Ukraine,Kard.Parolin:Utayari wa kuingilia kati upo kwa ngazi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, katika mahojiano na Tv2000, ambayo ni televisheni ya Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) amesisitiza kuwa “Ikiwa hatua yetu inaweza kusaidia sisi tupo pale”. Katibu wa Vatican amebainisha kwamba jambo la kwanza la kufanya ni kusimamisha silaha, yaani kusitisha mapigano, lakini juu ya yote kuepuka hata mwendelezo. Njia ya kwanza kwa mujibu wa Kardinali Parolin ya kuanja ni ya maneno ya uchochezi hasa. “Tunapoanza kutumia maneno fulani, misemo fulani, hayo hayafanyi chochote zaudi ya kuchochea akili na kusababisha karibu, ningesema, kwa kawaida, kwa kutumia matumizi ya njia nyingine kabisa, ambazo ni silaha za mauti ambazo tunaziona katika matendo ya wakati huu huko Ukraine”.
Katika mahojiano hayo Kardinali Parolin anakumbuka kwamba kuingilia kati kwa Vatican kunafanyika katika ngazi kadhaa, kuanzia na ile ya kidini na mwaliko wa sala ya kusisitiza kwamba Bwana atoe amani katika nchi hiyo inayoteswa na kuhusisha waamini katika sala hiyo ya kwaya. Halafu baadaye kuna uingiliaji wa kibinadamu, kupitia Caritas na majimbo yanayojibidisha na kujitolea kuwakaribisha wakimbizi kutoka Ukraine, na kama ilivyo taasisi nyingine nyingi. Hatimaye, kuna uwezekano wa mipango ya kidiplomasia. Tayari kuna majaribio kadhaa ameeleza ambayo yanafanyika ulimwenguni kote na kwa hivyo wako na uwezekano ikiwa inaaminika kuwa uwepo wa Vatican na hatua zao zinaweza kusaidia, wapo pale.