Wakimbizi wa Ukraine huko Hungaria Wakimbizi wa Ukraine huko Hungaria  

Ukraine:Kard.Czerny kwenda katikati ya wakimbizi huko Hungeria na mipakani

Mwenyekiti wa Muda wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu tarehe 8 Machi atakwenda kwa niaba ya Papa huko Budapest na miji mingine mahali ambapo atatembelea vituo vya wakimbizi kutoka Ukraine na hali halisi iliyopo hasa umakini na wasiwasi wa matatizo ya biashara haramu ya binadamu na majanga halisi ya sasa katika mipaka ya nchi.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Vatican imejiweka katika huduma kwa ajili ya kufikia amani nchini Ukraine. Kwa ishara hiyo maalum, Papa aliitangaza wakati wa sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, Dominika tarehe 6 Machi  2022 kwamba anawatumwa Makardinali wawili kama kielelezo cha mshikamano wa Kanisa kuelekea watu wa Ukaine wanaoteseka. Hawa ni Kardinali Konrad Krajewski, Mkuu wa Sadaka ya Kitume na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa muda wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu. Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari kuhusiana na utume huo nchini Ukraine, wamebainisha kuwa Kardinali Krajewski tarehe 7 Machi yuko katika safari kuelekea mpaka kati ya Poland na Ukraine mahali ambapo atatembelea wakimbizi na watu wa kujitolea katika vituo vya wakimbizi na katika nyumba.  Wakati Kardinali Michael Czerny atafika huko Hungeria siku ya  Jumanne asubuhi tarehe 8 Machi ili kutembelea baadhi ya vituo vya mapokezi ya wakimbizi kutoka Ukraine. Wote wawili wanaelekea huko Ukraine  kulingana na hali halisi ambayo inatarajiwa kuwafikia Nchi hiyo kwa siku zijazo.

Wakimbizi wa Ukraine wakiwa katika vituo vya muda katika shule  moja ya Hungeria
Wakimbizi wa Ukraine wakiwa katika vituo vya muda katika shule moja ya Hungeria

Makardinali hao wataweza kuwapelekea msaaada wenye kuhitaji na kuwakilisha si tu Papa lakini pia  watu wote wakristo ambao wanapenda kuelezea mshikamano kwa watu wa Ukraine kwa kuunga mkono maneno ya Papa aliyesema:  “ simamisheni vita kwani ni wazimu! Tafadhali simamisheni vita! Tazameni ukatili huu. Nchini Ukraine mito ya damu inatiririka na machozi. Hiyo sio operesheni ya kivita, bali ni vita ambavyo vinapanda kifo, uharibifu na shida” . (Papa katika Sala ya Malaika wa Bwana 6 Machi 2022). Papa Francisko alithibitisha kuwa “waathirka daima wanazidi kuwa idadi kubwa na kama wale wanaokimbia  hasa mama na watoto. Katika Nchi iliyokwisha teseka kila saa, kuna uhitaji wa msaada wa kibinadamu.

Ninatoa wito wangi kwa upya kwa sababu waweze kuhakikishiwa kweli mikondo ya kibinadamu na kuhakikishwa uhakika  wa kuingiza misaada katika maeneo yaliyovamiwa ili wasaidie  maisha ya kaka na dada wanaoteseka na kuishi katika mabomu na hofu. Ninashukuu wale ambao wanaendelea kukaribisha wakimbizi. Hasa ninaomba mashambulizi ya silaha yakome na kuanzishwa mchakato wa mazungumzo, na maana nzuri ishinde. Na tuheshimu sheria za kimataifa tena”.

Waamini wakiwa Uwanja wa Mtakatifu Petro kusali Sala ya Malaika wa Bwana na Papa
Waamini wakiwa Uwanja wa Mtakatifu Petro kusali Sala ya Malaika wa Bwana na Papa

Ishara ya Papa Francisko inataka kuwa wito hata kwa upya wa kuwa na umakini wa hali nyingi zinazofanana nazo ulimwenguni kote. Kama alivyokuwa amesema Papa Dominika iliyotangulia kwamba: “Huku mioyo yetu ikiwa imeteseka kwa kile kinachotokea Ukraine, tusisahau vita katika sehemu nyingine za dunia, kama vile Yemen, Siria, Ethiopia…  ninarudia: fungeni silaha hizo! Mungu yuko pamoja na wapatanishi, si pamoja na wale wanaotumia jeuri”. (Papa Malaika wa Bwana, 27.02).

Papa Francisko amerudia kuta wito wa kusitisha vita wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana
Papa Francisko amerudia kuta wito wa kusitisha vita wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana

Kardinali M. Czerny ataendelea kupitia hali hizi za huzuni kati ya mateso ya wanaukraine ambayo yamesahauliwa. Lakini zaidi ya hayo, ataibua  umakini hasa kwa wasiwasi wambao umejitokeza kwa  Waafrika na Watu wa Asia wanaoishi nchini Ukraine, ambao pia wanakabiliwa na woga na kufukuzwa na wanahisi  kutopata  hifadhi bila kubaguliwa. Pia kuna ripoti za kutisha za kuongezeka kwa biashara ya binadamu na shughuli za biashara ya wahamiaji mipakani na katika nchi jirani. Kwa kuwa wengi wa watu wanaokimbia ni waamini, atathibitisha juu ya  msaada wa kidini unapaswa kutolewa kwa watu wote, kwa kuzingatia mtazamo wa kiekumene na wa kidini. Hatimaye, pamoja na jitihada za kupongezwa za kutoa majibu ya kibinadamu na kuandaa mikonodo ya kibinadamu, kuna haja kubwa ya uratibu, mpangilio mzuri na mkakati wa pamoja, ili kukumbatia mateso ya watu na kutoa misaada yenye ufanisi.

07 March 2022, 15:18