazidi kuongezeka zaidi na zaidi. Uvamizi wa nchi huru umeunganisha Ulaya kuliko hapo awali. Ulaya, iliyogawanyika sana katika masuala mengi, haijawahi kuwa na umoja kama leo hii kusimama pamoja na watu wa Ukraine. Nchi jirani zimefungua mipaka yao kwa ajili ya wakimbizi. Poland, Hungaria, Romania, Slovakia, wamefungua mikono yao. Nchi nyingine ziko tayari kuwakaribisha walio uhamishoni. Maandamano na mipango ya amani na mshikamano na Ukraine inaendelea barani Ulaya na katika mabara mengine.
Jumuiya za Kikristo, parokia mbali mbali, vyama, Caritas, wamejipanga kutafuta na kupata misaada ya kibinadamu kwa njia zote. Rais Zelenskyi alisema kuwa watu wa Ukraine wanahisi uungwaji mkono wa Papa. Katika sala ya Malaika wa Bwana hivyo karibuni, Papa Fransisko alirudia kutoa wito wake wa kunyamazisha silaha, na alisema kwamba: “Mungu yuko upande wa wapatanishi wa amani, sio na wale wanaotumia vurugu: Na hao ni watu wa kawaida wanataka amani”. Kuna mshikamano mkubwa mbele ya picha za watoto, wanawake, wazee, wanaokimbia kwa miguu au wamefungiwa kwenye makazi ili kusali wakiwa na nyuso za huzuni au karibu na walikufa. Kwa sasa ni matumaini katika mazungumzo.
Kuna uwepo wa ukaribu mwingi kwa watu wa Ukraine. Watu wanaotaka amani na wameteseka sana. Katika miaka ya 1930, Stalin aliwafanya wawe na njaa kwa sababu walipinga sera za Kisovietiki: Watu kadhaa wa Ukraine kama milioni walikufa kwa sababu ya njaa. Ni maangamizi kidogo yanayojulikana, kama Holomodor, yalikuwa ni maangamizi ya watu kwa njaa. Warusi walio wengi wanaona aibu kwa uvamizi huo. Vyombo vya habari vinavyounga mkono serikali vinaiita “operesheni ya kijeshi” au “denazificatio”,yaani (Denazification ilikuwa mpango wa washirika uliolenga kuikomboa jamii, utamaduni, vyombo vya habari, uchumi, haki na siasa za Austria na Ujerumani kutoka katika mabaki yote ya itikadi ya Kitaifa). Kuna Warusi wengi wanaoamini. Lakini Warusi walio wengi wanaandamana kwa ajili ya amani dhidi ya shambulio hilo. Wengi wamesimamishwa. Tunawaunga mkono Warusi wanaopenda amani. Tunaunga mkono askari wa Urusi ambao hawataki kuwapiga risasi Waukraine, labda kwa mikono yao iyo wazi mbele ya mizinga. Hebu tuwasaidie Warusi wanaoamini katika vita hivi kuelewa uovu ulipo. Zaidi ya yote, tusiwaache watu wa Ukraine.