Papa Francisko:wanawake walinzi wa ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika kilele cha Siku ya Kimataifa ya wanawake 2022 iadhimishwayo kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka , imeangukia katika vita vilivyo wazi, kwa kuongezea vile ambavyo vimegawanyika vipande vipande ulimwenguni. Ni machozi mengi yanayotitirika kutoka machoni mwa wanawake wengi wakati wanawaaga waume zao mbele yao wakati mikononi wakiwa wameshikilia watoto wao ambao wanaogopa, wanawake wajasiri ambao wanapaza sauti zao katika viwanja wakisema hapana kufanya vita; wanawake ambao wako tayari tayari kuwasaidia wanajeshai ambao wangekuwa maadui lakini wakati huo huo wakiwasaidia vijana wenye hofu na wadhaifu. Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine umeonesha nyuso za wanawake walivyo leo hii, kwamba wanaweza kutunza kweli, ni wenye nguvu , wa dhati na kielelezo cha upendo ambao licha ya machungu, lakini upendo huo unafanya kuwa nyumba pia kimbilio.
Mama Maria anatafakari na kulinda
Wanawake hawa, wawe wa Urusi au Ukraine,na katika Ulimwengu leo hii unawatazama katika Siku ya Kimataifa ambayo imewekwa kwa ajili yao wote na katika maneno ya Papa Francisko ambayo mara nyingi ametamka , utafikiri yameshonwa nyuma yao, katika ngozi yao iliyoungua kwa huzuni mkubwa sana. Katika fursa ya Siku kuu ya Maria Mama wa Mungu, ambayo imewakwa na Mama Kanisa katika siku ya kwanza ya mwaka, Baba Mtakatifu alikumbusha kuwa: “Maria, Mwanamke ambaye analinda akiwa anatafakari ni Mama wote wanaotazama ulimwengu, si kwa ajili ya kuunyonya, lakini uwe na maisha, kwa kuutazama kwa moyo, na wanaweza kuzingatia kwa pamoja ndoto na udhabiti wake”.
Vurugu dhidi ya wanawake ni matatizo ya kishetani
Na wakati mama wengi wanatoa maisha na wanawake wanalinda ambapo inawezekana kabisa kufanya lolote hasa la kuhamasisha mama na kulinda wanawake. Papa alikumbuka ni vurugu ngapi zilizopo mbele ya wanawake! Alibainisha kwamba “ Kumdhuru mwanamke ni kukashifu Mungu ambaye alimuumba na kubeba ubinadamu, na si kutoka kwa Malaika, moja kwa moja, bali kutoka kwa mwanamke. Kama mwanamke, Kanisa ni mwanamke ambaye tunza ubinadamu wa watoto wake”. Vuguru kwa wanawake ni matatizo kabisa ya kishetani, alisema hivyo Papa Francisko katika mahojiano na televisheni ya Mediaset mnamo mwezi Desemba 2021, baada ya kusikiliza Giovanna ambaye nyuma ya mabega yake alikuwa na familia ngumu.
Ni hadhi gani ya wanawake wanaopigwa au kutumiwa
“Je ni hadhi gani ya wanawake wanaopigwa au kutumiwa? Papa aliuliza na kuongeza kusema: “Ninaijiwa na picha moja unapokuwa unaingia katika Kanisa Kuu la mtakatifu Petro kulia kuna picha ya Mama wa Huruma aliye jinyenyekeza mbele ya mtoto wake akiwa uchi, aliyesulibiwa, aliye kati kati ya macho ya wabaya. Lakini yeye hakupoteza hadhi yake na kutazama picha katika wakati mgumu kama ulivyo wa kwako wa kudhalalishwa na mahali ambapo unahisi kupoteza hadhi, kwa kutazama ile picha inatupatia nguvu. Tazama Mama, baki na ile picha ya ujasiri”. Papa Francisko kwa hakika Papa anasema mara kwa mara maneno mengi kuhusu wanawake. Mwanamke analeta maelewano, mwanamke ni maelewano, ni shairi, ni uzuri bila yeye ulimwengu usingekuwa hivi ilivyo mzuri…