Ufunguzi wa Kituo cha Tiba Shufaa cha Bambino Gesù
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Hali nzuri inayovuma kutoka katika bahari imetoa kama kitulizo la moyo ulioelemewa. Kituo cha Tiba shfaa, cha watoto wa Hopitali ya Kipapa ya Bambino Gesù, kimezinduliwa huko Passoscuro, katika kata ya Fiumicino Roma. Katika Uzinduzi huo alikuwapo Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican ambaye wakati wa kutoa hotuba yake alisema "Sio mahali pa uchungu, ni mahali pa kukarimu, pa mkubamtio wa huruma". Jengo hili lilifikiriwa kwa ajili ya kuwasindikiza watoto, kwa kile ambacho kinaitwa magonjwa yasiyo na tuba lakini pia kwa ajili ya mahitaji ya uangalizi na utunzaji. Ni tiba ambayo haindolewi hata kwa wagonjwa watoto, lakini inawatazma familia nzima ambayo inaishi ugonjwa huo kwa watoto wao.
Kituo hicho kina ghorofa 5 kuzungukwa na kijani na hatua chache kutoka baharini, kwa sasa kuna watoto 5 wa Kiukreni wenye magonjwa hatari sana kati ya watoto zaidi ya 60 wanaotunzwa na Hospitali ya Bambino Yesu tangu mwanzo wa vita. Rangi ya machungwa inatawala, juu ya kuta za vyumba, zilizo na jiko dogo, bafu iliyo na vifaa, sofa au kitanda cha sofa, kuna misemo ya Mfalme mdogo, na hadithi ya Antoine de Saint-Exupéry ambayo watoto hawaachi kamwe kupenda. “Kila wakati ninatazama nyota, inasoma picha ya bluu, inakumbuka matamanio yote ninayoweka moyoni mwangu”.
Maneno ambayo husaidia kupumua katika hali ya maumivu makubwa, husaidia mama, baba, ndugu ambao wana nafasi hapo ya kucheza katika uwanja wa mpira wa miguu, mpira wa kikapu na mpira wa wavu, kutembea kwenye bustani iliyohifadhiwa vizuri. Miundo 20 ya makazi ambayo tayari imekamilishwa, 10 katika iko katika maandalizi, watoto thelathini ambao wanaweza kuwa wageni: idadi muhimu sana ikiwa utazingatia kuwa nchini Italia kuna hospitali 7 za watoto ambao hupokea jumla ya 25. Kardinali Pietro Parolin alipeleka shukrani za Fransisko, akikumbuka kwamba Kanisa linasisitiza sana juu ya huduma shufaa na inatoa ishara thabiti kama vile muundo wa Passoscuro. "Ni kazi ya ya ulinzi ambayo inatoa maeneo mengi yanayopatikana na mazingira ya familia, mtu hajisikii hospitalini. Aina hii ya ugonjwa haipaswi kutenganisha bali kuunda vifungo vikubwa vya mshikamano na ukaribu ” alihitimisha.