Tafuta

Wakimbizi nchini Ukraine Wakimbizi nchini Ukraine  Tahariri

Ukraine:wanawake mfano wa tumaini,nguvu na upendo

Siku ya Kimataifa ya wanawake 2022 imejikita ndani ya vita nchini Ukraine,mahali ambapo maelfu ya wanawake wanalazimika kukimbia.

Massimiliano Menichetti

Katika siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka huu haiwezi kukosa kutazama kwa umakini juu ya ujasiri, nguvu, na majaribu ambayo wanavumiliwa nchini Ukraine, ambapo wanawake wanalazimika kuacha nyumba zao ili kulinda watoto wao. Wanawake wanaosali. Wanawake wanaoamua kubaki karibu na waume zao kupinga mizinga inayosonga mbele na roketi zinazolipuka. Wanawake wanaonyonyesha kwenye vifusi na chini ya moto, wanawake wanaosaidia, kuandaa chakula, wanaojifungua maisha, matumaini mapya, wakisubiri kwa masaa kwenye mipaka. Wanawake wanaoendesha magari na malori, kwa sababu taifa linashambuliwa. Wanawake wakiandamana na vitu vichache vilivyokusanywa, kati ya baridi na theluji.

Wanawake wanaopoteza maisha, wanaobakwa, wasichana wanaopigwa na mabomu na risasi. Ni nani anayeweza kukubali hofu hii yote? Nje ya Ukraine, wengine wanakusanya misaada, wanafanya kazi katika siasa, katika diplomasia ili kutafuta suluhisho, kuna maandamano mitaani, wengine wanakamatwa na kupigwa. Wanawake: mabinti, dada, mama, wake, marafiki, kwa ajili ya kujenga jamii, kusaidia uchumi, kuleta elimu na ubunifu, kulinda uumbaji, kulinda ubinadamu. Wanawake waliofungwa. “Kuumiza mwanamke ni kumkasirisha Mungu”, Papa alisema mnamo Januari Mosi mwaka huu, wakati vivuli vya vita huko Ulaya vilikuwa havijaonekana, lakini wanasonga mbele kimya, kama ilivyo mara nyingi nynyaso, dhuluma dhidi ya wanawake ulimwenguni.

Waathirika, mara nyingi sana wako katika ukimya, wa ukatili wa kisaikolojia na kimwili, wasichana waliolazimishwa kuolewa katika ndoa za kupangwa, kulazimishwa kufanya ukahaba, kufanya kazi za suruba, kutopata, kuuawa na wanaoona watoto wao wakifa vitani. Nani anaweza kunyamaza kwa machukizo kama haya? Wanawake katika ukawaida, msaada na mwongozo, mashujaa, hata kama ukawaida umeharibika. Wanawake ambao katika kila sehemu ya dunia wanapinga mantiki ya utengano na uadui, wanaofanya kazi kwa umoja. Katika historia ya Kanisa kuna Watakatifu wengi, vinara ambao wameleta nuru ya wokovu ya Kristo wakati wao na leo hii katika Ulaya iliyojeruhiwa na dhuluma na vitisho. Wasimamizi, walinzi wa bara hili kama vile: Mtakatifu Brigida, Hildegard wa Bingen, Teresa Benedetta wa Msalaba na Catherine wa Siena. Katika masaa haya yote ni kumkabidhi Maria, Mama wa Mungu, ili vurugu zote nchini Ukraine na duniani zikome na kila mwanamume na mwanamke waishi kwa amani.

SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE 2022
08 March 2022, 14:40