Shiriki sala ya masaa 24 siku ya Alhamisi na Ijumaa 24-25 Machi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ijumaa tarehe 25 Machi 2022, saa 11 Jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa Francisko anatarajia kuongoza ibada ya toba na ufunguzi wa utamaduni wa masaa 24 ya sala ya kuabudu kwa Bwana inayohamasisha ulimwenguni kote na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Unjilishaji Mpya. Kuhusiana na toba na sala ya masaa 24 inaongozwa na kauli mbiu: “Kwa njia yake tumepokea msamaha” (Kol 1,13-14). Katika fursa hiyo mara baada ya maungamo, Baba Mtakatifu ataiweka wakfu kwa Moyo safi wa Bikira Maria nchi ya Urussi na Ukraine.
Kwa maelezo zaidi bonyeza:
http://www.pcpne.va/content/pcpne/it/news/biglietti.html
Masaa ya sala na toba:
Alhamisi 24 Machi 2022: kuanzia saa 2.30-7.30 na 9.00-11.30 asubuhi.
Ijumaa 25 Machi 2022: Kuanzia saa 2.30-7.30 na 9.00-10.00 jioni.